Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka
amesema Viongozi Mkoani Simiyu wataendelea kufanya kazi
na kuwahudumia wananchi kwa
kuzingatia utawala bora, utawala unaofuata sheria na uongozi wa kuheshimiana na
kusikilizana.
Mtaka ameyasema hayo Mei Mosi, 2019 wakati alipokuwa
akizungumza na wafanyakazi na wananchi mkoani humo katika Maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Kimkoa, yaliyofanyika katika Uwanja wa Nguzonane Wilayani Maswa.
“Tungependa tujenge utumishi ambao ni wa kipekee
sana kwenye mkoa na kila mtumishi aliye kwenye mkoa huu ajisikie fahari kufanya
kazi Simiyu; ahadi yangu kwenu ni kwamba tutaendelea kufanya kazi kwa
kuheshimiana,kusikilizana na kutiana moyo katikati ya changamoto ambazo
watumishi wanazipitia” alisema
Aidha,
amewashukuru wafanyakazi kwa namna walivyojitoa kwa hali na mali kuhakikisha kwamba malengo ya Serikali ya
kuwahudumia wananchi yanatekelezeka na
kusisitiza kuwa mkoa utaendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Vyama vyote vya
wafanyakazi na kuwataka waajiri wote wathamini vipaji vya watumishi wao.
Kwa
upande wake Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw.
Said Mselem ameomba Serikali kushughulikia suala la upandaji wa mishahara na
madaraja kwa watumishi ili kuwaongezea ari na motisha katika kazi.
Katika
hatua nyingine Mselem ameiomba Serikali kuu kuona uwezekano wa kuwabadilishia
mfumo wa malipo ya mshahara watumishi wanaolipwa kupitia mapato ya ndani na
kuanza kuwalipa kupitia HAZINA, ili wawe na uhakika wa kupata mishahara yao na
michango yao ya mifuko ya hifadhi ya jamii iwasilishwe kwa wakati.
Nao
baadhi ya wafanyakazi kutoka vyama tofauti
vya wafanyakazi wamesema Wafanyakazi Mkoani Simiyu wanapenda kazi zao na
wanafanya kazi kwa uadilifu, hivyo wameiomba Serikali iendelee kuboresha mazingira na
kuwasaidia kutatua changamtozao ili waweze kufanya kazi wa uhuru na kujituma
zaidi.
‘Watumishi
tunapenda kazi zetu na tunafanya kwa bidii na uadilifu, tunajua wapo wachache
wanaotuangusha lakini tunaendelea kuwahimiza wawajibike kutimiza azma ya
kuwatumikia wananchi, ombi letu kwa Serikali itukumbuke kwenye kupanda madaraja
wapo ambao hawajapanda toka mwaka 2015” alisema Mwenyekiti CWT Itilima Mwl.
Rehema Shalali.
“Watumishi
wanaolipwa kwa mapato ya ndani wanakutana na changamoto ya mafao yao wanapostaafu,
mafao hayaendi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kuwa wakati maana hawalipwi
mishahara kwa wakati tunamwomba Mhe. Rais aliangalie hili, ili watumishi hao
nao waweze kulipwa na HAZINA moja kwa moja” alisema Sara Kiyuga Mjumbe wa
Baraza Kuu TALGWU Taifa.
Maadhimisho ya Mei Mosi kwa mwaka 2019 yamebebwa na
Kauli Mbiu “ TANZANIA YA UCHUMI WA KATI INAWEZEKANA, WAKATI WA MISHAHARA NA
MASLAHI BORA KWA WAFANYAKAZI NI SASA” ambapo yamefanyika kwa mara ya saba sasa Kimkoa
tangu mkoa wa Simiyu kuanziswa mwezi Machi, 2012.
MWISHO
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kulia) akiimba wimbo wa mshikamano
daima wa Wafanyakazi na baadhi ya viongozi wa Serikali na Vyama vya Wafanyakazi
katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa
Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akipokea Maandamano ya Wafanyakazi
katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika
Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi
ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi
ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi
ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi
ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakiwa kwenye maandamano, katika maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane
wilayani Maswa.
Baadhi
ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakiimba wimbo wa Mshikamano Daima katika
maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
Mei Mosi yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wafanyakazi wa mkoa huo Mei
Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika
Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Katibu
wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Said Mselem
akitambulisha viongozi wa vyama vya wafanyakazi Mei Mosi, 2019
katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika
Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Katibu
wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Simiyu, Bw. Said Mselem akisoma
risala ya wafanyakazi wa mkoa wa Simiyu kwa Mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa
Simiyu,, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho
ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane
wilayani Maswa.
Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt. Seif Shekalaghe akizungumza kabla ya kumkaribisha
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka aweze kuzungumza na wafanyakazi wa
mkoa huo Mei Mosi, 2019 katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Kwaya
ya walimu wilayani Maswa wakitoa burudani ya wimbo katika maadhimisho ya Siku
ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa
Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Makatibu Tawala wa Wilaya za Mkoa huo, katika maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa
Nguzonane wilayani Maswa.
Naibu
Waziri wa Madini, Mhe. Stanslous Nyongo akiwasalimia wafanyakazi na wananchi
kwa ujumla, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019
yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na
Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, katika maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa
Nguzonane wilayani Maswa.
Baadhi
ya wafanyakazi mkoani Simiyu wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.
Anthony Mtaka(hayupo pichani), katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari
Dereva wake Bw.Viecent Mtebe, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani
Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari
Mtunza Kumbukumbu wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega Bi. Laurencia katika
maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa
katika Uwanja wa Nguzonane wilayani Maswa.
Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi zawadi ya Ufanyakazi hodari
Mfamasia wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Bw. Oscar Tenganamba katika maadhimisho ya
Siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi, 2019 yaliyofanyika Kimkoa katika Uwanja
wa Nguzonane wilayani Maswa.
0 comments:
Post a Comment