Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka amesema Kambi za Kitaaluma mkoani Simiyu kwa wanafunzi wa darasa
la saba, kidato cha nne na kidato cha Sita, ambayo ni madarasa yanayofanya Mitihani
ya Taifa ya kuhitimu elimu ya Msingi na Sekondari zitakuwa endelevu.
Mtaka amesema hayo Aprili 28,
2019 wakati akihitimisha Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha sita
iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa,
iliyohusisha wanafunzi 1166 kutoka katika shule 12 mkoani hapa.
Amesema Mkoa utaendelea kufanya
jitihada na kuboresha zaidi kambi hizo huku akieleza kuwa ameshawaelekeza Wakurugenzi
wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga fedha kwa ajili ya motisha kwa walimu na
wanafunzi watakaokuwa wakifanya vizuri.
“Kambi za kitaaluma zitaendelea kuwepo katika kipindi chote nitakacho
kuwepo na tutaendelea kuboresha; mwaka huu nimewaambia Wakurugenzi ni lazima
kila Halmashauri itenge fedha kwa ajili ya motisha katika elimu, motisha kwa walimu
na wanafunzi wanaofanya vizuri” alisema Mtaka.
Katika hatua nyingine Mtaka amewashukuru walimu,
wanafunzi na wadau mbalimbali waliochangia kufanikisha kambi ya kidato cha
sita, huku akiwasisitiza wanafunzi wa hao kuendeleza juhudi walizozionesha wakiwa
kambini na kutumia mbinu walizopewa na walimu mahiri ili waweze kufanya
vizuri mitihani yao ya mwisho.
Naye Mchungaji wa Kanisa la Waadventista
Wasabato kutoka Jijini Mwanza, Nicodemo Ntabindi amewaonya wanafunzi wa Kidato
cha sita kutojihusisha na masuala ya mapenzi badala yake wajikite katika masomo
tu kwa sasa ili waweze kufikia ndoto zao.
Kwa upande wao wanafunzi waliokuwepo
katika kambi hiyo ya Kitaaluma wamesema kambi hiyo imekuwa msaada kwa wanafunzi
kwa kuwa imechangia kuwasaidia kupata ufumbuzi wa mada ngumu zilizokuwa
zinawapa shida na kuahidi kufanya vizuri katika mtihani wa Taifa kutokana na
namna walivyoandaliwa vema.
“Tunashukuru uwepo wa kambi hii
maana imetusaidia kupata maarifa ya namna ya kujibu maswali kwenye mitihani, lakini
tumeweza kusaidiwa na walimu kutatua mada ngumu ambazo zilikuwa zinatushinda,
ninaamini kwa namna tulivyoandaliwa hatutamuangusha Mkuu wetu wa Mkoa” alisema
mwanafunzi Farida Omary.
“Kambi hizi hazijafanyika popote
hapa nchini tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa kwa kuja na wazo la kuwa na kambi kwa
sababu tumejifunza mengi, tumekutana na wenzetu wa shule mbalimbali hapa mkoani
kwetu na tukapata maarifa ambayo awali hatukuwa nayo, tuna imani tufanya vizuri
“ alisema mwanafunzi Casto Nyakarungu.
Katika kambi hii Ofisi ya Mkuu wa
mkoa wa Simiyu, imetoa shilingi milioni 12 kwa ajili ya motisha kwa walimu waliokuwa
wakifundisha kambini hapo na imeahidi kutoa shilingi milioni nne kwa mwanafunzi
atakayepata ‘division one, pointi tatu’ na kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi
bora Kitaifa.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa.wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka akizungumza na wanafunzi wa Kidato Cha Sita Mkoani humo, wakati wa
kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi
mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28,
2019.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato Cha Sita
Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma ya
Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.
Aliyekuwa mlezi(Patron) wa kambi ya
kitaaluma ya kidato cha sita kwa wanafunzi wa kidato cha Sita mkoani Simiyu,
Mwl.Pimbili Chalya kutoka Mwandoya, akitoa tathmini ya kambi hiyo , iliyofanyika
kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na
kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Joseph Mathias Mwanafunzi kutoka Shule
ya Sekondari Bariadi akitoa tathmini ya kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita
mkoani Simiyu, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.
Anthony Mtaka.
Mwanafunzi wa kidato cha Sita Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa, akitoa burudani ya wimbo, wakati wa kufunga Kambi
ya Kitaaluma kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu
wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista
Wasabato kutoka Mkoani Mwanza, Nicodemo Ntabindi akizungumza na wanafunzi wa
Kidato Cha Sita Mkoani Simiyu, wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma kwa
wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.
Anthony Mtaka.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana
Maswa, Mwl. Kuyunga Jackson akitoa tathmini ya kambi ya kitaaluma ya kidato cha
sita mkoani Simiyu, wakati wa kufunga kambi hiyo , iliyofanyika kwa takribani
mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili
28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Mchungaji wa Kanisa la Waadventista
Wasabato kutoka Mkoani Mwanza, Nicodemo Ntabindi (wa pili kushoto) akiongoza
maombi kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha sita mkoani Simiyu wanaotarajia
kuanza Mtihani wao wa taifa Mei 06, 2019 wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma
kwa wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa
huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Wakuu wa Shule za Sekondari za Kidato
cha Sita mkoani Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka
(hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita , wakati
wa kufunga Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani
mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili
28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita
mkoani Simiyu wakiimba wimbo wa kuwapongeza viongozi, walimu na wanafunzi
wenzao mkoani humo kwa kufanikisha Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao,
iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana
Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato Cha Sita
Mkoani Simiyu wakinyosha mikonoyao juu kukubali kuwa watafanya vizuri mara
baada ya kuhojiwa na Mkuu wa Mkoa huo,
Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) ikiwa wako tayari kufanya vizuri alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga
Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja
katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 .
Vijana wa Skauti wakimvisha skafu Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kabla ya Mkuu huyo wa Mkoa kuhitimisha Kambi ya Kitaaluma ya Wanafunzi wa
Kidato cha Sita Aprili 28, 2019 ,
iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana
Maswa.
Mmoja wa walimu mahiri akitoa tathmini ya
kambi ya kitaaluma ya kidato cha sita mkoani Simiyu wakati wa kufunga kambi
hiyo , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.
Anthony Mtaka.
Wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani
Simiyu, wakiwa katika maombi maalum wakati wa kufunga kambi ya kitaaluma kwa
wanafunzi hao , iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa
huo, Mhe. Anthony Mtaka.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato Cha Sita
Mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa kufunga Kambi ya Kitaaluma ya
Wanafunzi hao, iliyofanyika kwa takribani mwezi mmoja katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28, 2019 na Mkuu wa Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka akimkabidhi cheti cha pongezi kwa mmoja wa walimu Mwl. Makame Makame ikiwa
ni kutambua mchango wake katika kuwafundisha wanafunzi kwenye Kambi ya
Kitaaluma ya Wanafunzi wa Kidato cha Sita, iliyofanyika kwa takribani mwezi
mmoja katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na kuhitimishwa Aprili 28,
2019.