Wafanyabiashara
kutoka nchini Uturuki wameonesha nia na dhamira ya kuwekeza katika ujenzi wa
kiwanda cha kutengeneza nguo mkoani Simiyu ambacho kitakuwa na uwezo wa kuajiri
watu zaidi ya 4000.
Hayo
yamebainishwa katika kikao kati ya Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof.
Elizabeth Kiondo ambaye aliambatana na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na
mwakilishi wa Wafanyabiashara wa Uturuki kutoka makampuni saba ya nchi hiyo,
katika kikao maalum na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, Wakuu wa Taasisi mbalimbali
na jumuiya ya wafanyabiashara ya mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Novemba 22,
2018 Mjini Bariadi.
Balozi
Kiondo amesema Wafanyabiashara hao wanayo azma ya kuwekeza katika kiwanda cha
kutengeneza nguo katika mnyororo mzima wa utengenezaji kutoka bidhaa ya awali
ya pamba mpaka bidhaa ya mwisho kabisa, ambayo ni nguo kwa ubia(partineship) na
Watanzania.
Rais wa
Jumuiya ya Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS amesema mpaka sasa ni makampuni sita kutoka nchini
humo yameonesha nia ya kuwekeza katika kiwanda cha nguo mkoani Simiyu na
akaahidi kwenda kuwashawishi wafanyabiashara wenzake hivyo watakaporudi kwa
mara nyingine makapuni mengi yatakuja
kuwekeza katika viwanda vya nguo.
“Nikirudi
nyumbani kama kiongozi wa wafanyabiashara nitawashawishi wengine pia waje
wawekeze katika viwanda vya nguo,ombi langu kwenu ni kwamba ninahitaji
Mfanyabiashara Mtanzania ambaye tutashirikiana naye katika uwekezaji
huu(partinership), lakini niwahakikishie tu kuwa katika kiwanda tutakachojenga
mashine na vifaa vyote vipo tayari kule Uturuki” alisema Cengiz.
Mkuu wa
Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amewahakikishia wafanyabiashara hao upatikanaji wa
soko la uhakika la nguo zitakazotengenezwa, pamoja na upatikanaji wa malighafi
kwa kuwa Simiyu ndiyo mkoa unaozalisha zaidi ya asilimia 55 ya pamba yote nchini,
ambapo kwa mwaka 2018 Simiyu imezalisha
takribani kilo milioni 131.
Ameongeza
kuwa pamoja na uhakika wa soko na malighafi Simiyu ina viwanda vingi vya kuchambua pamba, ardhi itatolewa bure,
miundombinu muhimu yote ipo, utashi wa kisiasa kwa viongozi wa wilaya upo,
hivyo akawatoa hofu wawekezaji hao na kuwaeleza kuwa mkoa utashirikiana nao,
huku akiomba waone uwezekano wa kuwekeza katika uongezaji thamani wa mazao ya
mifugo kama ngozi na nyama
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola amesema
wako tayari kushirikiana na mwekezaji huyo, huku akibainisha kuwa kuanzishwa
kwa kiwanda hicho kitawasaidia wanaochambua pamba na wakulima kupata faida
ikilinganishwa na sasa ambapo zaidi ya asilimia 75 ya pamba inasafirishwa nje
ya nchi.
Naye
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu, Mhe. Najlu Silanga ameahidi ushirikiano
kwa wawekezaji aho kutoka Uturuki na kuiomba Wizara ya Viwanda, Baiashara na
Uwekezaji kuzitambu na kusughuliakia changamoto mbalimbali za wafanyabiashara
hapa nchini .
Wakati
huo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO) Prof. Mkumbukwa Mtambo amepongeza Mkoa wa Simiyu
kwa kuzingatia Utafiti na maendeleo katika Viwanda, huku akisisitiza kuwa ili viwanda
vinavyoanzishwa viweze kuwa endelevu ipo haja ya kufanya utafiti na maendeleo
na akaahidi kuwa Taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na Simiyu katika tafiti
mbalimbali za maendeleo ya viwanda.
MWISHO
Kutoka
kulia Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof.
Elizabeth Kiondo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Dkt. Edwin Mhede wakiteta jambo mara baada ya kumalizika kwa kikao kati ya
viongozi na watendaji wa Serikali na ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki,
kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa
Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania
nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa
Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini
Bariadi.
Mwenyekiti
na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS,
akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya
viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof.
Elizabeth Kiondo katika kikao kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mbunge wa
Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia hoja katika viongozi wa Mkoa wa Simiyu,
baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki
Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Mwenyekiti na mwakilishi wa Wafanyabiashara
kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika
Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda
vya nguo mkoani humo.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha kuchambua Pamba cha Alliance Ginnery, Bw. Boaz Ogola akichangia
hoja katika viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za
Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akizungumza viongozi wa
Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali katika kikao kilichofanyika
Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda
vya nguo unaotarajiwa kufanywa na Wafanyabiashara kutoka nchini Uturuki katika
mkoa wa Simiyu.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo(wa pili kushoto), na Rais
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki,
Bw. Cengiz ERTAS( wa tatu kulia), Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede( wa pili
kulia) na viongozi wa Serikali pamoja na wafanyabiashara wa mkoa huo, mara
baada ya kuhitimisha kikao mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika
viwanda vya nguo.
Mkuu
wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akichangia hoja katika kikao cha viongozi
wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa
Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa
Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Bw.
Gungu Silanga mmoja wa wafanyabiashara mkoani Simiyu, akichangia hoja katika kikao
cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi
wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth
Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa Wafanyabiashara
kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika
Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda
vya nguo mkoani humo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda(TIRDO), Prof. Mkumbukwa
Mtambo, akichangia hoja katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya
viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof.
Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa
Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Diwani
wa Kata ya Zanzui Wilayani Maswa, Mhe. Jeremia Shigala akichangia hoja katika
kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za
Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa
Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania
nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini
Bariadi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo
(SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji, akichangia hoja katika kikao cha
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Kutoka
kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin
Mhede, Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof.
Elizabeth Kiondo na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini wakionesha
nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Simiyu, baada ya viongozi hao
kukabidhiwa mwongozo huo Novemba 22, 2018.
Afisa
Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Bibi. Kija Kayenze akiwasilisha
taarifa ya fursa za uwekezaji katika kikao cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu,
baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki
Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara na mwakilishi wa
Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS kilichofanyika Novemba 22,
2018 Mjini Bariadi kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo
mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa taarifa ya mkoa wakati wa ugeni wa
Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo aliyembatana na, Rais
wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki Bw. Cengiz ERTAS, Novemba 22, 2018
Mjini Bariadi.
Bw.
John Sabo mmoja wa wafanyabiashara mkoani Simiyu, akichangia hoja katika kikao
cha viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo(wa pili kushoto), Rais wa
Jumuiya ya Wafanyabiashara
na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS (wa nne kulia),
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Edwin
Mhede( wa tatu kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia Viwanda
Vidogo (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji(kulia)
na viongozi wengine wa Serikali wa mkoa huo, mara baada ya kuhitimisha kikao
mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.
Mkuu
wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia hoja katika kikao cha
viongozi wa Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini Bariadi
kwa lengo la kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika kikao cha viongozi wa
Mkoa wa Simiyu, baadhi ya viongozi wa Taasisi za Serikali, Balozi wa Tanzania
nchini Uturuki Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo na Rais wa Jumuiya ya
Wafanyabiashara na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS, kilichofanyika Novemba 22, 2018 Mjini
Bariadi.
Kushoto
Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
na
mwakilishi wa Wafanyabiashara kutoka Uturuki, Bw. Cengiz ERTAS na Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka, ( kulia) Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Mhe.
Prof. Elizabeth Kiondo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Dkt. Edwin Mhede wakiteta jambo, mara baada ya kuhitimisha kikao
mjini Bariadi kilichofanyika kujadili uwekezaji katika viwanda vya nguo.
0 comments:
Post a Comment