Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameagiza
Shirika la Mawasiliano nchini TTCL kufikisha mkongo wa Taifa katika Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu ili vifaa vinavyotumika kutoa huduma vinavyowezeshwa
na Mtandao wa Intanenti viweze kufanya kazi yake sawa.
Mhe. Makamu wa Rais
ameyasema hayo wakati akifungua Jengo la Huduma kwa Wateja la TTCL Mkoa wa
Simiyu Machi 07, 2020 mjini Bariadi , ambapo amewahimiza watendaji wa TTCL
kutoa huduma bora na kwa ufanisi.
Aidha,
Mhe. Makamu wa Rais ametoa wito kwa wananchi kutunza na kulinda miundombinu ya
mawasiliano na watakaobainika kuhujumu miundombinu hiyo watashtakiwa kama
wahujumu uchumi.
0 comments:
Post a Comment