Sunday, May 5, 2019

DKT. NDUGULILE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA KISIASA KUTOINGILIA KAZI ZA TAALUMA YA AFYA



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ametoa rai kwa viongozi wa Kisisasa hapa nchini kuacha kuingilia kazi za Kitaaluma katika sekta ya Afya na kuwaomba wawaache wataalam wafanye kazi zao kwa misingi na miiko ya Kitaaluma inayowaongoza.

Dkt. Ndugulile ameyasema hayo Mei 05, 2019 katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, chini ya Kauli Mbiu “Wakunga Watetezi wa Haki za Wanawake”, ambapo alikuwa akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Amesema hivi karibuni kumekuwa na matamko yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa yanayowakatisha tamaa watumishi wa sekta ya afya na baadhi ya viongozi wameanza kuingilia masuala ya kitaalum, hivyo akawaomba ikiwa viongozi hao  watakutana na changamoto za watendaji wa afya waishirikishe wizara ya afya ili wachukuliwe  hatua kwa mujibu wa taaluma zao.

“Niwaombe sana viongozi wa Serikali na Viongozi wa vyama, masuala ya kitaaluma yanashughulikiwa kitaaluma kama kuna changamoto na wanataaluma ndiyo maana tuna mabaraza ya taaluma na ndiyo maana sisi wizara tupo mtushirikishe, nimelisema hili kwa sababu nimeona sekta imeanza kuingiliwa” alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt. Faustine Ndugulile amewataka wakunga hapa nchini kuendelea kuzingatia miiko na misingi ya taaluma yao katika huduma wanazotoa kwa jamii na kuahidi kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote watakaokiuka misingi hiyo kwa kuwa jamii inahitaji heshimu, utu, upendo na kutiwa moyo

Katika hatua nyingine Dkt. Ndugulile ametoa wito kwa  wadau mbalimbali wa maendeleo na jamii kwa ujumla kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za afya ili changamoto ya vifo vitokanavyo na uzazi vibaki kuwa historia ambapo amesema kwa sasa wanawake 11,000 wanakufa kila mwaka kutokana na uzazi.

Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania, Bibi. Feddy Mwanga ameiomba Serikali kuongeza idadi ya wakunga ili mkunga aweze kutoa huduma kwa kiwango kinachokubalika Kitaifa na kimataifa huku akisisitiza Serikali kuona haja ya kujenga nyumba za wakunga katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya vinavyoboreshwa na vinavyojengwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthoy Mtaka amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa shilingi bilioni saba  fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali tatu za Wilaya Bariadi, Busega na Itilima ambazo ujenzi wake unaendelea vizuri.

Aidha, Kiswaga ameshukuru Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNPFA) kwa namna linavyoshirikiana na Serikali mkoani Smiyu kwa kukarabati baadhi ya vituo, kununuaa vifaa mbalimmbali, kutoa mafunzo kwa wakunga jitihada ambazo zimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Akitoa taarifa ya Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema
Idadi ya wakunga katika vituo vya kutolea huduma za afya Simiyu imeongezeka hali iliyofanya wajawazito wengi kujifungulia katika vituo vya afya kutoka asilimia 62 mpaka asilimia 68, hivyo vifo vya mama wajawazito vimepungua kutoka vifo 48 mwaka 2017 mpaka vifo 40 mwaka 2018.

Naye Makamu Mwakilishi Mkaazi wa UNFPA hapa nchini, Dkt.Hashina Begum amesema kwa kushirikiana na Chama cha Wakunga nchini (TAMA) limetoa mafunzo kwa wakunga 90 kutoka katika vituo vilivyoboreshwa ili kuwasaidia wakina mama wajawazito na watoto kupata huduma za dharura na kupunguza vifo kwa mama na mtoto vitokanavyo na uzazi.

Grace Magengeni Mkunga kutoka Jijini Dodoma amesema” siku yetu imefana tunashukuru hotuba ya Naibu Waziri imetutia moyo katika kuwahudumia wanawake na watoto, nawashauri wenzangu tusimamie taaluma zetu tufanye kazi kwa bidii naamini hao wanaotuingilia majukumu yetu wataachaa maana ni kweli,  tunashukuru Naibu Waziri kulisemea hili suala”
MWISHO




Baadhi ya wakunga wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.


Baadhi ya wakunga na wanafunzi wa shule za sekondari Mjini Bariadi wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (wa nne kushoto)  na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wadau wa afya  wakipokea maandamano ya wakunga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (wa nne kushoto)  na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na wadau wengine wa afya  wakielekea katika kukagua mabanda ya maonesho ya shughuli za wakunga, katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia ) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wakunga ya namna wanavyowahudumia wakina mama wajawazito na watoto wakati alipotembelea Banda la Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA),  katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) na Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA),  Bibi. Feddy Mwanga wakifurahia jambo na katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia ) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wakunga ya namna wanavyowahudumia wakina mama wajawazito na watoto wakati alipotembelea Banda la Wakunga Tanzania Tawi la Hospitali ya Mloganzila  katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mwenyekiti wa CCM Komredi. Enock Yakobo wakiteta jambo katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.  , Mhe. Festo Kiswaga akitoa salamu za mkoa kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, kuzungumza na wakunga pamoja  na wananchi kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Tanzaia Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakunga wakicheza kwa furaha wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kulia ) akiangalia baadhi ya vitabu vinvyotuika kutoa elimu kwa wananchi wakati alipotembelea banda la maonesho la Shirika lisio la kiserikali la AGPAHI, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akitoa taarifa ya Mkoa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile (kushoto) akiagana na baadhi ya wakunga mara baada ya kumalizika kwa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Makamu Mwakilishi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu Duniani(UNFPA) akizungumza na wakunga na wananchi mkoani Simiyu, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakunga wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Wakunga wakiimba pamoja na Kwaya ya AICT Bariadi Town wimbo maalum, wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wanawake wakisubiri huduma za upimaji katika moja ya banda linalotoa huduma katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakunga wakiwa katika maandamano wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Baadhi ya wakunga wakionesha igizo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mwenyekiti wa CCM Komredi. Enock Yakobo wakiteta jambo, katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania(TAMA),  Bibi. Feddy Mwanga akitoa taarifa ya chama hicho katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na wakunga pamoja na wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi mmoja wa kunga wa moa wa Simiyu cheti kama zawadi ya kufanyakazi nzuri, katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(wa nne kulia walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu, viongozi wa wajkunga, wadau wa afya na baadhi ya wakunga wa mkoa waSimiyu waliofanya vizuri (wenye vyeti), katika Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani ambayo yamefanyika Kitaifa leo Mei 05, 2019 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!