Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
amewahakikishia waumini na viongozi wa madhehebu ya dini mkoani hapa kuwa
viongozi wa serikali wako pamoja nao na wataendelea kushirikiana na kila
watakapo wahitaji .
Mtaka ameyasema hayo jana Mei 30, 2019 katika futari
aliyoiandaa kwa waumini na viongozi wa madhehebu ya Kiislam katika Viwanja vya
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mjini Bariadi.
“Ndugu zangu waislam mliopo hapa naomba muamini
kabisa kwamba viongozi wa mkoa na viongozi wote wa Serikali kwenye maeneo yetu ndani ya mkoa wa Simiyu wako pamoja na ninyi;
kwa jambo lolote, eneo lolote ambalo mngehitaji ushirikiano kwenye mkoa wetu sisi
tuko tayari kuunga mkono” alisema Mtaka.
Aidha, ameshauri viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Simiyu
kuomba kuandaa tukio moja kubwa la Kitaifa kufanyika Mkoani Simiyu kama ambavyo
yamekuwa yakifanyika katika mikoa mingine na akaahidi kushirikiana na viongozi
hao endapo watakuwa tayari kuandaa tukio lolote.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito pia kwa
viongozi wa Madhehebu ya Kiislam kutengeneza mazingira mazuri kwa vijana na
kuwafundisha ikiwa ni njia moja wapo ya kuwaandaa kushiriki katika mashindano
ya kuhifadhi Quran ili Mkoa wa Simiyu na nchi kwa ujumla iweze kuwakilishwa vema
katika mashindano hayo.
Sambamba na hilo amewashukuru viongozi wa dini kwa
kuendelea kuiombea nchi, viongozi wake, kuombea amani, umoja na mshikamano
miongoni mwa Watanzania ambapo amebainisha kuwa Serikali inatambua mchango wa
Taasisi za dini katika nchi na kwa namna viongozi wa dini wanavyoshirikiana na
Serikali katika masuala na mtukio mbalimbali.
Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mahamoud Kalokola amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa
namna anavyoenzi waislam na akatoa wito kwa watu wengine kuiga mfano wake kwa
kuwa kila anyefanya hivyo anapata thawabu yake kwa Mwenyezi Mungu.
Ameongeza kuwa tendo hilo la kufuturisha
linawakusanya watu pamoja walio waislam na wasio waislam jambo ambalo
linadumisha umoja, upendo, ushirikiano na mshikamano kwa wote bila kujali
tofauti ya dini zao.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
amempongeza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambao nao watajipanga kufanya
jambo hili ili nao waweze kupata baraka za Mwenyezi Mungu.
Huu umekuwa ni utaratibu kwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
kuandaa furati kwa waumini viongozi wa madhehebu ya dini ya Kiisla, ambayo pia
huwahusisha viongozi wengine wa chama na Serikali wakati wa mfungo wa mwezi
Mtukufu wa Ramadhani.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Sheikh wa Mkoa wa Simiyu,
Mahamoud Kalokola mara baada ya futari
iliyoandaliwa kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine
jana Mei 30, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi
mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa
madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari
aliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili yao, Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa
madhehebu ya Kiislam na viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari
aliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili yao, Mei 30, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na
viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam
na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya futari aliyoandaliwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam na viongozi wengine jana Mei 30,
2019.
Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na
viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam
na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu
ya Kiislam na viongozi wa Chama na Serikali wakishiriki futari iliyoandaliwa
kwa ajili ya na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka jana Mei 30, 2019.
Baadhi ya waumini wa madhehebu
ya Kiislam na viongozi wa Chama na Serikali wakishiriki futari iliyoandaliwa
kwa ajili ya na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka jana Mei 30, 2019.
Mwakilishi wa Chama Cha
Mapinduzi Mkoa wa Simiyu akizungumza na waumini wa madhehebu ya Kiislam na
viongozi mbalimbali walioshiriki katika futari aliyoindaa kwa ajili yao, Mkuu
wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kwa ajili ya waumini wa madhehebu ya Kiislam
na viongozi wengine jana Mei 30, 2019.
0 comments:
Post a Comment