Mkuu wa wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
amesema mfumo wa ununuzi wa mazao
mchanganyiko kupitia vyama vya msingi vya Ushirika ( AMCOS) utakaoanza
kutekelezwa mwaka huu 2020 umelenga kuwakomboa wakulima na kuwawezesha kupata soko la uhakika lenye ushindani pamoja na kuwaondoa wanunuzi
wanyonyaji.
Kiswaga
ameyasema hayo jana katika kikao cha
wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika shule ya sekondari Kusekwa Memorial mjini
Bariadi mkoani Simiyu, lengo lilikuwa kujadiliana namna ya kutekeleza maelekezo
yaliyotolewa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.
Hussein Bashe kupitia tangazo alilolitoa
Februari 14, 2020 kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko,dengu ,mbaazi , na soya kupitia
Vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa
mikoa yote inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Amesema
wakulima wa mazao ya jamii ya mikunde pamoja na mbegu wamekuwa wakiuza kiholela
pasipokuwa na mfumo rasmi hali iliyokuwa ikipelekea kuuza kwenye mizani ambayo
haijahakikiwa huku wanunuzi wakijiamlia bei wanazozitaka.
"Serikali imeamua kuja na mpango huo mzuri na lengo
lake kubwa ni kuwakomboa wakulima pamoja
na kuwaondoa wanunuzi wanyonyaji kwani wamekuwa wakinunua mazao kwa wakulima kwa
bei zao wenyewe jambo ambalo linapelekea kuwa na kilimo kisichokuwa na tija;kila
mmoja anayehusika na mazao hayo atashirikishwa tutazifikia kata zetu zote kutoa
elimu,"alisema Kiswaga.
Ameongeza
kuwa mfumo huo wa kuuza kupitia AMCOS
utawezesha kila zao kuwa na bei halisi hatua ambayo itapunguza
manung'uniko ya wakulima juu ya
unyonywaji huku akiwasisitiza pembejeo bora za kilimo ikiwemo mbolea na mbegu bora ili waweze kuwa na kilimo chenye tija.
Sambamba
na hayo aliongeza kuwa changamoto kubwa ya wakulima ni uzalishaji ,masoko na
namna ya upataji wa fedha baada ya kuuza huku akibainisha kuwa mkutano huo ni
mwanzo mzuri wa kuhakikisha wanawasaidia wakulima kuwa wabunifu kwa kujua
wanazalisha nini kwa kiasi gani na uchaguzi sahihi wa mbegu ,matumizi sahihi ya
mbolea na viuadudu.
Kwa
upande wake Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika upande wa uhamasishaji, Bw.
Charles Malunde amesema kuwa mfumo unaoweza kuwanufaisha wakulima na
wenye tija ni wa stakabidhi ghalani na kuwa nguvu ya ushirika inapatikana kwa
jinsi wanaushirika wanavyoshirikiana.
Naye
mkurugenzi wa uendeshaji soko la bidhaa (TMX), Bw. Augustino Mbulumi amesema kupitia
mfumo huu wakulima watapata taarifa za soko kwa mazao yao na watapaswa kupata
malipo ya mazao yao ndani ya saa 48 hivyo ni vema wakafungua akaunti benki ili
kurahisisha mapokezi ya fedha zao.
Akizungumza
kwa niaba ya wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu, Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi Melkizedeck Humbe amesema ni vema kila mmoja akatimiza
wajibu wake ili mfumo huu uweze kufanikiwa huku akibainisha kuwa mfumo huo
utazisaidia Halmashauri kupata takwimu sahihi na namna ya ukusanyaji mapato.
Awali akisoma tangazo la maelekezo ya serikali
kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko
,dengu, mbaazi, soya, na ufuta mrajis
msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Simiyu Ibrahim Kadudu amesema tangazo hilo litaanza
kutumika mwaka huu 2020 ambapo mazao hayo yatauzwa kupitia mfumo wa ushirika
kwa mfumo wa minada ya vyama vikuu vya ushirika katika maeneo yao .
Aidha
imedaiwa kuwa tume ya maendeleo ya ushirika kwa kushirikiana na soko la bidhaa
(TMX) itaendesha minada kwa maeneo maalum kwa mazao hayo kupitia mfumo wa soko
la bidhaa na taratibu zake zitabainishwa na TMX.
Wakizungumza
kwa niaba ya wakulima baadhi viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika Amcos
walisema kuwa ni vema watendaji wa idara ya kilimo na ushirika wakatembelea
kata zote kutoa elimu kwa wakulima ili mfumo huo ufahamike kwa wote.
MWISHO.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi. Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Baadhi ya wadau wa
mazao mchanganyiko mkoani Simiyu, wakifuatilia kikao cha wadau hao kilichofanyika
jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu,
mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa
inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Naibu Mrajisi wa Vyama
vya Ushirika (Uhamasishaji), Bw. Charles Malunde akitoa ufafanuzi wa masuala
mbalimbali katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana
Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu,
mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)kwa mikoa inayolima
mazao hayo kuanzia mwaka huu .2020.
Mrajisi Msaidizi wa
Vyama Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahim Kadudu akitoa ufafanuzi a masuala
mbalimbali katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana
Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu,
mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS)kwa mikoa inayolima
mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Mkurugenzi wa
Uendeshaji Soko la Bidhaa(TMX), Bw.
Augustino Mbulumi akitoa mada katika kikao
cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la
kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein
Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama
vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka
huu 2020.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe akizungumza kwa niaba ya Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Simiyu, katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Bw. James Petro akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Bw. Daniel Masilimbi akichangia hoja katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Baadhi ya viongozi wakifuatilia kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua baadhi ya masuala kwa wadau wa mazao mchangamyiko katika kikao cha wadau hao kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Mtaalam wa masuala ya stakabadhi ghalani akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali katika kikao cha wadau wa mazao mchanganyiko kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Baadhi ya wadau wa
mazao mchanganyiko mkoani Simiyu, wakifuatilia kikao cha wadau hao kilichofanyika
jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu,
mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa
inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Baadhi ya wadau wa mazao mchanganyiko mkoani Simiyu, wakifuatilia kikao cha wadau hao kilichofanyika jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu, mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
Baadhi ya wadau wa
mazao mchanganyiko mkoani Simiyu, wakifuatilia kikao cha wadau hao kilichofanyika
jana Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili namna ya kutekeleza maelekezo ya Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe kuhusu mfumo wa ununuzi wa choroko, dengu,
mbaazi na soya kupitia vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) kwa mikoa
inayolima mazao hayo kuanzia mwaka huu 2020.
0 comments:
Post a Comment