Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali akiweka jiwe la msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari
tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi,wakati wa mbio za
mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ameweka Jiwe la Msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi, ambayo kikamilika kwake kutawapunguzia wanafunzi wa Kata ya Isanga kutembea Mwendo mrefu ambapo sasa wanasoma katika Shule za Sekondari Biashara Kata ya Sima na Kidinda Kata ya Bariadi.
Awali akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru,
Ndg. Mzee Mkongea Ali, Mwenyekiti wa Mtaa wa Majahida, Ndimi Silanga amesema
vyumba hivyo vimejengwa kwa gahrama ya shilingi milioni 97 ikiwa ni michango ya
wananchi, wadau mbalimbali wa elimu pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhe.
Andrew Chenge.
Kwa upannde wake Elizabeth Jailo ambaye ni mkazi wa Majahida na
mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Biashara amesema kujengwa kwa shule hiyo
kutasaidia kupunguza changamoto ya upungufu wa madarasa katika shule anayosoma
maana wanafunzi wa shule hiyo wanaotoka karibu na Shule mpya watasoma hapo na
kupunguziwa adha ya kutembea takribani kilometa 15 kwa siku.
Pamoja na kuweka Jiwe la Msingi Madarasa hayo, Mwenge wa Uhuru
umepitia miradi mbalimbali ikiwepo kufungua Nyumba ya Kulala wageni Nghunde
Classic Lodge, kuona mradi wa Uhifadhi wa Mazingira wa Msitu wa Kanisa Katoliki
Old Maswa Sesele.
Aidha,umefungua jengo la Wodi ya Wazazi Zahanati ya Mwakibuga na
kuona shughuli za wanawake Wajasiriamali pamoja na kuzindua klabu ya kupinga
rushwa na klabu ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya shule ya Sekondari
Kusekwa.
MWISHO
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali akiweka jiwe la msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari
tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi,wakati wa mbio za
mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Isanga wakishuhidia uwekaji wa
jiwe la msingi katika Madarasa sita ya Shule ya Sekondari tarajiwa ya Dkt. Yohana
Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi,wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini
Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali akikagua moja ya vyumba sita vya madarasa Shule ya Sekondari
tarajiwa ya Dkt. Yohana Balele iliyopo Majahida Mjini Bariadi,wakati wa mbio za
mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru na askari wa FFU wakiondoka baada ya
kufungua Nyumba ya Kulala wageni Nghunde Classic Lodge wakati wa mbio za mwenge
wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali akizindua Jengo la Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Mwakibuga, wakati
wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Jengo la Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Mwakibuga
lililozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali akipewa maelezo kuhusu namna hifadhiya msitu wa Sesele
inavyotunzwa, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mjini Bariadi Mei 25, 2019.
0 comments:
Post a Comment