MaktabaPICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI MKOANI

KUAPISHWA KWA WAKUU WA WILAYA ZA MKOA WA SIMIYU

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo S. Kiswaga akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) Julai Mosi, 2016. (Picha  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Seif A. Shekalaghe akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) Julai 01, 2016. (Picha  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Joseph E. Chilongani akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simyu, Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) Julai 01, 2016. (Picha  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J.Mtaka (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Simiyu ( Kushoto na kulia kwake) na baadhi ya Viongozi wa madhehebu ya dini wa Mkoa wa Simiyu, (wa kwanza kushoto) Mchungaji wa K.K.K.T Bariadi, Harold Mkaro.(wa pili kulia), Sheikh wa Mkoa , Mahamoud Kalokola baada ya kukamilisha zoezi la kuwaapisha wakuu wa wilaya, Julai Mosi, 2016. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)

 
Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano S. Mwera akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) Julai 01, 2016. (Picha  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Benson S. Kilangi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) Julai 01, 2016. (Picha  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Benson Kilangi akipokea kitabu cha dini kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini kabla ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J. Mtaka Julai 01, 2016. (Picha  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Joseph E. Chilongani akipokea Katiba Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoka kwa  Mkuu wa Mkoa wa Simyu, Anthony J. Mtaka mara baada ya kuapishwa Julai 01, 2016. (Picha  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J. Mtaka (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano S. Mwera (kulia) baada ya kuapishwa, Julai Mosi, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J. Mtaka (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo S. Kiswaga (kulia)baada ya kupishwa, Julai 01, 2016. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)

Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Anthony J. Mtaka (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Seif A. Shekalaghe (kulia) baada ya kuapishwa, Julai Mosi, 2016. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony. J. Mtaka (kushoto) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Joseph E. Chilongani (kulia) mara baada ya kuapishwa Julai Mosi, 2016. Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J.Mtaka (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Simiyu (kushoto ni Seif Shekalaghe (Maswa), Benson Kilangi (Itilima) , Tano Mwera (Busega) na (kulia) Festo Kiswaga (Bariadi) na Joseph Chilongani (Meatu). (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J.Mtaka (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Simiyu ( Kushoto na kulia kwake), waliosimama ni Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Simiyu. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J.Mtaka (wa nne kulia)  na Katibu Tawala Mkoa  Simiyu, Jumanne A. Sagini (wa nne kushoto) na wajumbe wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,  wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Simiyu. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
)

Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani) akizungumza nao mara baada kuapishwa. Kutoka kulia Festo Kiswaga (Bariadi),Benson Kilangi (Itilima),  Seif Shekalaghe (Maswa), Josph Chilongani (Meatu) na Tano Mwera (Busega). Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J.Mtaka (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Simiyu ( Kushoto na kulia kwake), waliosimama na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Simiyu. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony J.Mtaka (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa wilaya za Mkoa wa Simiyu ( Kushoto na kulia kwake) waliosimama na Wajumbe wa Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya zote za  Mkoa wa Simiyu. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa)


Mkuu wa Wilaya ya Busega Tano S. Mwera akipokea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simyu, Anthony J. Mtaka, mara baada ya kuapishwa,  Julai Mosi, 2016. (Picha  na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu) 

MAKABIDHIANO YA MAKATIBU TAWALA WA MKOA WA SIMIYU

Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa, Bibi. Mwamvua A. Jilumbi akisaini taarifa ya makabidhiano kabla ya kumkabidhi mrithi wake Bw. Jumanne A. Sagini Mei 02, 2016.(Picha Na Stella A. Kalinga)
Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa, Bibi. Mwamvua A. Jilumbi akimkabidhi  Katibu Tawala Mkoa Mpya Bw. Jumanne A. Sagini taarifa ya ya Mkoa Mei 02, 2016. (Picha Na Stella A. Kalinga)
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne A. Sagini akisaini taarifa ya mkoa mara baada ya kukabidhiwa na mtangulizi wake katika nafasi hiyo Bibi. Mwamvua A. Jilumbi, Mei 02, 2016.(Picha Na Stella A. Kalinga)
Aliyekuwa Katibu  Tawala Mkoa Bibi.Mwamvua Jilumbi na Katibu Tawala Mkoa Mpya Bw. Jumanne A. Sagini wakisaini taarifa na nyaraka mbalimbali mara baada ya kufanya makabidhiano Mei 02, 2016. (Picha Na Stella A. Kalinga)


Baadhi ya Wakuu wa Sehemu na Vitengo wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Mpya Bw. Jumanne A. Sagini akizungumza na Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu mara baada ya makabidhiano Mei 02, 2016. Kutoka kushoto Bw. Albert D. Wegina (Katibu Tawala Msaidizi-Mipango na Uratibu), Dkt. Matoke Muyenjwa (Kaimu Mganga Mkuu Mkoa), Bw. Hamis J. Waziri (Mkaguzi wa Ndani mkuu), na Bw.Maganga B. Simon(Picha na Stella A. Kalinga)


Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne A. Sagini akisalimiana  Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na mtangulizi wake katika nafasi hiyo Bibi. Mwamvua A. Jilumbi, Mei 02, 2016.(Picha Na Stella A. Kalinga)


Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bw. Jumanne A. Sagini akizungumza na wakuu wa Seksheni na Vitengo wa Sekretraieti ya Mkoa (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa Ofisi na mtangulizi wake katika nafasi hiyo Bibi. Mwamvua A. Jilumbi, Mei 02, 2016.(Picha Na Stella A. Kalinga)

MAKABIDHIANO YA WAKUU WA  MKOA SIMIYU


Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka akipokelewa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Simiyu na wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , Kushoto ni Mkuu wa Mkoa anayemaliza muda wake Mhe. Elaston J. Mbwilo.(Picha na Stella Kalinga) 


Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka akipokelewa na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa , Kushoto ni Mkuu wa Mkoa anayemaliza muda wake Mhe. Elaston J. Mbwilo.(Picha na Stella Kalinga)

Mkuu wa Mkoa anayemaliza muda wake Mhe. Elaston J. Mbwilo (katikati) akimkabidhi nyaraka mbalimbali za ofisi Mhe. Anthony J. Mtaka Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu ofisini kwake, kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Joseph S. Nandrie.(Picha na Stella Kalinga)

Mkuu wa Mkoa anayemaliza muda wake Mhe. Elaston J. Mbwilo (katikati) akimkabidhi nyaraka mbalimbali za ofisi Mhe. Anthony J. Mtaka Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu ofisini kwake, kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Joseph S. Nandrie.(Picha na Stella Kalinga)

Mkuu wa Mkoa anayemaliza muda wake Mhe. Elaston J. Mbwilo (katikati) akipeana mkono baada ya makabidhiano ya nyaraka za ofisi na  Mhe. Anthony J. Mtaka Mkuu mpya wa Mkoa wa Simiyu ofisini kwake, kulia ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Joseph S. Nandrie.(Picha na Stella Kalinga)

Kutoka kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Joseph S. Nandrie, Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe. Georgina Bundara, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Ponsiano Nyami, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe. Rosemary Kirigini na Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Paul Mzindakaya wakisikiliza jambo ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wakati wa makabidhiano .(Picha na Stella Kalinga)

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu wakishuhudia makabidhiano ya kiofisi kati ya Mkuu wa Mkoa anayemaliza muda wake Mhe. Elaston J. Mbwilo na Mkuu wa Mkoa mpya Mhe. Anthony J. Mtaka. (Picha na Stella Kalinga)

0 comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!