Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka
2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa viongozi wilayani Meatu kuwasaidia
wakulima wa pamba kupata zana bora za
kilimo ili kuongeza tija katika
uzalishaji na wilaya hiyo iendelee kuwa
kinara katika uzalishaji wa zao la pamba nchini.
Ndg. Ali ameyasema hayo wakati Mwenge wa Uhuru
ulipopita na kukagua Shamba la Mbegu
bora ya pamba lenye ukubwa wa ekari 13 katika Kijiji cha Mwabusalu ambapo
alimpongeza mkulima Jidayi Charles na kumtunuku cheti cha kumtambua kama
mkulima bora.
“Ninampongeza
sana Bwana Jidayi maana ni wazee wachache sana wanaojihusisha na kilimo ni
vizuri mkachukua jitihada za makusudi kumsaidia apate zana za kisasa, kama
analima ekari 13 akiwa hana trekta nina uhakika akiwezeshwa atafanya vizuri
zaidi, kama mmeshaanza utaratibu wa kumpatia mkopo uharakishwe ili kiwango cha
uzalishaji kiweze kuongeza zaidi” alisema Mzee
Mkongea Ali.
Mkuu
wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani amesema wilaya ya Meatu ndiyo wilaya
kinara katika uzalishaji wa pamba nchini ambapo amebainisha kuwa katika msimu
wa mwaka 2018/2019 ilizalisha takribani kilo milioni 31 za pamba na akaeleza kuwa
mkakati wa wilaya ni kuendelea kuwasaidia wakulima kwa utaalam na mikopo za
kununua zana bora ili waweze kuzalisha kwa tija zaidi.
Akitoa
taarifa ya mradi wa shamba hilo, Afisa Kilimo wa Wilaya ya Meatu, Bw.Thomas
Shilabu amesema uzalishaji wa zao la pamba unakabiliwa na changamoto ya baadhi
ya wakulima kulima wa kilimo cha mazoea kwa kusia mbegu na kupalilia maotea.
Kwa
upande wake Bw. Jidayi Charles amesema kwa sasa anatumia trekta ya kukodi
kulima shamba lake lenye ukubwa wa ekari 13 ambalo linachangia kuchelewesha uandaaji
wa shamba kwa kuwa linatumiwa na wakulima wengi, lakini endapo atakapata trekta
lake litamrahisishia kuandaa shamba mapema na kwa urahisi zaidi.
Pamoja
na kutembelea mradi wa shamba za kuzalisha mbegu bora za pamba, Mwenge wa Uhuru
ukiwa Wilayani Meatu umezindua vyumba viwili vya maabara shule ya Sekondari
Mwandoya, kutembelea mradi wa maji wa SangaItiinje na kupanda miti katika
Chanzo cha maji, kukagua klabu ya wanafunzi ya wapinga RUSHWA na Klabu ya
wanafunzi ya kupambana na mimba za utotoni shule ya msingi Isengwa.
Wakati
mwenge wa uhuru ulipopita kuona shughuli za klabu ya mapambano dhidi ya mimba
za utotoni, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ameupongeza uongozi wa wilaya
ya Meatu kuanzisha klabu hizo shuleni na akatoa wito kwa wataalam wa Ustawi wa
Jamii na Dawati la jinsia na vyombo vya dola kutowahurumia wote wanaobanika
kusababisha mimba za utotoni.
Aidha,
ulifungua Nyumba ya kulala wageni TS Lodge, kukagua shughuli za kikundi cha
vijana wajasiriamali, kukagua shughuli za mapambano dhidi ya rushwa, mapambano
dhidi ya mimba za utotoni na mapambano dhidi ya malaria.
MWISHO
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akikagua shamba la mbegu bora za pamba katika Kijiji cha Mwabusalu wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Sehemu ya shamba la
mbegu bora za pamba ekari 13 linalomilikiwa na Mkulima Jidayi Charleas wilayani
Meatu, lililotembelewa na kukaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019
wilayani humo.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akifungua Vyumba viwili vya maabara katika
shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akipanda mti katika chanzo cha maji cha Mradi
wa maji wa SangaItinje wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiwa na wakimbiza mwenge wa Uhuru wengine wakikagua
pampu ya maji katika Mradi wa maji wa Sanga Itinje wilayani Meatu, Mei 23,
2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Dkt. Joseph Chilongani (kulia) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu
wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe katika Kijiji cha Sangaitinje wilayani
Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (mwenye galoni la maziwa ya Meatu(Meatu Milk)
akiangalia bidhaa za maziwa zinazozalishwa katika kiwanda cha Meatu Milk kinachomilikiwa
na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani
humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimkabidhi cheti
Mwenyekiti wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa
mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (kulia) akiangalia burudani kutoka kwa
Wanachama wa Klabu ya Kupinga Mimba za Utotoni katika shule ya Msingi Isengwa,
wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 22, 2019.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ( wa tatu kulia) akizungumza na kikundi
vijana wanaotengeneza Batiki Mjini Mwanhuzi wilayani Meatu, wakati wa mbio za
Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akizungumza na Wanachama wa klabu ya Kupinga
mimba za Utotoni katika Shule ya Msingi Isengwa wilayani Meatu, wakati wa mbio
za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiangalia mazoezi kwa vitendo ya wanafunzi
wa shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, wakati wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akiangalia mazoezi kwa vitendo ya wanafunzi
wa shule ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu, wakati wa Mbio za Mwenge wa
Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Sehemu ya mbele ya Vyumba vya
maabara vilivyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 katika shule
ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akizungumza na
wanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa
mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akisaini cheti cha
Klabu ya Wapinga Rushwa katika shule ya Msingi Isengwa, wakati wa mbio za
Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei 23, 2019.
Baadh ya vikundi vya
vijana vya wilaya ya Meatu vilivyokaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani
humo, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akitoa ujumbe wa mbio
za Mwenge wa Uhuru mara baada ya kuzindua vyumba viwili vya maabara katika
Shule ya Sekondari Mwandoya wilayani Meatu, Mei 23, 2019.
Kiongozi wa Mbio za
Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali, wakimbiza Mwenge wa
Uhuru wengine na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Meatu wakiwa katika picha ya
pamoja na Wanachama wa klabu ya Kupinga mimba za Utotoni katika Shule ya Msingi
Isengwa wilayani Meatu, wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wilayani humo, Mei
23, 2019.
Nyumba ya pampu na
jenereta katika Mradi wa Maji wa SangaItinje wilayani Meatu ambao ulitembelewa
na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 wilayani humo.
Sehemu ya Vyumba vya
maabara vilivyozinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mei 23, 2019 katika shule
ya sekondari Mwandoya wilayani Meatu.
0 comments:
Post a Comment