Mamlaka
ya Chakula na Dawa(TFDA) imetoa msaada wa katoni 111 za taulo za kike zenye thamani
ya shilingi milioni tano, kwa wanafunzi wa kike 538 walio katika kambi ya
kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019, inayoendelea katika Shule
ya Sekondari ya wasichana Maswa Mkoani hapa.
Akikabidhi
msaada huo Aprili 05, 2019 Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama, amesema Mamlaka hiyo imetoa
msaada huo kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuinua elimu mkoani Simiyu,
ili kuwasaidia watoto wa kike wasome kwa uhuru na utulivu kambini hapo hususani
wakati wa hedhi.
Amesema TFDA
kama wadau wa mkoa wataendelea kushirikiana na Serikali mkoani Simiyu katika
sekta ya elimu na masuala mengine ya Maendeleo, huku akiwasisitiza wanafunzi walio kambini kusoma kwa bidii na kutumia
vizuri muda walionao ili waweze kufikia
malengo yao.
Akipokea
msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Mamlaka hiyo
kwa msaada uliotolewa kwa wanafunzi wa kike, huku akiwasisitiza wanafunzi
wote walio katika kambi ya kitaaluma kusoma kwa bidii.
Aidha,
Mtaka amewashukuru wadau mbalimbali ambao wameendelea kutoa michango kwa ajili
ya kufaninisha kambi ya kitaaluma inayoendelea
mkoani humo, huku akiahidi kuwa wadau wote waliochangia watatambuliwa na kupewa
vyeti.
Katika
hatua nyingine Mtaka ametoa ufafanuzi kwa wadau na wananchi kuhusu utaratibu wa
kambi za kitaaluma mkoani Simiyu, kwamba kambi hizi hufanyika katika ngazi za
shule na baadaye huundwa kambi moja ya mkoa kuwakutanisha wanafunzi kwa ajili
ya kambi ya mkoa.
“Kambi
za Kitaaluma kwenye mkoa zilianza muda mrefu lakini kama mkoa tumeweka
utaratibu wa kuwa na kambi moja ya kimkoa inayounganisha shule zote za kidato
cha sita; kambi za kidato cha nne nazo zinaendelea kwa hiyo tutakapofika mwezi
wa saba tutaanza kuunganisha shule, kama tulivyofanya mwaka jana tuliunganisha
shule 24 pale Simiyu Sekondari” alisema.
Nao
wanafunzi wa kike wa Kidato cha Sita walio katika Kambi hiyo ya Kitaaluma wameishukuru
Mamlaka ya Chakula na Dawa kwa msaada huo ambao wamesema utawasaidia sana kusoma
kwa uhuru na kujiamini zaidi wakati wa hedhi.
“Tulikuwa
tunakumbana na changamoto ya kutokuwa na amani na kushindwa kujiamini wakati wa
hedhi kwa hiyo hata kusoma tulikuwa tunasoma lakini tunakuwa na wasiwasi, kupitia
msaada huu ‘tutakuwa comfortable ‘ (tutakuwa na amani) kabisa tunaishukuru sana
TFDA”Mwanaidi Halfan.
“Huu
msaada tuliopata utanisaidia kufikia ndoto zangu maana wasichana wengi
wanapokosa taulo hizi za kike wanashindwa kusoma, wanakuwa na hofu wengine hata
darasani hawaendi, lakini kwa kuwa wote tumepata msaada huu najua muda tutakao
kuwa hapa tutakuwa huru kujisomea hatutaogopa tena maana zinatuhakikishia
usalama tunapokuwa hedhi” alisema Hidaya Simba
Jumla ya
wanafunzi 1166 wa kidato cha Sita mwaka 2019 kutoka shule 12 mkoani Simiyu wako
katika kambi ya kitaaluma kwa siku 28 katika shule ya sekondari Maswa, kwa
ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa unaotarajia kufanyika mwezi Mei, 2019.
MWISHO
Baadhi ya wanafunzi wa
kikewa kidato cha Sita mwaka 2019 mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru
Mwasulama (katikati), mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike zilizotolewa
kwa ajili yao na mamlaka hiyo, katika kambi
ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kushoto)akiwa na baadhi ya wanafunzi wa kike wa
kidato cha sita mkoani humo, wakipokea sehemu ya msaada wa taulo za kike
zilizotolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kuwasilishwa na Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru
Mwasulama (wa tatu kulia), katika kambi
ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru
Mwasulama (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka(kushoto) na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na baadhi ya wanafunzi sehemu ya maboksi ya taulo za kike ambazo
zimetolewa msaada kwa wanafunzi kike walio kwenye kambi ya kitaaluma ya
wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari
ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
Mwanafunzi
Winfrida Nasoro kutoka Shule ya Sekondari Dutwa, akitoa shukrani kwa niaba ya
wenzake mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike uliotolewa na Mamlaka ya
Chakula na Dawa(TFDA) kwa wanafunzi wa kike 538 walio katika kambi ya Kitaaluma
ya Kidato cha Sita inayoendelea wilayani Maswa.
Sehemu ya katoni za
taulo za kike zilizotolewa msaada Aprili
05, 2019 na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kwa wanafunzi wa kike 538 walio
katika kambi ya Kitaaluma ya Kidato cha Sita mwaka 2019 Mkoani Simiyu
inayoendelea wilayani Maswa.
Baadhi ya wanafunzi wa
kikewa kidato cha Sita mwaka 2019 mkoani Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru
Mwasulama (katikati), mara baada ya kupokea msaada wa taulo za kike zilizotolewa
kwa ajili yao na mamlaka hiyo, katika kambi
ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanafunzi wa
kike wa kidato cha Sita mwaka 2019 mkoani Simiyu wakishangilia jambo kabla ya kupokea
msaada wa taulo za kike zilizotolewa kwa ajili yao na Mamlaka ya chakula na
dawa(TFDA) katika kambi ya kitaaluma ya wanafunzi
wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akizungumza jambo na baadhi ya wanafunzi wa kike
wa idato cha sita mkoani humo, mara baada ya waanfunzi hao kupokea msada wa
taulo za kike zilizotolewa msaada na Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) kwa
wanafunzi wa kike takribani 538 walio katika Kambi ya Kitaaluma ya Kidato cha
Sita mwaka 2019 inayoendelea Wilayani Maswa, (wa pili kushoto) Mwakilishi wa
Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Kanda ya Ziwa, Bi. Nuru Mwasulama.
Diwani wa Viti Maalum
wilayani Maswa(kushoto) na baadhi ya wanafunzi wakipokea sehemu ya msaada wa
taulo za kike zilizotolewa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na kuwasilishwa
na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Ziwa,
Bi. Nuru Mwasulama (kulia), katika kambi
ya kitaaluma ya wanafunzi wa kidato cha sita mwaka 2019 inayoendelea katika
Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akiaganana na baadhi ya wanafunzi Aprili 05, 2019 mara
baada ya kupokea msaada wa taulo za kike uliotolewa na Mamlaka ya Chakula na
Dawa (TFDA) kwa wanafunzi wa kike walioko katika kambi ya Kitaaluma ya Kidato
cha Sita mwaka 2019 inayoendelea wilayani Maswa.
0 comments:
Post a Comment