Tuesday, March 17, 2020

SIMIYU YAFUNGA KAMBI YA KITAALUMA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu umefunga kambi ya Kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha Sita iliyokuwa ikifanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa , ikiwa ni sehemu ya tahadhari dhidi ya Homa kali ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona.

Akifunga kambi hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini amesema uongozi wa mkoa umefikia hatua hiyo kuchukua tahadhari kama ilivyoelekezwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa juu ya kuzuia mikusanyiko ya watu wengi isiyo ya lazima katika kipindi hiki ambacho kumeripotiwa idadi ya watu kadhaa kubainika kuwa na virusi vya Corona katika nchi mbalimbali.

“Kutokana na Maelekezo ya Serikali Mkoa umeona kambi hii ifungwe kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Corona,  Mhe. Rais amesitisha mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2020, Mhe. Waziri Jafo amesitisha UMISETA na UMITASHUMTA na tahadhari mbalimbali zimeendelea kutolewa na Serikali ikiwemo ya kuzuia mikusanyiko; sisi hapa tuna wanafunzi  takribani 1000 kutoka shule 10 hivyo tumekubaliana kwa pamoja tuifunge kambi hii,” alisema Sagini.

Aidha, Sagini amesema pamoja na kambi za kitaaluma kufungwa Mkoa utaendelea kusimamia utekelezaji wa mkakati wa taaluma wa mkoa ili walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu waweze kutimiza wajibu wao kuhakikisha Mkoa unatimiza adhma yake ya kuwa miongoni mwa mikoa itakayofanya vizuri katika mitihani yote ya Kitaifa.

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema wanafunzi hao walitakiwa kukaa kambini muda wa wiki sita kwa ajili ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa unaotarajiwa kufanyika mwezi Mei 2020, hivyo pamoja na kusitisha kambi hiyo walimu wamehimizwa kutimiza wajibu wao katika ufundishaji na wanafunzi wametakiwa kwenda kusoma kwa bidii ili kufikia lengo la Mkoa.

Awali akitoa elimu ya ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona kwa wanafunzi na walimu kabla ya kambi kufungwa, Afisa Afya wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Reuben Malimi amesema ugonjwa huo hauna tiba matibabu yanayofanyika yanazingatia dalili zinazoonekana kwa mgonjwa, hivyo ni vema kila mmoja  akachukua tahadhari kwa kuzingatia maelekezo na elimu inayotolewa na wataalamu wa afya katika maeneo mbalimbali.

Nao wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Mkoa wa Simiyu wameshukuru uongozi wa Mkoa kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwa kutoa elimu kuhusu Corona  kabla ya kufunga kambi, huku wakieleza namna ambavyo kufungwa kwa kambi kunaweza kuathiri malengo yao waliyojiwekea.

“Tunashukuru uongozi wa Mkoa kutoa elimu  na kuchukua tahadhari ya Corona kwa kufunga kambi ni hatua ya kutuhakikishia usalama, lakini kambi ilitusaidia kujua namna ya kujibu maswali ya mtihani wa Taifa na kujifunza mada ngumu tulizoshindwa shuleni kupitia kwa walimu mahiri, tutatumia muda huu kujisomea kwa bidii ili tufaulu vizuri mtihani wa Taifa,” alisema Isack Ndassa kutoka Shule ya Sekondari Kanadi Itilima.
MWISHO


 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao jana  ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.


 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(hayupo pichani) akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao jana  ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.


 Afisa Afya wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Reuben Malimi akitoa elimu ya tahadhari dhidi ya Homa ya Mapafu inayosababishwa na Virusi vya Korona kwa wanafunzi wa kidato cha Sita mkoani humo waliokuwa katika kambi ya Kitaaluma shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa, kabla ya kambi hiyo kufungwa jana ili kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.


 Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha Sita wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(hayupo pichani) akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao jana  ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.


 Afisa Elimu wa Mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju akitoa taarifa ya hali ya kambi ya kitaaluma kwa waanfunzi wa kidato cha sita mkoani humo, kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kuzungumza na wanafunzi hao, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao jana  ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.


 Mwanafunzi wa kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Nyaranja wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Ndebile Charles akizungumzia hali ya kambi ya kitaaluma, kabla ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kuzungumza na wanafunzi hao na kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao jana  ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.


 Mmoja wa walimu mahiri katika Kambi ya Kitaaluma ya Kidato cha Sita iliyokuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa, Mwl. Haruna Boniface  akitoa maelezo juu ya kambi hiyo kabla ya kambi hiyo kufungwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.


Baadhi ya walimu na wanafunzi wakimfuatilia Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini(hayupo pichani) akizungumza na wanafunzi wa Kidato cha Sita mkoani humo, kabla ya kufunga kambi ya kitaaluma kwa wanafunzi hao jana  ambayo ilikuwa ikiendelea katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa kwa lengo la kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.

Wednesday, March 11, 2020

UNUNUZI MAZAO MCHANGANYIKO KUPITIA AMCOS UTAWAKOMBOA WAKULIMA: DC BARIADI



Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema  mfumo wa ununuzi wa mazao mchanganyiko kupitia vyama vya msingi vya Ushirika ( AMCOS) utakaoanza kutekelezwa mwaka huu 2020 umelenga kuwakomboa wakulima na  kuwawezesha kupata soko la uhakika  lenye ushindani pamoja na kuwaondoa wanunuzi wanyonyaji.

Kiswaga ameyasema  hayo jana katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika shule ya sekondari Kusekwa Memorial mjini Bariadi mkoani Simiyu, lengo lilikuwa kujadiliana namna ya kutekeleza maelekezo yaliyotolewa na  Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.  Hussein Bashe kupitia tangazo alilolitoa Februari 14, 2020 kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko,dengu ,mbaazi , na soya kupitia Vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)  kwa mikoa yote inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.

Amesema wakulima wa mazao ya jamii ya mikunde pamoja na mbegu wamekuwa wakiuza kiholela pasipokuwa na mfumo rasmi hali iliyokuwa ikipelekea kuuza kwenye mizani ambayo haijahakikiwa huku wanunuzi wakijiamlia bei wanazozitaka.

"Serikali  imeamua kuja na mpango huo mzuri na lengo lake kubwa  ni kuwakomboa wakulima pamoja na kuwaondoa wanunuzi wanyonyaji kwani wamekuwa wakinunua mazao kwa wakulima kwa bei zao wenyewe jambo ambalo linapelekea kuwa na kilimo kisichokuwa na tija;kila mmoja anayehusika na mazao hayo atashirikishwa tutazifikia kata zetu zote kutoa elimu,"alisema Kiswaga.

Ameongeza kuwa mfumo huo wa kuuza kupitia AMCOS  utawezesha kila zao kuwa na bei halisi hatua ambayo itapunguza manung'uniko  ya wakulima juu ya unyonywaji huku akiwasisitiza pembejeo bora za kilimo ikiwemo  mbolea na mbegu bora ili  waweze kuwa na kilimo chenye tija.

Sambamba na hayo aliongeza kuwa changamoto kubwa ya wakulima ni uzalishaji ,masoko na namna ya upataji wa fedha baada ya kuuza huku akibainisha kuwa mkutano huo ni mwanzo mzuri wa kuhakikisha wanawasaidia wakulima kuwa wabunifu kwa kujua wanazalisha nini kwa kiasi gani na uchaguzi sahihi wa mbegu ,matumizi sahihi ya mbolea na viuadudu.

Kwa upande wake Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika upande wa uhamasishaji, Bw. Charles Malunde  amesema  kuwa mfumo unaoweza kuwanufaisha wakulima na wenye tija ni wa stakabidhi ghalani na kuwa nguvu ya ushirika inapatikana kwa jinsi wanaushirika wanavyoshirikiana.

Naye mkurugenzi wa uendeshaji soko la bidhaa (TMX), Bw. Augustino Mbulumi amesema kupitia mfumo huu wakulima watapata taarifa za soko kwa mazao yao na watapaswa kupata malipo ya mazao yao ndani ya saa 48 hivyo ni vema wakafungua akaunti benki ili kurahisisha mapokezi ya fedha zao.

Akizungumza kwa niaba ya wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Melkizedeck Humbe amesema ni vema kila mmoja akatimiza wajibu wake ili mfumo huu uweze kufanikiwa huku akibainisha kuwa mfumo huo utazisaidia Halmashauri kupata takwimu sahihi na namna ya ukusanyaji mapato.

Awali  akisoma tangazo la maelekezo ya serikali kuhusu  mfumo wa ununuzi wa choroko ,dengu, mbaazi, soya, na ufuta  mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Simiyu Ibrahim   Kadudu amesema tangazo hilo litaanza kutumika mwaka huu 2020 ambapo mazao hayo yatauzwa kupitia mfumo wa ushirika kwa mfumo wa minada ya vyama vikuu vya ushirika katika maeneo yao .

Aidha imedaiwa kuwa tume ya maendeleo ya ushirika kwa kushirikiana na soko la bidhaa (TMX) itaendesha minada kwa maeneo maalum kwa mazao hayo kupitia mfumo wa soko la bidhaa na taratibu zake zitabainishwa na TMX.

Wakizungumza kwa niaba ya wakulima baadhi viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika Amcos walisema kuwa ni vema watendaji wa idara ya kilimo na ushirika wakatembelea kata zote kutoa elimu kwa wakulima ili mfumo huo ufahamike kwa wote.
MWISHO.

 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya  kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.



Baadhi ya wadau wa mazao mchanganyiko mkoani Simiyu, wakifuatilia kikao cha wadau hao kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika (Uhamasishaji), Bw. Charles Malunde akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu .2020.

Mrajisi Msaidizi wa Vyama Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahim Kadudu akitoa ufafanuzi a masuala mbalimbali katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji  Soko la Bidhaa(TMX), Bw. Augustino  Mbulumi akitoa mada katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.


 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu, katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika  jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.


 Bw. James Petro  akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.


 Bw. Daniel Masilimbi akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.


 Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.


 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua baadhi ya masuala kwa wadau wa mazao mchangamyiko katika kikao cha wadau hao kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.


 Mtaalam wa masuala ya stakabadhi ghalani akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.


Baadhi ya wadau wa mazao mchanganyiko mkoani Simiyu, wakifuatilia kikao cha wadau hao kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.



 Baadhi ya wadau wa mazao mchanganyiko mkoani Simiyu, wakifuatilia kikao cha wadau hao kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.

Baadhi ya wadau wa mazao mchanganyiko mkoani Simiyu, wakifuatilia kikao cha wadau hao kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.

Monday, March 9, 2020

MAKAMU WA RAIS AONGOZA KILELE MAADHIMISHO SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KITAIFA MKOANI SIMIY


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniania ambayo yamefanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Maadhimisho haya yenye Kauli Mbiu “Kizazi cha Usawa Kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na ya Baadaye” yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali waliopo madarakani na wastaafu wakiwemo Mama Getrude Mongela, Mama Anna Abdallah, Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Mhe. Anne Makinda, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg. Gaudensia Kabaka, Katibu wa UWT Taifa, Ndg. Queen Mlozi na viongozi wengine
Katika maadhimisho hayo Mhe. Makamu wa Rais ametembelea mabanda ya Maonesho ya kazi mbalimbali za wanawake, mashirika, taasisi na wadau wa maendeleo wanaojihsisha na masuala ya wanawake na baadaye akapokea maandamano ya wanawake kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Maandamano kwenye Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri Bariadi Mkoani Simiyu leo March 08,2020.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Wananchi Wanawake Mkoani Simiyu wakiwa kwenye Maandamano ya kusherehekea Maadhimisho ya  siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu  March 08,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga akiongoza Maandamano kwenye Maadhimisho ya  siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu leo March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Wananchi Wanawake Mkoani Simiyu wakiwa kwenye Maandamano ya kusherehekea Maadhimisho ya  siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu  March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

Wananchi Wanawake Mkoani Simiyu wakiwa kwenye Maandamano ya kusherehekea Maadhimisho ya  siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu  March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

 Wananchi Wanawake Mkoani Simiyu wakiwa kwenye Maandamano ya kusherehekea Maadhimisho ya  siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu  March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

 Wananchi Wanawake Mkoani Simiyu wakiwa kwenye Maandamano ya kusherehekea Maadhimisho ya  siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu  March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

 Askari Polisi wa Kike wakiwa na Furaha Kwenye Maandamano ya  siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

Mkurugenzi  Mipango wa  Pamba  Samweli Kilua akimkabidhi Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba Mkoani Simuyu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwenye maonesho ya kilele cha siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauriya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu  March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimsikiliza Afisa Mikopo katika benki ya Postal Bank Tanzani TPB Tawi la Simiyu Shedrack Daudi alipotembelea banda la Banki hiyo kwenye maonesho ya kilele cha siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya aina ya bidhaa ya kitenge alipotembelea Banda la Benki ya Posta Tanzania TPB Tawi la Simiyu kwenye maonesho ya kilele cha siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu  March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
 Baadhi ya viongozi na wadau walioshiriki katika Kilele cha Maadhimisho ya Wanawake Duniani Machi 2020, yaliyofanyika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akimtuza Msanii na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe. Vick Kamata wakati alipotumbuiza kwa wimbo maalum katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri Bariadi Mkoani Simiyu March 08,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )

MAPATO YATAKAYOTOKANA NA STENDI BARIADI YAKAFANYE KAZI ZA WANANCHI: MAKAMU WA RAIS


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema wafanyabiashara watakaopangishwa katika jengo la Stendi ya Kisasa ya Mji wa Bariadi inayojengwa sasa pale itakapokamilika, wahakikishe wanalipa kodi na mapato hayo yatumike katika shughuli za maendeleo ya wananchi na kuitunza stendi hiyo.
Mhe. Makamu wa Rais ametoa agizo hilo wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la stendi hiyo Mjini Bariadi.

MAKAMU WA RAIS AAGIZA TTCL KUPELEKA MKONGO WA TAIFA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA SIMIYU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameagiza Shirika la Mawasiliano nchini TTCL kufikisha mkongo wa Taifa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu ili vifaa vinavyotumika kutoa huduma vinavyowezeshwa na Mtandao wa Intanenti viweze kufanya kazi yake sawa.
Mhe. Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati akifungua Jengo la Huduma kwa Wateja la TTCL Mkoa wa Simiyu Machi 07, 2020 mjini Bariadi , ambapo amewahimiza watendaji wa TTCL kutoa huduma bora na kwa ufanisi.
Aidha, Mhe. Makamu wa Rais ametoa wito kwa wananchi kutunza na kulinda miundombinu ya mawasiliano na watakaobainika kuhujumu miundombinu hiyo watashtakiwa kama wahujumu uchumi.



MAKAMU WA RAIS AWATAKA WANANCHI KUKILINDA CHUO CHA IFM SIMIYU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa wananchi wa Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi kuwa walinzi wa Tawi jipya la Kanda ya Ziwa la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) linalojengwa katika eneo hilo.
Mhe. Makamu wa Rais ametoa rai hiyo Machi 06, 2020 wakati alipozungumza na wananchi wa Kata ya Sapiwi Machi 06, 2020 mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Tawi jipya la Chuo hicho.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakishangilia mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa  wa Tawi jipya la Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Machi 06, 2020.

MAKAMU WA RAIS AWAONYA WANANCHI WASITUNZE FEDHA MAJUMBANI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wananchi wa Wilayani ya Busega kutokaa na fedha majumbani badala yake watumie Taasisi za kifedha kutunza fedha zao kwa ustawi wa maisha yao na Usalama wa Fedha zao.

Mhe. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati akifungua tawi la NMB Nyashimo wilayani Busega Machi 06, 2020 ambapo ameipongeza benki huyo kusogeza huduma karibu na wananchi.

"Wilaya hii ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla una uchumi mkubwa, mna uchumi utokanao na ziwa yaani uvuvi, uchumi wa mifugo, uchumi wa kilimo; hivyo sikae na fedha mikononi pelekeni benki ili benki itumie kwa maendeleo yetu na ya kwako binafsi," alisema Mhe. Makamu wa Rais.

Katika hatua nyingine Mhe. Makamu wa Rais ameipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha huduma za bima na huduma maalum kwa ajili ya kundi la waendesha pikipiki (bodaboda) na kubainisha kuwa huduma hiyo umechangia kuwapunguzia hali ya kubaki na fedha mfukoni na kuwapunguzia haki ya kuendelea kuwashawishi wanafunzi wa kike na kuwalaghai na wakati mwingine kuwapa ujauzito.

Naye Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Ashatu Kijaji ameagiza Benki Kuu ya Tanzania kukaa na benki nyingine nchini ili kujadili namna ya kupunguza riba kwa wakopaji(wananchi) kwa kuwa Serikali imezipunguzia benki hizo riba katika mitaji ya kuendeshea benki hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Benki ya NMB kwa namna ambavyo imekuwa ikichangia katika maendeleo ya Mkoa wa Simiyu ambapo hadi sasa imechangi shilingi milioni 200 katika sekta ya Elimu.
MWISHO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan(wa pili kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi la NMB Busega, katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Simiyu, Machi 06, 2020.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na viongozi wa Benki ya NMB wakishangilia mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan(wa pili kulia) kufungua Tawi la NMB Busega, katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Simiyu, Machi 06, 2020.
Jengo la Tawi la NMB Busega lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Machi 06, 2020.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea eneo la Jukwaa kwa ajili ya kwenda kuzungumza na wananchi mara baada ya kuzindua Tawi la NMB Busega, katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Simiyu, Machi 06, 2020


WAZIRI WA AFYA AZITAKA HALMASHAURI KUTENGA ASILIMIA 10 YA VIKUNDI


Kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa amabyo yatafanyika Bariadi Mkoani Simiyu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri zote ambazo hazijatenga asilimia kumi ya mapato ya ndani ambayo ni fedha kwa ajili Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kuhakikisha zinatenga fedha hizo ifikapo Machi 30, 2020 ili kuyawezesha makundi hayo kupata mikopo.

Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo Machi 05, 2020 wakati wa Uzinduzi wa Maonesho ya shughuli za wanawake wajasiriamali na jitihada za wadau katika kuwezesha wanawake kiuchumi na kuleta usawa wa kijinsia, katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akisaini katika ubao kwa kutumia chaki zinazotengenezwa Maswa mkoani Simiyu(Maswa Chalks) wakati wa alipotembelea banda la Maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa katika maonesho  ya wanawake wajasiriamali, taasisi na vikundi mbalimbali Machi 05, 2020.

BASHEAZINDUA MKAKATI WA MAPINDUZI YA KILIMO SIMIYU


Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amezindua Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) Mkoa wa Simiyu na kuwahimiza wakulima wote kufungua akaunti za benki kwa kuwa katika msimu ujao Wakulima watalipwa fedha zao kupitia mfumo wa benki ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za wakulima yanayofanywa na baadhi ya viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika(AMCOS).

Aidha, Mhe. Bashe amesema Serikali imedhamiria kuwekeza katika kilimo na kujenga ushirika imara ikiwa ni pamoja na kufufua baadhi ya Viwanda vya kuchambua pamba(ginneries) vya wakulima kikiwepo kiwanda cha Luguru wilayani Itilima na viwanda vingine wiwili kutoka wilayani ya Maswa. 

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amezindua Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kusekwa Mjini Bariadi, Machi 05, 2020.
Baadhi ya viongozi na watendaji wakifuatilia uzinduzi wa Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kusekwa Mjini Bariadi, Machi 05, 2020.

Monday, March 2, 2020

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KITAIFA MKOANI SIMIYU


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kitaifa yatafanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Mjini Bariadi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Maadhimisho haya yanaongozwa na kauli Mbiu "Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na ya  baadaye"  ambapo yataanza tarehe 02 Machi 2020 mpaka tarehe 08 Machi 2020.

"Katika Maadhimisho haya tunawatarajia wageni mbalimbali na shughuli mbalimbali kufanyika; mathalani kuanzia Tarehe 02 Machi 2020 maonesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wanawake zitaoneshwa, wajasiriamali kutoka maeneo yote nchini wamethibitisha kushiriki pia kutakuwa na upimaji kwa magonjwa mbalimbali ya Wanawake,"

"Siku ya tarehe 06 Machi 2020 kutakuwa na Jioni ya mwanamke ambapo wake za Viongozi waliopo madarakani na wastaafu na Watendaji mbalimbali wa Taasisi watashiriki; mpaka sasa Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya nne,  Mama Tunu Pinda, Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania na viongozi mbalimbali Wanawake wamethibitisha kushiriki, wakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu," alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kushiriki katika  shughuli zote zitakazofanyika katika Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa na kilele chake ambazo zitafanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Katika hatua nyingine Mtaka amesema Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku tatu Mkoani Simiyu kuanzia tarehe 06 Machi 2020 hadi 08 Machi  2020.

Amesema tarehe 06 Machi, 2020 Mhe. Makamu wa Rais atafungua Tawi la Benki ya NMB katika Kata ya Nyashimo makao Makuu ya Wilaya ya Busega na baadaye kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi (IFM), katika Kata ya Sapiwi wilayani Bariadi.

Ameongeza kuwa tarehe 07 Machi, 2020 Mhe. Makamu wa Rais atafungua Ofisi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ya Mkoa na siku hiyo hiyo ataweka jiwe la msingi Ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Halmashauri ya Mji wa Bariadi kilichopo Kata ya Somanda.

"Nitumie nafasi kuwaomba Wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususani katika maeneo yote ambayo Mhe. Makamu wa Rais atapita kujitokeza kwa wingi kumsikiliza kwa kuwa katika maeneo yote ambayo Mhe. Makamu wa Rais atafungua na kuweka mawe ya msingi miradi,   atazungumza na wananchi, " alisema Mtaka.

Mhe. Makamu wa Rais atahitimisha ziara yake Mkoani Simiyu tarehe 08 Machi kwa kuwaongoza wananchi katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa.
MWISHO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,  Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Waandishi wa habari(hawapo pichani)  Ofisini kwake Mjini Bariadi, kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yanayofanyika Mkoani Simiyu pamoja Ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!