Wednesday, May 29, 2019

WANANCHI ZAIDI YA 300,000 KUNUFAIKA NA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA

Jumla ya wakazi 346,365 wa Wilaya ya Itilima na maeneo ya jirani wanatarajia kunufaika na ujenzi wa mradi wa hospitali ya Wilaya ya Itilima inayotarajiwa kukamilika Juni 30 mwaka 2019.


Mradi huo wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya na kusogeza karibu huduma hiyo kwa wananchi ,hadi kukamilika kwake unatarajia kutumia kiasi cha sh bil 1 .5.


Akisoma taarifa ya mradi wa Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Itilima kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019,Mzee Mkongea Ali ,mganga mkuu wa Wilaya hiyo Dk Anorld Charles amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutarahisisha huduma za  wananchi wa Wilaya humo.

Dk Charles ameeleza kuwa wananchi wengi wa Wilaya hiyo wamekuwa wakitembea umbali mrefu wa wastani wa kilometa 45 hadi 50 kufuata huduma za afya katika hospitali ya Bariadi.

Amesema kutokana na hali hiyo ya kutembea umbali mrefu,wengi wao hupoteza maisha kwa kukosa huduma stahiki za haraka hususani akinamama wajawazito ambao wengi wao hupoteza damu nyingi njiani.

Ameongeza kuwa endapo hospitali hiyo itakamilika kwa muda muafaka,itasaidia sana kupunguza vifo vya akinamama wajawazito wanaopoteza damu nyingi pindi wawapo njiani kuelekeza katika hospitali ya wilaya ya Bariadi.

Amesema kwa mwaka 2018 (Jan hadi Dec) pekee jumla ya akinamama 5 walipoteza maisha kwa kuvuja damu nyingi kwa kucheleweshwa kufika mapema katika zahanati na hospitali zilizo karibu nao.

Naye kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2019 Ndg. Mzee Mkongea Ali alisema kuwa jitihada za Ukamilishaji wa hospitali hiyo zinatakiwa ziwe za haraka iwezekanapo kabla ya kuisha mwaka wa fedha, kwani endapo wakishindwa kukamilisha kwa muda husika hawataweza kupata fedha za ukamilishaji huo.

" napenda kuwashauri kuwa ukamilishaji wa hospitali hiyo unatakiwa uwe Juni 30 mwaka huu kama ilivyoelekezwa hivyo ni lazima ujenzi uende kwa haraka usiku na mchana...la sivyo mwaka ya fedha 2018/2019 utakapomalizika itakuwa vigumu kupata fedha hizo zilizokuwa zimetengwa katika bajeti ya 2018/2019.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi amesemaViongozi wilayani humo watahakikisha Hospitali hiyo inakamilika kabla ya juni 30, 2019 kama ilivyoelekezwa na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rai TAMISEMI.

Marangwa Maduhu mkazi wa kijiji cha Nguno Wilayani humo,amesema uwepo wa hospitali hiyo itawasaidia sana kupunguza gharama za usafiri walizokuwa wakizitumia kufuata matibabu Wilayani Bariadi.

Mpaka sasa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Itilima tayari imeshatumia kiasi cha sh bil 1.2 sawa na asilimia 81 ya utekelezaji wake

Katika hatua nyingine kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2019 Ndg. Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa wananchi kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti rafiki katika vyanzo vya maji na kusisitiza wale wote ambao watakiuka sheria wachukuliwe hatua.
MWISHO
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akipata maelezo kuhusu ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Itilima, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimtwisha mama ndoo mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa Mwamapalala wilayani Itilima, wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru wilayani humo,  Mei 24, 2019. 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akikabidhi cheti wanachama wa Klabu ya wapinga rushwa katika shule ya Sekondari Mwamapalala, mara baada ya kuzindua klabu hiyo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akikagua moja ya vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya Msingi Lagangabilili, wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.
wanachama wa Klabu ya wapinga rushwa katika shule ya Sekondari Mwamapalala, wakifurahia uzinduzi wa klabu hiyo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (mwenye skafu) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa misitu wilayani Itilima, mara baada ya kutembelea mradi huo wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.
                                     Moja ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Itilima
Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Benson Kilangi akimkaribisha Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kabla ya kukabidhiana Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Dkt. Joseph Chilongani
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza :- Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (hayupo pichani) wakati wa mbio za mwenge wa uhuru Mei 24, 2019 wilayani humo.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!