Mkoa
wa Simiyu utahakikisha vifo vya akina mama wajawazito na watoto
wachanga vinapungua kwa kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imewekeza
na kutumia gharama kubwa katika kuandaa wataalam(wakunga) wenye jukumu la kuhakikisha
wanatoa huduma zitakazotoa majibu sahihi ya utatuzi wa changamoto hiyo.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga wakati akifunga
mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za dharura kwa wakina mama na
watoto wachanga chini ya mradi wa Mkunga Okoa Maisha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka yaliyohusisha wakunga kutoka katika Halmashauri
zote sita mkoani humo.
Kiswaga
amesema pamoja na kuwepo dalili za kupungua kwa vifo vya akina mama wajawazito
na watoto wachanga mkoani huo bado ipo
haja ya kujitathmini ili kubaini ukubwa wa tatizo kama njia ya kulipatia
ufumbuzi wa kudumu.
“
Ni kweli ukilinganisha takwimu za mwaka jana na mwaka huu zinaonyesha idadi ya
vifo vinavyotokana na matatizo mbalimbali ya uzazi vimepungua, lakini naomba
niwape angalizo, tusizichukulie takwimu
hizi kama kigezo cha ubora wa huduma zinazotolewa katika vituo vyetu, bali iwe
chachu ya kufanya kazi kwa bidii ili
fikapo mwezi Desemba mwaka huu tuwe katika nafasi ya juu zaidi”.
Aidha
Kiswaga amewaasa wahitimu wa mafunzo hayo kuhakikisha wanaitumia kikamilifu
elimu waliyoipata ili iwawezeshe kukabiliana na dharula wakati wa kuwahudumia
wakina mama wajawazito na watoto wachanga na kuongeza kuwa serikali
haitamvumilia mkunga yeyete atakayetumia kisingizio cha aina yoyote kwa
kusababisha kifo cha mama au mtoto.
Halikadhalika
Kiswaga ameishukuru serikali ya Canada kupitia chama cha wakunga cha nchi hiyo
CAM na kusema kuwa imefanya uamuzi sahihi wa kuisaidia Tanzania katika eneo
hili nyeti la kuwajengea uwezo wataalamu hao watakaotumika kuboresha huduma
za afya ya mama na mtoto na kuahidi kuwa
serikali iko tayari kupokea ushauri utakaosaidia kukabiliana na changamoto
hiyo.
Kwa
upande wake rais wa chama cha wakunga Tanzania TAMA Feddy Mwanga amesema tafiti za hivi karibuni
zinaonyesha kuwa mkunga mwenye mafunzo yuko katika nafasi nzuri zaidi ya
kukabiliana na changamoto zinazowakabili akina mama wajawazito na watoto
wachanga kwa 87%.
“
Hivyo kwa sisi wakunga tunaamini hatua hiyo ni nzuri na kwamba kinachofuata
sasa ni kuwahimiza wakina mama wahudhurie kliniki mapema na kwa wakati na hapa
ndipo tunaweza kupima mafanikio ya mpango huu kupitia kwa wahitimu hawa tunaowakabidhi
vyeti hii leo” alisema Bi Mwanga.
Akizungumza
kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo hayo yaliyobebwa na kauli mbiu ya Mkunga Okoa Maisha
-Jonas Julius ameiomba Serikali kuboresha mazingira yao ya kutolea huduma
ikiwemo kuwapatia nyumba za kuishi jirani na vituo vya kazi sambamba na
kuwaendeleza kitaaluma ili waweze kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.
Mkoa
wa Simiyu una jumla ya wakunga 500 ambapo
kupitia mpango huo jumla ya wakunga 220 wamenufaika na mafunzo hayo
yanayofadhiliwa na CUSO International, Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) pamoja
na Chama cha wakunga Canada (CAM) .
MWISHO
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifunga mafunzo ya wakunga yanayohusu
utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga chini
ya Mradi wa Mkunga Okoa Maisha, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
Rais
wa chama cha wakunga Tanzania TAMA Feddy
Mwanga akitoa taarifa ya mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za
dharura kwa akina mama wajawazito na
watoto wachanga chini ya Mradiwa Mkunga Okoa Maisha, wakati wa hafla ya kufunga
mafunzo hayo mkoani Simiyu, Septemba 28, 2018.
Mkunga
Jonas Julius akisoma risala mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga aliyefunga mafunzo ya wakunga yanayohusu utoaji wa huduma za dharura
kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga chini ya Mradi wa Mkunga Okoa Maisha,
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
Mwakilishi
wa Chama cha Wakunga cha nchini Canada (CAM) Bi. Sylivia akitoa uzoefu wake wa
namna wakunga wanavyofanya kazi nchin humo, wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina
mama wajawazito na watoto wachanga, iliyofungwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,
Septemba 28, 2018.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Mugune Maeka akizungumza jambo katika hafla
ya kufunga mafunzo ya
utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, iliyofungwa
na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswa(katikati walioketi) akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Chama cha wakunga nchini (TAMA), Mwakilishi wa Chama cha
Wakunga cha nchini Canada (CAM) Bi. Sylivia, baadhi ya viongozi wa mkoa wa
Simiyu na baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu walioshiriki mafunzo ya yanayohusu utoaji wa huduma za
dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, baada ya kufunga mafunzo
hayo Septemba 28, 2018.
Mwakilishi
wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Grace Mgombera akizungumza jambo katika
hafla ya kufunga mafunzo ya yanayohusu
utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, iliyofungwa na Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
Baadhi
ya wakunga wa mkoa wa Simiyu walioshiriki mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina
mama wajawazito na watoto wachanga, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga aliyefunga mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswa(wa pili kulia) pamoja na viongozi wa
Chama cha wakunga nchini (TAMA), , baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na
baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu wakiimba wimbo pamoja na wakunga(hawapo
pichani) walioshiriki mafunzo ya ya
utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, kabla
ya kufunga mafunzo hayo Septemba 28, 2018.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswa(wa pili kulia) pamoja na viongozi wa
Chama cha wakunga nchini (TAMA), baadhi ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na
baadhi ya wakunga wa mkoa wa Simiyu wakiimba wimbo pamoja na wakunga(hawapo
pichani) walioshiriki mafunzo ya ya
utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga, kabla
ya kufunga mafunzo hayo Septemba 28, 2018.
Baadhi
ya wakunga wa mkoa wa Simiyu walioshiriki mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito
na watoto wachanga, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
aliyefunga mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka, Septemba 28, 2018.
Baadhi
ya wakunga wa mkoa wa Simiyu walioshiriki mafunzo ya utoaji wa huduma za dharura kwa akina
mama wajawazito na watoto wachanga, wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga aliyefunga mafunzo hayo, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka, Septemba 28, 2018.