Thursday, November 29, 2018

RC MTAKA ATOA WITO KWA WALIMU KUEPUKA VITENDO VINAVYOHARIBU HAIBA NA HESHIMA YA UALIMU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa walimu kuendelea kuwa walezi wa wanafunzi wao na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoharibu haiba na heshima ya ualimu, ili waweze kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili kwao na kwa wanafunzi wanaowafundisha.


Mtaka ameyasema hayo Novemba 28, 2018 katika mahafali ya 26 ya kidato cha nne shule ya sekondari Mwembeni (ambayo alisoma kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 1997-mwaka 2000),  iliyopo Mjini Musoma ambapo alikuwa mgeni rasmi.

Amesema katika baadhi ya maeneo baadhi ya walimu wamekuwa wakifanya mambo ambayo yanaharibu heshima na haiba ya ualimu jambo ambalo linapelekea wazazi kutowaamini walimu na kuogopa kuwapeleka watoto wao katika shule hizo.

" Naishukuru sana bodi ya shule na walimu wa Mwembeni kwa kuendelea kuhakikisha walimu wetu wanalinda heshima na haiba ya ualimu na wazazi wameendelea kuiamini shule kwa kuleta watoto wao, kwa sababu hakuna matukio yanayohatarisha uwepo wa watoto wao shuleni na masuala la elimu, maadili na nidhamu kwenye shule hii kama Taasisi yameendelea kuimarishwa" alisema.

Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa wazazi, walezi na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wanafunzi waliosoma katika shule ya Mwembeni miaka ya nyuma kuchangia katika ujenzi wa shule(vyumba vya madarasa) ili kupanua wigo kwa wanafunzi kuanza kusoma masomo ya sayansi, ikizingatiwa kuwa katika dunia ya sasa ni ya ushindani wa sayansi na teknolojia.

"Dunia tunayoiendea sasa ni ya ushindani wa sayansi na teknolojia na kama shule imejielekeza kwenye masomo ya sayansi ni jambo la kuungwa mkono; niwaalike wenzangu wote tuliosoma katika shule ya sekondari Mwembeni kuona haja ya kurejesha kwenye shule katika kile tulichopata katika shughuli zetu za kimaisha, tukirejeshe tujenge shule yetu ili iendelee kuwa kwenye ushindani mkubwa na kuwa miongoni mwa shule bora mkoani Mara" alisisitiza Mtaka.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwembeni, Bro.Erasmus Marando amewaomba wadau wasaidie kujenga vyumba zaidi vya madarasa, shule hiyo ianze kutoa masomo ya mchepuo wa sayansi, ili kuwaanda wataalam watakaoenda sambamba na sera ya Serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya Viwanda.

Naye Mwalimu Anselm Mnibhi ambaye amemfundisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika Shule ya Sekondari ya Mwembeni mwaka 1997 hadi mwaka 2000, amemshukuru kwa kukumbuka shule aliyosoma na kuonesha nia ya kusaidia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na kubainisha kuwa hakuna mwanafunzi yeyote aliyesoma hapo zamani aliyeonesha nia na dhamira hiyo na akawaomba wote waliosoma shuleni hapo kujitoa kujenga shule yao.

Kwa upande wake mhitimu wa Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni, Sharon Buganda ametoa wito kwa wanafunzi waliobaki kuondokana na dhana ya kuogopa kusoma masomo ya sayansi wakiamini kuwa ni magumu, badala yake wasome masomo hayo ili waweze kuwa wataalam wajao katika maeneo mbalimbali ikiwemo  viwanda ambavyo ni sera ya Serikali ya Awamu ya tano.

Katika mahafali hayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka aliahidi kuchangia shilingi milioni tano na kuhamasisha wenzake aliosoma nao shuleni hapo Mwembeni kuchangia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa vitakavyotumika na wanafunzi wa mchepuo wa sayansi, kutoa zawadi ya shilingi milioni moja (kwa mwanafunzi wa kiume) na shilingi milioni moja na laki tano(kwa mwanafunzi wa kike) atakayekuwa miongoni mwa wanafunzi kumi bora Kitaifa  katika mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2018.
MWISHO


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni Mjini Musoma, ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo iliyofanyika shuleni hapoNovemba 28, 2018.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na Mwl.Anselm Mnibhi wa Shule ya Sekondari Mwembeni ambaye pia alimfundisha yeye akiwa mwanafunzi wa shule hiyo mwaka 1997-2000, wakati wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo,  iliyofanyika shuleni hapoNovemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye kipaza sauti) akiwa na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997- mwaka 2000 na baadhi ya walimu waliwafundisha, katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa  shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani ya ngoma ya asili ya kabila la Wakurya, katika  mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  alikuwa mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997- mwaka 2000 na baadhi ya walimu waliowafundisha, katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.

Baadhi ya wazazi na walezi wa wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwembeni  wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018. 


Loveness Leonidas mhitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwembeni Mjini Musoma akisoma risala kwa niaba ya wenzake, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.




Mhitimu wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari Mwembeni Mini Musoma Pius Mwita akipokea cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,  katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwembeni ya Mjini Musoma Bro. Erasmus Marando(kulia) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa mgeni rasmi  , katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwembeni ya Mjini Musoma Bro. Erasmus Marando(kushoto ) na Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo Dkt. Mniko wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018. 
Mkuu wa shule ya Sekondari Mwembeni ya Mjini Musoma Bro. Erasmus Marando(kushoto) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka , katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi.


Vijana wa Skauti wa Shule ya Sekondari Mwembeni ya mjini Musoma wakimvisha skafu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka , kama ishara ya upendo kwake na kumkaribisha katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwemeni ya Mjini Musoma, wakifuatilia masuala mbalimbali, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wazazi, walimu, walezi , wanafunzi na wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwembeni ya mjini Musoma, ambapo alikuwa mgeni rasmi, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akiwatambulisha wenzake alisoma nao katika Shule ya Sekondari ya Mwembeni ya Mjini Musoma, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi .
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (mwenye kipaza sauti) akiwa na wenzake aliosoma nao katika shule ya sekondari Mwembeni mwaka 1997-2000 na baadhi ya walimu waliwafundisha, katika  mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne wa  shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo alikuwa mgeni rasmi.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani, katika  mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  alikuwa mgeni rasmi.
Mhitimu wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari Mwembeni Mini Musoma Jesca Gozbert  akipokea cheti cha pongezi kwa kufanya vizuri katika masomo yake kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,  katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambapo alikuwa Mgeni rasmi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Mwembeni Mjini Musoma, ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe Anthony Mtaka akisaini kitabu cha wageni katika Shule ya Sekondari Mwembeni ya Mjini Musoma ambako alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.
Baadhi ya walimu na watumishi wasio walimu wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwembeni mjini Musoma wakitoa burudani, katika  mahafali ya 26 ya ya wanafunzi wa kidato cha nne wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka  alikuwa mgeni rasmi.
Afisa Elimu (Sekondari) wa Manispaa ya Musoma akizungumza na wazazi, walimu, walezi , wanafunzi na wahitimu wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwembeni ya mjini Musoma, ambapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka alikuwa mgeni rasmi, katika mahafali ya 26 ya wanafunzi wa kidato cha nne  wa shule hiyo iliyofanyika shuleni hapo Novemba 28, 2018.

Monday, November 26, 2018

RC MTAKA ATOA WITO KWA KKKT KUENDELEA KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO, HUDUMA ZA JAMII SIMIYU

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameliomba Kanisa la Kiinjili na Kilutheri Tanzania (KKKT) kuendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo na huduma mbalimbali za jamii mkoani hapa.

Mtaka ameyasema hayo Novemba 25, wakati alipozungumza na waumini wa Kanisa hilo katika Usharika wa Tumain Bariadi Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, ambapo alikuwa mgeni rasmi katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10'ya vyoo katika Shule Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo.

Amesema kanisa hilo limekuwa na mchango mkubwa katika miradi mingi ya maendeleo hususani katika sekta ya elimu, afya, maji na maeneo mengine muhimu ikiwemo sekta ya fedha ambapo Kanisa hilo linamiliki Benki ya Maendeleo.

"Pamoja na mradi huu wa shule ya msingi, tunaendelea kuliomba Kanisa kuona umuhimu wa kuwekeza katika miradi mingine ya maendeleo kwenye mkoa wetu; Kanisa lina hospitali, benki na vyuo vikuu; huu ni mkoa ambao bado haujawa na vyuo vikuu vingi kwa hiyo ipo nafasi kwa kanisa kuona kama linaweza kuwa na chuo cha ufundi, chuo cha kati au Tawi la Chuo Kikuu au kuwekeza katika eneo jingine ."alisema Mtaka.

Aidha, amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa kuwa limekuwa sehemu ya mafanikio ya nchi yetu tangu imepata uhuru, kwani wapo Viongozi na Watanzania wengi katika maeneo tofauti nchini ambao wamepata elimu katika Vyuo na shule za kanisa, huku akisisitiza kanisa kuendelea kuombea amani na mshikamo wa nchi.

Naye Askofu wa KKKT, Dayosis ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala amesema Kanisa litaendelea kushirikiana Serikali katika kuwafanya watu.wamjue Mungu na kuwaletea wananchi maendeleo, ambapo amebainisha kuwa ujenzi wa shule ni moja ya njia za kushirikiana na Serikali katika kuondoa ujinga na kujenga Taifa lenye watu walioelimika jambo ambalo litairahisisha Serikali katika kuwaongoza wananchi wake.

"Kanisa litaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha watu wa Simiyu katika wilaya zote wanamjua Mungu; tunajenga shule ili tuondoe ujinga watu waelimike, ujinga ukiondoka hata Serikali inapata nafuu kuwaongoza watu wake" alisema Askofu Makala.

Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi, Katibu wa Kamati ya Ujenzi, Mwl. Oberlin Kileo amesema ujenzi wa Shule ya Tumaini ulianza mwaka 2012, ambapo jumla ya vyumba vya madarasa tisa, matundu ya vyoo 10, jiko, stoo na viwanja vya michezo vilijengwa na kugharimu shilingi milioni 200 zikijumuisha na gharama za uwekaji wa miundombinu ya maji na umeme.

Ameongeza kuwa ili kujenga vyumba vya madarasa vitano na matundu 10 ya vyoo vivyokusudiwa kujengwa kwa awamu ya pili jumla ya shilingi milioni 120 zinahitajika.

Katika harambee hiyo jumla ya shilingi 41,526,500/= zilipatikana, kati ya hizo fedha taslimu zikiwa ni shilingi 7,466, 500  na ahadi shilingi 34, 060,000/= pamoja na vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo  mifuko 60 ya saruji, nondo tani moja, mchanga lori kubwa nne na kokoto tripu mbili.
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akimsikiliza Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya  Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
.Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakifurahia jambo katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka( wa pili kushoto) akiimba pamoja na Kwaya ya Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi  ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi, mstari pili ni Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto walioketi kwenye viti) na Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala wakiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam, mara baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi  ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Waimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakiimba pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mchungaji wa KKKT Bariadi, Greyson Kinyaha, mara baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi..
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Maswa , Mhandisi. Paul Jidayi akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, wakifuatilia masuala mbalimbali katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala akizungumza na waumini wa kanisa hilo katika Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na viongozi wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika wa Tumaini Bariadi na Kamati ya Ujenzi ya Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School), baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule hiyo inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Kwaya ya Uinjilisti KKKT Kijitonyama, viongozi wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika wa Tumaini Bariadi Mjini Bariadi, baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School)  inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) katika picha ya pamoja na Kwaya ya Uinjilisti KKKT Bariadi, Timu ya Kusifu na kuabudu Bariadi, viongozi wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Usharika wa Tumaini Bariadi, baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School)  inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Waimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakiimba pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala, , mara baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.
Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Tumaini Bariadi Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, wakifuatilia masuala mbalimbali katika harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Awali na Msingi ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi

Waimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti kutoka KKKT Kijitonyama jijini Dar es Salaam wakiimba pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria, Dkt. Emmanuel Makala, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na Mchungaji wa KKKT Bariadi, Greyson Kinyaha, mara baada ya harambee ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika Shule ya Msingi na Awali ya Tumaini (Tumaini Pre & Primary School) inayomilikiwa na kanisa hilo, iliyofanyika Novemba 25, 2018 Mjini Bariadi.



Friday, November 23, 2018

WAFANYABIASHARA WA UTURUKI WAONESHA NIA YA KUWEKEZA KATIKA KIWANDA CHA NGUO SIMIYU

Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki wameonesha nia na dhamira ya kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza nguo mkoani Simiyu ambacho kitakuwa na uwezo wa kuajiri watu zaidi ya 4000.


Hayo yamebainishwa katika kikao kati ya Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo ambaye aliambatana na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Uturuki kutoka makampuni saba ya nchi hiyo, katika kikao maalum na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali na jumuiya ya wafanyabiashara ya mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Balozi Kiondo amesema Wafanyabiashara hao wanayo azma ya kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza nguo katika mnyororo mzima wa utengenezaji kutoka bidhaa ya awali ya pamba mpaka bidhaa ya mwisho kabisa, ambayo ni nguo kwa ubia(partineship) na Watanzania.

Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS amesema  mpaka sasa ni makampuni sita kutoka nchini humo yameonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha nguo mkoani Simiyu na akaahidi kwenda kuwashawishi wafanyabiashara wenzake hivyo watakaporudi kwa mara nyingine  makapuni mengi yatakuja kuwekeza katika viwanda vya nguo.

“Nikirudi nyumbani kama kiongozi wa wafanyabiashara nitawashawishi wengine pia waje wawekeze katika viwanda vya nguo,ombi langu kwenu ni kwamba ninahitaji Mfanyabiashara Mtanzania ambaye tutashirikiana naye katika uwekezaji huu(partinership), lakini niwahakikishie tu kuwa katika kiwanda tutakachojenga mashine na vifaa vyote vipo tayari kule Uturuki” alisema  Cengiz.

Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia wafanyabiashara hao upatikanaji wa soko la uhakika la nguo zitakazotengenezwa, pamoja na upatikanaji wa malighafi kwa kuwa Simiyu ndiyo mkoa unaozalisha zaidi ya asilimia 55 ya pamba yote nchini, ambapo kwa  mwaka 2018 Simiyu imezalisha takribani kilo milioni 131.

Ameongeza kuwa pamoja na uhakika wa soko na malighafi  Simiyu ina viwanda vingi  vya kuchambua pamba, ardhi itatolewa bure, miundombinu muhimu yote ipo, utashi wa kisiasa kwa viongozi wa wilaya upo, hivyo akawatoa hofu wawekezaji hao na kuwaeleza kuwa mkoa utashirikiana nao, huku akiomba waone uwezekano wa kuwekeza katika uongezaji thamani wa mazao ya mifugo kama ngozi na nyama

Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola amesema wako tayari kushirikiana na mwekezaji huyo, huku akibainisha kuwa kuanzishwa kwa kiwanda hicho kitawasaidia wanaochambua pamba na wakulima kupata faida ikilinganishwa na sasa ambapo zaidi ya asilimia 75 ya pamba inasafirishwa nje ya nchi.

Naye Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Mhe. Najlu Silanga ameahidi ushirikiano kwa wawekezaji aho kutoka Uturuki na kuiomba Wizara ya Viwanda, Baiashara na Uwekezaji kuzitambu na kusughuliakia changamoto mbalimbali za wafanyabiashara hapa nchini .

Wakati huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda  (TIRDO) Prof. Mkumbukwa Mtambo amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kuzingatia Utafiti na maendeleo katika Viwanda, huku akisisitiza kuwa ili viwanda vinavyoanzishwa viweze kuwa endelevu ipo haja ya kufanya utafiti na maendeleo na akaahidi kuwa Taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Simiyu katika tafiti mbalimbali  za  maendeleo ya viwanda.

MWISHO




Kutoka kulia Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede wakiteta jambo mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya viongozi na watendaji wa Serikali na ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.

Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, 

akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi  
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola akichangia hoja katika viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akizungumza viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo unaotarajiwa kufanywa na Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki katika mkoa wa Simiyu.




Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto)  akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo(wa pili kushoto), na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na  mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS( wa tatu kulia),  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede( wa pili kulia) na viongozi wa Serikali pamoja na wafanyabiashara wa mkoa huo, mara baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.

Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.

Bw. Gungu Silanga mmoja wa wafanyabiashara mkoani Simiyu, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akichangia hoja katika kikao cha  viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda(TIRDO), Prof. Mkumbukwa Mtambo, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Diwani wa Kata ya Zanzui Wilayani Maswa, Mhe. Jeremia Shigala akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo  (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Kutoka kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede, Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakionesha nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu, baada ya viongozi hao kukabidhiwa mwongozo huo Novemba 22, 2018.
Afisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Kija Kayenze akiwasilisha taarifa ya fursa za uwekezaji katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa taarifa ya mkoa wakati wa ugeni wa Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo aliyembatana na, Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki Bw. Cengiz ERTAS, Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
Bw. John Sabo mmoja wa wafanyabiashara mkoani Simiyu, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto)  akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo(wa pili kushoto), Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS (wa nne  kulia),  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede( wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo  (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji(kulia) na viongozi wengine wa Serikali wa mkoa huo, mara baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.




Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,  kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
Kushoto Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ( kulia) Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede wakiteta jambo, mara baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!