Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA),
Mhandisi. Anthony Sanga na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Bennet Contractors Sabato
Boaz kutoka Mwanza, wamesaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo
wilayani Busega utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.8.
Mkataba
wa Mradi huo utakaonufaisha vijiji vya Bukabile, Mwagulanja na Bulima na
kuhudumia wananchi 20,030 , umesainiwa Nyashimo wilayani Busega na kushuhudiwa
na wananchi, viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya Busega na Mkoa wa
Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Akizungumza
na wananchi na viongozi waliofika kushuhudia zoezi hilo Mtaka amemtaka
Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kuzingatia muda na viwango katika utekelezaji wa mradi huo, huku akisisitiza
kuhakikisha mradi huo unawanufaisha wananchi wanaozunguka eneo la mradi kwa
kutoa ajira za muda na ununuzi wa vifaa vya ujenzi.
“Mkataba
unaonesha mradi huu ni wa miezi 15, nikuombe mkandarasi miezi 15ni mingi tungehitaji
tunapoanza maandalizi ya kutengeneza ilani ya CCM mwaka 2020 tuzungumzie utekelezaji
wa ilani siyo mpango; tunahitaji jamii yetu inufaike kupitia mradi huu, vijana
wapate ajira, mama ntilie wapike chakula na baadhi ya vifaa vya ujenzi
vinunuliwe kwenye maduka ya hapa” alisema Mtaka.
Ameongeza
kuwa Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 16.4 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maji wilayani
Busega, ikiwa ni pamoja na Mradi wa Lamadi, Kiloleli, Mwamanyili na ukarabati
wa visima maeneo mbalimbali, ambayo itakapokamilika itaongeza hali ya upatikanaji wa maji safi na salama
Busega kutoka asilimia 39 ya sasa na kufikia asilimia 74.
Naye
Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni amesema pamoja na mradi wa Nyashimo Serikali
inatekeleza miradi mingine ya maji wilayani Busega ukiwepo wa Kiloleri Mradi wa
Lamadi, hivyo akasisitiza wananchi kulinda na kutunza miradi hiyo ili
iwanufaishe.
Nao
wananchi wamesema“Tunashukuru kuletewa huu mradi tulikuwa tunapata adha ya maji
tulikuwa tunanunua kwenye madumu na kufua ziwani, lakini endapo mradi huu uliosainiwa
mkataba leo ukikamilika itakuwa ni neema kwetu hasa sisi wakina mama ambao ndiyo
tunapata tabu zaidi na familia zetu” Sara Nanyori mkazi wa kijiji cha Bulima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi. Anthony
Sanga amesema mradi wa Nyashimo ni utekelezaji
wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli aliyoitoa kwa wananchi na unafadhiliwa kwa asilimia 100 na fedha za Serikali
ya Tanzania.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bennet Contractors(Mkandarasi) Sabato Boaz kutoka
Mwanza, amesema pamoja na kwamba mkataba unaonesha utekelezaji ni miezi 15,
kampuni yake inatarajia kutekeleza kwa ubora na kwa muda mfupi kadri
itakavyowezekana ili kuleta huduma ya
maji safi na salama haraka kwa wananchi wa Nyashimo.
MWISHO
Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA), Mhandisi.
Anthony Sanga (kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bennet Contractors, Sabato
Boaz kutoka Jijini Mwanza wakibadilishana nakala za mkataba waliosaini Mei 10, 2019 wilayani
Busega , kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa
Maji wa Nyashimo na kushuhudiwa na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya
Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye
suti ya rangi ya kijivu) ambao utakaogharimu
zaidi ya shilingi bilioni 1.8
Mkurugenzi Mtendaji wa
Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi.
Anthony Sanga (kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bennet Contractors Sabato Boaz kutoka Jijini Mwanza wakitia saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji wa Nyashimo
Mei 10, 2019 wilayani Busega na kushuhudiwa na viongozi wa Chama na Serikali wa
Wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka(mwenye suti ya rangi ya kijivu) ambao utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni
1.8.
Kutoka kushoto Mkurugenzi
Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza(MWAUWASA),
Mhandisi. Anthony Sanga, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na
Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni
wakielekea eneo maalum la utiaji saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo
wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kutoka Jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi wa
kata ya Nyashimo wakifuatilia zoezi la utiaji
saini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya
MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza,
mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya
Nyashimo.
Mkuu wa Wilaya ya
Busega, Mhe. Tano Mwera akitoa neno la shukrani wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo
wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha
wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mbunge wa Busega, Dkt.
Raphael Chegeni akizungumza na wananchi
wa Kata ya Nyashimo wakati wa kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo
wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha
wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mwananchi kutoka kata
ya Nyashimo akifurahia jambo na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Mickness Mahela wakati
wa zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo
wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha
wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi
ya Viongozi wa Serikali na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA wakifuatilia mambo
mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kabla ya zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi
wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi
Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu
shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya Viongozi wa
Serikali na Wajumbe wa Bodi ya MWAUWASA wakifuatilia mambo mbalimbali
yaliyokuwa yakiendelea kabla ya zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa
maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet
Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na
kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya wananchi wa
Kata ya Nyashimo wakiwa wamejipanga kwa lengo la kutoa kero zao kwa Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) kabla ya kuanza kwa zoezi la kusaini
mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA
na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi
utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka(kulia) akitoa ufafanuzi wa moja ya kero iliyowasilishwa na mkazi
wa Kata ya Nyashimo, kabla ya kushuhudia zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo
wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha
wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Kaimu Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu akitambulisha viongozi wa mkoa walifika
kushuhudia zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo
wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha
wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Busega, Komredi.
kueleza juu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo, kabla ya kushuhudia zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo
wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha
wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Baadhi ya wananchi wa
kata ya Nyashimo wakifuatilia zoezi la kusaini
mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA
na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi
utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyashimo, kabla ya kushuhudia
zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo
wilayani Busega kati ya MWAUWASA na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors
kutoka Jijini Mwanza, mradi utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha
wananchi wa Kata hiyo
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(kulia) akiwahamasisha viongozi kumchangia
mama mwenye uhitaji na pichani ni baadhi ya viongozi waliojitokeza kumsaidia
mama huyo, kabla ya kushuhudia zoezi la kusaini
mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji wa Nyashimo wilayani Busega kati ya MWAUWASA
na Mkandarasi Kampuni ya Bennet Contractors kutoka Jijini Mwanza, mradi
utakaogharimu shilingi bilioni 1.8 na kuwanufaisha wananchi wa Kata ya Nyashimo.
0 comments:
Post a Comment