Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa
wananchi wa Wilayani ya Busega kutokaa na fedha majumbani badala yake watumie
Taasisi za kifedha kutunza fedha zao kwa ustawi wa maisha yao na Usalama wa
Fedha zao.
Mhe. Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati
akifungua tawi la NMB Nyashimo wilayani Busega Machi 06, 2020 ambapo
ameipongeza benki huyo kusogeza huduma karibu
na wananchi.
"Wilaya
hii ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla una uchumi mkubwa, mna uchumi
utokanao na ziwa yaani uvuvi, uchumi wa mifugo, uchumi wa kilimo; hivyo sikae
na fedha mikononi pelekeni benki ili benki itumie kwa maendeleo yetu na ya
kwako binafsi," alisema Mhe. Makamu wa Rais.
Katika
hatua nyingine Mhe. Makamu wa Rais ameipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha
huduma za bima na huduma maalum kwa ajili ya kundi la waendesha pikipiki
(bodaboda) na kubainisha kuwa huduma hiyo umechangia kuwapunguzia hali ya kubaki
na fedha mfukoni na kuwapunguzia haki ya kuendelea kuwashawishi wanafunzi wa
kike na kuwalaghai na wakati mwingine kuwapa ujauzito.
Naye Naibu
Waziri wa Fedha, Mhe. Ashatu Kijaji ameagiza Benki Kuu ya Tanzania kukaa na
benki nyingine nchini ili kujadili namna ya kupunguza riba kwa
wakopaji(wananchi) kwa kuwa Serikali imezipunguzia benki hizo riba katika
mitaji ya kuendeshea benki hizo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Benki ya NMB kwa
namna ambavyo imekuwa ikichangia katika maendeleo ya Mkoa wa Simiyu ambapo hadi
sasa imechangi shilingi milioni 200 katika sekta ya Elimu.
MWISHO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan(wa pili kulia) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi la NMB Busega,
katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Simiyu, Machi 06, 2020.
Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali pamoja na viongozi wa
Benki ya NMB wakishangilia mara baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan(wa pili kulia) kufungua Tawi la NMB
Busega, katika siku ya kwanza ya ziara yake Mkoani Simiyu, Machi 06, 2020.
Jengo
la Tawi la NMB Busega lililofunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Machi
06, 2020.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan akielekea eneo la Jukwaa kwa ajili ya kwenda kuzungumza na
wananchi mara baada ya kuzindua Tawi la NMB Busega, katika siku ya kwanza ya
ziara yake Mkoani Simiyu, Machi 06, 2020
0 comments:
Post a Comment