Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki ametoa
wito kwa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista
Wasabato Tanzania (ATAPE) na wawekezaji
wengine wazawa kuchangamkia fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini na
kusajili miradi yao ya Uwekezaji katika
Tume ya uwekezaji ya Taifa (TIC).
Kairuki ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa 20
wa chama cha wanataaluma na wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania (ATAPE) Mjini Bariadi, ambapo
amebainisha kuwa kwa mwaka huu 2019 wawekezaji wazawa zaidi ya asilimia 72
wamesajili miradi yao ya uwekezaji TIC.
“ Kwa mwaka huu peke yake tumepata wawekezaji wazawa waliosajili
miradi yao ya uwekezaji TIC zaidi ya asilimia 72, hii inanipa faraja sana kama
waziri wa nchi ninayesimamia uwekezaji ninapoona Watanzania wenzangu
wanachangamkia fursa”
"Naomba mchangamkie fursa hizo kwa sababu
wawekezaji wa nje tunapenda waje tu endapo watakuja kuungana nasi kwenye mtaji,
kubadilishana nasi ujuzi na uzoefu " alisema Kairuki.
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira
ya biashara, uwekezaji na kuweka vipaumbele kwa ajili ya kuvutia wawekezaji katika
sekta ambazo zitakuwana athari na tija kubwa kiuchumi kwa wananchi, ili
kuimarisha minyororo ya thamani katika kilimo,uvuvi, na mifugo ambayo ni maeneo
yanayoajiri Watanzania wengi zaidi.
Aidha, Waziri Kairuki amezitaja sekta nyingine za
kipaumbele kuwa ni uzalishaji wa mafuta
ya kula kwa kutumia mbegu zinazozalishwa nchini, uzalishaji wa sukari,
uzalishaji wa dawa za binadamu, vifaa tiba na kemikali, ujenzi wa miundombinu
ya uvuvi wa kisasa, viwanda vya kuchakata samaki, kusindika nyama, viwanda vya
kubangua korosho, viwanda vitakavyotumia pamba na viwanda vya pembejeo na mbolea.
Katika hatua nyingine Waziri Kairuki ameipongeza ATAPE
kwa jinsi inavyoshirikiana na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali za
kijamii ikiwemo sekta ya afya, elimu, maji pamoja na huduma nyingine.
Kairuki amesema serikali pekee haiwezi kutatua
changamoto zote hivyo kwa kushirikiana na wadau ikiwemo taasisi za dini
wanaweza kuwahudumia wananchi na kuleta mabadiliko chanya ikiwa ni pamoja
na kuhubiri amani, huku akisisitiza kuwa masomo ya ujasiriamali yanayotolewa
kwa wana ATAPE wayatumie kwa manufaa ya kanisa na jamii kwa ujumla.
Awali akimkatibisha waziri Kairuki, mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkutano huo umewasaidia watu wa
Simiyu kukutana na watu wa maeneo mengine hatua iliyopelekea
kubadilishana uzoefu sambamba na kuongeza na kupata masoko mapya .
‘’watu wetu wameongeza wigo wa masoko, mmebadilishana
uzoefu ....huu ni mkoa wa kibiashara na ni mkoa wenye fursa nyingi; tunajenga tawi la chuo cha usimamizi wa fedha
(IFM) hivyo ninawaalika wafanyabiashara na Watanzania wote kuja kuwekeza ujenzi
wa hosteli eneo lile linalojengwa tawi hilo"alisisitiza Mtaka.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa ATAPE Freddie Manento
amesema kwa miaka mitatu ATAPE imewekeza miradi ya bilioni 1.2 katika miradi
yenye manufaa kwa kanisa, wanajamii na wana ATAPE.
Alisema wamewekeza kwenye miradi ya maji kwenye maeneo
yenye uhitaji mkubwa, miradi ya miti ya matund), korosho na miradi ya mashamba
ya mihogo kwa kutengeneza ajira na faida katika vijiji walivyolima mashamba
yao.
‘’Wana ATAPE wamejitoa kwelikweli na wameitikia dhana
yetu ya kutumia vipaji na rasilimali zetu kwa ajili ya kazi ya MUNGU, hii iko
katika mathayo 28;19, 20…hii ndio dhana yao’’ alisema Manento.
Mkutano wa Wanataaluma na Wajasiriamali (ATAPE) kutoka
kanisa la Waadventista Wasabato umefanyika mkoani Simiyu kwa muda wa siku sita
ambapo umehudhuriwa na wananchama zaidi ya 1500.
.....MWISHO....
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki akizungumza na Wanachama wa
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi,
Aprili 20, 2019.
Baadhi ya Wanachama wa
Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE), wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji,
Mhe. Angela Kairuki wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi,
Aprili 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.
Anthony Mtaka akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa
kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE), Bw. Freddie Manento akimtambulisha rasmi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki (mwenye skafu) kama mwanachama mpya mbele ya
wanachama, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho Mjini Bariadi,
2019.
Kutoka kushoto Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki, Msaidizi wa
Askofu Mkuu wa Kanisa la Waadventista Wasabato, Ukanda wa Afrika Mashariki na
Kati(nchi 11) , Mchungaji Emanuel Pelote, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe. Anthony
Mtaka na Mchungaji Joshua Njuguna kutoka nchini Kenya, wakifurahia jambo wakati
wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa
la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), hicho Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.
Anthony Mtaka(mwenye shati la Kitengekushoto) akiimba pamoja na wanakwaya ya
Bulka kutoka Jijini Arusha, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE), hicho Mjini Bariadi,
Aprili 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.
Anthony Mtaka akionesha ngao/tuzo alichopewa na Chama cha Wanataaluma na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), kama
shukrani ya kuwezesha mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho kufanyika Mjini Bariadi
mkoani Simiyu, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho Mjini
Bariadi, 2019.
Askofu wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la Kaskazini , Dkt. Godwin Lekondayo
akizungumza na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama
hicho Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka, wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),Mjini
Bariadi, Aprili 20, 2019 (wa pili kulia) Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Jimbo Kuu la Kusini, Mch. Mark Malekana na kulia ni Katibu wa ATAPE James Laban.
Vijana
watenegenza njia wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania wakitoa heshima
kwa viongozi kablaya kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE),Mjini Bariadi,
Aprili 20, 2019.
Kutoka kushoto ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki ,Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu,Mhe. Anthony Mtaka, Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu
la Kusini, Mch. Mark Malekana na Katibu wa Chama cha Wanataaluma na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), James Laban
wakifuatailia jambo kwa makini wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa ATAPE Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akimsalimia Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki mara baada ya kuwasili Mjini
Bariadi kwa ajili ya kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), Aprili 20,
2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki (mwenye skafu) akimkabidhi Askofu
wa Kanisa la Waadventista Wasabato Jimbo Kuu la Kusini, Mch. Mark Malekana
ngao/tuzo iliyotolewa na Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE) kutambua mchango wake, wakati wa kufunga
mkutano mkuu wa ATAPE Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Kwaya
ya Kanisa la Waadventista Wasabato kutoka Suguti wilayani Musoma Mkoani Mara
wakiimba wakati wa kufunga mkutano wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na
Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE) , Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Kwaya ya Kanisa la
Waadventista Wasabato kutoka Nyarugusu Mkoani Geita wakiimba wakati wa kufunga
mkutano wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la
Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE) , Mjini
Bariadi, Aprili 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.
Anthony Mtaka akifurahia jambo na Mchungaji Dkt. Joshua Njuguna kutoka nchini
Kenya wakati wa kufunga mkutano wa 20 wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali
wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE) , Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki akizungumza na Wanachama wa Chama
cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi,
Aprili 20, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.
Anthony Mtaka(kulia) akiteta jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
Uwezeshaji, Mhe. Angela Kairuki, wakati wa kufunga mkutano wa 20 wa Chama cha
Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE)
, Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Baadhi ya wadau(waliosimama) waliotoa Ng’ombe 12 kwa ajili ya chakula cha wanachama wakati wa mkutano wa 20
wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE) , kaam
walivyotambulishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka wakati wa
kufunga mkutano huo Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
PICHA T:-Baadhi ya
viongozi wa Serikali na Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa
la Waadventista Wasabato Tanzania(ATAPE), wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki wakati wa kufunga mkutano mkuu wa
20 wa Chama hicho Mjini Bariadi, Aprili 20, 2019.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angela Kairuki akizungumza na Wanachama
wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali wa Kanisa la Waadventista Wasabato
Tanzania(ATAPE), wakati wa kufunga mkutano mkuu wa 20 wa Chama hicho Mjini Bariadi,
Aprili 20, 2019
0 comments:
Post a Comment