Vijana takribani 4200 hapa nchini
wanatarajia kunuafaika na kilimo kupitia mradi wa kitalu nyumba(green house),
ambao utaanza kutekelezwa katika mikoa sita ambayo imekuwa kinara kwa kutenga
maeneo kwa ajili ya shughuli za vijana, ukiwemo mkoa wa Simiyu na Halmashauri
zake zote sita.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri ,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi ,Vijana Ajira na Walemavu Mhe.
Anthony Mavunde hiyo wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu yenye lengo la kukagua
maeneo ya ujenzi wa vitalu nyumba na uwepo wa maji yatakayotumika katika kilimo cha umwagiliaji.
Mvunde amesema katika kutekeleza mradi huo vijana
watawezeshwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili iwe sehemu ya ajira yao,
ambapo vijana watafundishwa kulima kwa tija kupitia kitalu nyumba na kujua
namna ya kutengeneza vitalu nyumba na wananchi wengine wanapohitaji kujifunza
namna ya kutengeneza vitalu nyumba wajifunze kwao.
“Tutaleta green house (Kitalu nyumba) ambayo itafungwa
hapa na vijana wataelekezwa kulima kupitia huko, lakini pia tutawaunganisha na
chama cha Wauza mboga Tanzania kwa ajili ya kutengeneza masoko ya uhakika ili
green house (kitalu nyumba) hizo ziwe na tija” alisema Naibu Waziri Mavunde.
Akiwa katika ziara yake Naibu Waziri huyo amekutana na
baadhi ya vijana ambao watatekeleza mradi huo na kuwapongeza kwa uamuzi
waliochukua na akatoa rai kwa vijana wote nchini kuachana kukaa vijiweni na badala yake wajishughulishe na
teknolojia hiyo ili waondokane na umasikini.
Akiwa wilayani Busega, Bariadi na Itilima Mavunde
ameeleza kuridhishwa kwake na maeneo yaliyotengwa na akatoa wito kwa viongozi
wote kuwalea vijana wote watakaoanza kutekeleza mradi huo ili mradi huo uweze
kuwa endelevu na uweze kuwaletea tija.
Mkuu wa Mkoa wa Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru Serikali kwa mpango huo ambao
utawasaidia vijana kujiajiri kupitia vitalu nyumba na akamhakikishia Naibu
Waziri kuwa mkoa wa Simiyu utahakikisha vijana wanafanya vizuri katika mradi
huo.
Mkuu wa wilaya ya Itilima amesema pamoja na vijana
wilayani humo kujiandaa na mradi wa kilimo kwa kutumia kitalu nyumba Wilaya
hiyo pia imeweka mpango wa kutoa mafunzo ya ujasiriamali na ufundi stadi
yatakayowawezesha kupata maarifa ya namna ya kufanya shughuli za ujasiriamali
na ufundi kama ajira zao.
Kwa upande wao vijana watakaofaidika na mradi wa kitalu
nyumba wamesema wanaupokea mradi huo kwa mikono miwili na wakaomba Serikali
iwasaidie kupata mikopo ili waweze kununua vifaa vya kisasa hususani mashine na
zana za kilimo zitakazowawezesha kutekeleza mradi huo.
“Mradi huu sisi vijana tunaupokea kwa mikono miwili ombi
letu kwa serikali tusaidiwe mikopo itakayotuwezesha kupata mtaji utakatufanya
vijana tunufaike na kilimo, tupate vifaa bora kama mashine za kumwagilia na
zana nyingine za kilimo ili tuweze kulima kisasa” alisema Matogolo Samwel
kutoka Mwanyili wilayani Busega.
Katika ziara hiyo Mavunde ametembelea Halmashauri ya
wilaya ya Busega, Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika viwanja vya nane nane Nyakabindi na Halmashauri
ya Wilaya ya Itilima makao makuu ya Wilaya Lagangabilili.
MWISHO
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akimwagilia bustani ya kijana Matogolo Samwel wa
Kijiji cha Mwamanyili wilayani Busega, wakati wa Ziara ya kukagua maeneo
yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa vitalu nyumba mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akikagua eneo litakalotumika kujenga vitalu
nyumba Halmashauri ya Mji wa Bariadi katika Viwanja vya Nanenane Nyakabindi,
wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo hayo mkoani Simiyu.
:-Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Mhandisi. Mohammed
Ali akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi,
Ajira, Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde(mwenye miwani) juu ya eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi
wa Kitalu nyumba lililopo Mwamanyili, wakati akiwa katika zi ara ya kukagua
maeneo hayo mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde(wa pili kulia mbele) akizungumza na viongozi na baadhi ya Vijana wa
Itilima, alipotembelea eneo la ujenzi wa Vitalu Nyumba
Lagangabilili akiwa katika ziara ya kukagua maeneo hayo mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu(baadhi hawapo pichani) mara
baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa ajili ya ziara ya kukagua maeneo
yaliyotengwa kujenga vitalu nyumba mkoani humo, (kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt. Joseph Chilongani.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza wakati
ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira,
Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde, aliyofanya mkoani humo kwa ajili ya
kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde(mwenye miwani), Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu
Silanga(katikati) na Mkuu wa Wilaya
ya Itilima, Mhe. Benson Kilangi(kulia) wakifurahia pamoja na wanafunzi wa
Shule ya sekondari Kanadi na baadhi ya viongozi wa Mkoani Simiyu wakati Naibu Waziri
Mavunde akiwa katika ziara ya kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba
mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia vifaa vya ufundi uashi vinavyotumiwa
na vilivyotolewa na Shirika la World Vision kama msaada vijana wa Kanadi,
wakati wa ziara yake ya kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba mkoani Simiyu.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia asali inayozalishwa na vikundi vya
Vijana wilayani Itilima, wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira,
Vijana na Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde, wakati wa ziara ya mkoani humo.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Bunge, Sera, Kazi, Ajira, Vijana na
Walemavu, Mhe. Anthony Mavunde akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya ya Itilima mara baada ya kuwasili wilayani humo kwa ajili ya ziara ya
kukagua maeneo ya kujenga vitalu nyumba mkoani Simiyu.
0 comments:
Post a Comment