Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaongoza wananchi
katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniania ambayo yamefanyika Kitaifa katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.
Maadhimisho haya yenye
Kauli Mbiu “Kizazi cha Usawa Kwa Maendeleo ya Tanzania ya Sasa na ya Baadaye” yamehudhuriwa
na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali waliopo madarakani na wastaafu
wakiwemo Mama Getrude Mongela, Mama Anna Abdallah, Spika Mstaafu wa Bunge la
Tanzania, Mhe. Anne Makinda, Mwenyekiti wa UWT Taifa, Ndg. Gaudensia Kabaka,
Katibu wa UWT Taifa, Ndg. Queen Mlozi na viongozi wengine
Katika maadhimisho
hayo Mhe. Makamu wa Rais ametembelea mabanda ya Maonesho ya kazi mbalimbali za
wanawake, mashirika, taasisi na wadau wa maendeleo wanaojihsisha na masuala ya
wanawake na baadaye akapokea maandamano ya wanawake kutoka maeneo mbalimbali
nchini.
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea
Maandamano kwenye Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika
Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri Bariadi Mkoani Simiyu leo March
08,2020.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Wananchi Wanawake Mkoani Simiyu
wakiwa kwenye Maandamano ya kusherehekea Maadhimisho ya siku ya
Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji
wa Bariadi Mkoani Simiyu March
08,2020. (Picha na
Ofisi ya Makamu wa Rais )Wananchi Wanawake Mkoani Simiyu wakiwa kwenye Maandamano ya kusherehekea Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Mkurugenzi Mipango wa Pamba Samweli Kilua akimkabidhi Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba Mkoani Simuyu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwenye maonesho ya kilele cha siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauriya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya aina ya bidhaa ya kitenge alipotembelea Banda la Benki ya Posta Tanzania TPB Tawi la Simiyu kwenye maonesho ya kilele cha siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu March 08,2020. .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Baadhi ya viongozi na wadau walioshiriki katika Kilele cha Maadhimisho ya Wanawake Duniani Machi 2020, yaliyofanyika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akimtuza Msanii
na Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe. Vick Kamata
wakati alipotumbuiza kwa wimbo maalum katika kilele cha Maadhimisho ya
siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika Kitaifa katika Uwanja wa Halmashauri
Bariadi Mkoani Simiyu March 08,2020. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
0 comments:
Post a Comment