Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 umeanza mbio zake Mei 22,
2019 Mkoani Simiyu ambapo unatarajia kupitia miradi 34 kutoka katika sekta
binafsi, maji, elimu, afya, viwanda, kilimo, barabara, maendeleo ya jamii na
hifadhi ya mazingira ambayo ina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 8.8.
Akizungumza mara baada ya kupokea Mwenge wa Uhuru
kutoka Mwanza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema katika thamani
hiyo ya miradi ambayo ni shilingi 8, 878,598,412.25 shilingi 904,170,725.00 ni
nguvu za wananchi, Halmashauri shilingi 428, 403,532.63, Serikali Kuu ni
shilingi 5, 992,582,072.37, wahisani shilingi 1,256,475,082.25 na sekta Binafsi
shilingi 296,967,000.00
Akizungumzia
Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 “MAJI NA HAKI YA KILA MTU TUTUNZE VYANZO
VYAKE NA TUKUMBUKE KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA” Mtaka
amesema, wastani wa upatikanaji maji Simiyu ni asilimia 50.4 ambao unahudumia
wakazi 817, 968 na kubainisha kuwa
Serikali inaendelea kuhamasiha wananchi kulinda vyanzo vya maji ili kuwezesha
upatikanaji wa huduma hiyo.
Aidha,
amesema Mkoa wa Simiyu umejipanga na unaendelea kuandaa mazingira mazuri ya
amani na utulivu, yatakayowezesha wananchi kutumia haki yao ya kidemokrasia
kushiriki kikamilifu katika mchakato mzima wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
mwaka 2019.
Kwa
upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea
Ali amewataka viongozi wa mkoa wa Simiyu
na wilaya zote mkoani humo kuhakikisha taarifa zote za miradi ya maendeleobitakayopitiwa
na Mwenge wa uhuru ziwepo eneo la mradi na wataalam wote wanaohusika na miradi
hiyo wawepo.
Baada
ya kupokelewa Mkoani Simiyu Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake wilayani Maswa
ambapo umepitia mradi wa urasimishaji wa makazi Malampaka, ukaguzi wa ujenzi wa
barabara za lami Mjini Maswa, mradi wa maji Nyashimba, Kiwanda cha viazi lishe
Njiapanda, vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja Kijiji cha Mwadila.
Aidha,
Mwenge wa Uhuru ulitembelea na kuona shughuli za wajasiriamali na kutoa hundi
za wajasiriamali, kuzindua klabu za kutokomeza rushwa na dawa za kulevya,
kuzindua kampeni ya tokomeza malaria na kukagua shughuli za utoaji elimu ya
kuhimiza upimaji wa VVU/UKIMWI.
Mwenge
wa Uhuru takimbiza kwa mua wa siku sita mkoani Simiyu Mei 22 mpaka Mei 27, 2019
na Mei 28, 2019 utakabidhiwa mkoani Mara.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye
fulana nyeupe) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.
John Mongela katika kijiji cha Jihu wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(mwenye
fulana nyeupe) akipokea hati ya makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. John Mongela katika kijiji cha Jihu wilayani Maswa, Mei
22, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia)
akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif
Shekalaghe katika kijiji cha Jihu
wilayani Maswa, Mei 22, 2019 ikiwa ndiyo wilaya ya kwanza kuanza Mbio za Mwenge
wa Uhuru mkoani Simiyu.
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Maswa akitoa maelezo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge
wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kabla ya kuweka jiwe la
msingi mradi maji wa Nyashimba katika Kijiji cha Nyashimba wilayani Maswa, Mei
22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka
2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akifungua vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja
ya mwalimu Mkuu katika shule ya
sekondari Mwadila Mei 22, 2019.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiangali
baadhi ya machapisho yanayotumika na wanachama wa Klabu yaMapambano dhidi ya
Rushwa katika shule ya sekondari Lalago wilayani Maswa kutoa elimu ya vita
dhidi ya rushwa kabla ya kuzindua klabu hiyo, Mei 22, 2019
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019,
Ndg. Mzee Mkongea Ali(wa nne kushoto) na
wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa wengine wakiangalia mbegu za viazi lishe, kabla ya kuweka jiwe la msingi
Kiwanda cha kusindika Viazilishe katika Kijiji cha Njiapanda wilayani Maswa,
Mei 22, 2019.
Baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi na Vijana wa
Skauti mkoani Simiyu wakipita na Mwenge wa uhuru katika moja ya barabara
zinazojengwa kwenye mtandao wa Kilomita
1.5 katika Mji wa Maswa, ambapo mradi huo ulikaguliwa na Mbio za mwenge wa
Uhuru Mei 22, 2019.
Mbunge wa Maswa mashariki na Naibu Waziri wa Madini,
Mhe. Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi, wakati wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza
na wananchi, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka
2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali(wa pili kulia)
akiwasiliza wanawake wajasiriamali wa wilayani Maswa, wakati alipopita
kukagua kazi zinazofanywa na wanawake hao baada ya kuwezeshwa na Halmashauri
kuwezeshwa mikopo inayotoka na asilimia nne ya mapato ya ndani, wakati wa mbio
za mwenge wa Uhuru wilayani humo Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka
2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimkabidhi hati ya kiwanja Mkazi wa Malampaka, Bw.
Martini Kamuzora mara baada ya kuzindua zoezi la urasimishaji wa makazi ya
wananchi katika Mji wa Malampaka, Mei 22, 2019.
Moja ya mabanda yaliyoandaliwa na Halmashauri ya
Wilaya ya Maswa kutoa elimu kwa wananchi juu ya vita dhidi ya dawa za kulevya
kupitia Klabu ya kupiga vita dawa za kulevya shule ya sekondari Lalago, wakati
wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Mei 22, 2019.
Wanachama wa Klabu ya kupiga vita dawa za kulevya
kutoka shule ya Sekondari Lalago wakitoa maelezo kwa Kiongozi wa mbio za mwenge
wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali, kabla ya kuzinduliwa kwa
klabu hiyo wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo Mei 22, 2019.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ndg. Latifa Khamis
Juwakali akitoa ujumbe wa Mwenge kwa wananchi wa Lalago wilayani Maswa(hawapo
pichani), Mei 22, 2019.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka
2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akizungumza na wanawake wajasiriamali
wanaojihusisha na kilimo cha pamba alipokuwa akikagua kazi wanazofanya wanawake
hao, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani Maswa, Mei 22, 2019.
0 comments:
Post a Comment