Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka amepiga marufuku wakopeshaji wanaowakopesha walimu, kushikilia kadi zao za kutolea fedha benki
(ATM) na vyeti vya taaluma kama dhamana ya mkopo.
Mtaka ametoa marufuku hiyo wilayani Itilima wakati wa
hafla ya kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa mwaka 2019.
“Walimu jiepusheni na mikopo isiyo na ulazima, benki yenu
ipo itumieni; imefika wakati walimu wanaweka
kadi zao za ATM kama dhamana wengine wanaweka
mpaka vyeti vya taaluma; hii biashara hapana, kitambulisho cha benki na vyeti
ni mali mwalimu,”alisema Mtaka.
Aidha, amewapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayofanya na
kuwaeleza kuwa wana nafasi kubwa ya kuufanya mkoa kufanya vizuri zaidi katika mitihani yote ya Kitaifa ambapo ameeleza kuwa lengo la Mkoa ni kutoka
kwenye nafasi kumi bora na kushika nafasi tatu bora kwa mitihani yote ya
Kitaifa kwa shule za msingi na sekondari.
Katika hatua nyingine Mtaka ameendelea kusisitiza
utekelezaji wa agizo la walimu kupewa kiupaumbele kuhudumiwa katika taasisi za Umma
ili wapate muda wa kwenda kuwafundisha wanafunzi wanaowaacha shuleni wakati
wanapoenda kupata huduma.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wialya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo amesema hali ya ufaulu katika
Halmashauri hiyo imekuwa ikipanda kila mwaka, kutoka asilimia 56.2 mwaka 2016
hadi kufikia asilimia 78.52 mwaka 2019.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini ametoa
wito kwa walimu na wadau wengine wa elimu kutekeleza mkakati wa elimu wa mkoa
kila mmoja kwa nafasi yake ili mkoa uweze kufikia lengo la kuwa miongoni mwa
mikoa mitatu bora.
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga amewapongeza
walimu kwa kazi nzuri waliyofanya na kuahidi kuwa Wilaya hiyo itaendela kufanya
vizuri kimkoa na Kitaifa huku akieleza mpango wa Wilaya ya Itilima kuwa ni
kuhakikisha kila shule ya sekondari wilayani humo inakuwa na bweni.
Nao walimu wa Wilaya ya Itilima wamesema kuwa wataendelea
kufanya kazi kwa bidii huku wakiahidi kutekeleza ikakati yote inayowekwa katika
ngazi ya Mkoa, wilaya mpaka ngazi ya shule ili waweze kufikia azma ya
kuufikisha mkoa katika mikoa tatu bora nchini katika mitihani yote ya Kitaifa.
“Kutokana na mikakati ambayo mkoa umeweka ukiwemo wa
kambi za kitaaluma na wanafunzi kupata chakula cha machana shuleni itasaidia
sana kuinua ufaulu kwa shule za msingi na sekondari,” alisema mwalimu Bindi
Busagala.
Shule na walimu waliofanya vizuri katika mitihani ya
Kitaifa wamepewa zawadi ya vyeti na fedha taslimu.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na walimu wa wilaya ya Itilima katika hafla ya
kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri
katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika
makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Baadhi ya walimu wa
Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo
pichani) wakati akizungumza nao katika hafla ya kuwapongeza kutokana na ufaulu
mzuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020
katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga katika hafla ya kuwapongeza walimu wa Shule ya Msingi na Sekondari wilayani Itilima kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na wilaya ya Itilima wakicheza pamoja na walimu wa Wilaya ya Itilima, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa Shule ya Msingi na Sekondari wilayani Itilima kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019,iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Kutoka kushoto Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya itilima, Mhe. Mahamoud Mabula, Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga wakicheza pamoja na baadhi ya viongozi na walimu wa Wilaya ya Itilima, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa Shule ya Msingi na Sekondari wilayani Itilima kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima, Bi. Elizabeth Gumbo akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya elimu ya wilaya hiyo, katika hafla ya kuwapongeza walimu wa Shule ya Msingi na Sekondari wilayani Itilima kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na walimu wa wilaya ya Itilima katika hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019,iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Baadhi ya walimu wa Wilaya ya Itilima wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akizungumza nao katika hafla ya kuwapongeza kutokana na ufaulu mzuri katika Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba na Kidato cha Nne mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi cheti na fedha taslimu Mmoja wa Walimu wa Wakuu, katika hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akizungumza na walimu wa wilaya ya Itilima katika hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020 katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
Vijana wa Skauti wa
Wilaya ya Itilima wakimvika skafu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika
hafla ya kuwapongeza walimu Shule ya Msingi na Sekondari kutokana na kufanya
vizuri katika Mitihani ya Taifa mwaka 2019, iliyofanyika Februari 28, 2020
katika makao makuu ya Wilaya ya Itilima Lagangabilili.
0 comments:
Post a Comment