Wednesday, February 26, 2020

KIWANDA CHA VIFAA TIBA SIMIYU KUIPUNGUZIA MSD UAGIZAJI WA VIFAA TIBA NJE YA NCHI


Kukamilika kwa kiwanda cha vifaa tiba vitokanavyo na zao la pamba kinachotarajiwa kujengwa Bariadi mkoani Simiyu kutaipunguzia Bohari ya dawa (MSD) uagizaji wa bidhaa hizo toka nje ya nchi kwa asilimia 38.3.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Mhe. Angella Kairuki kwenye mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi, kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali za biashara na uwekezaji na ufumbuzi wake.

“MSD imekuwa ikitumia zaidi ya shilingi bilioni 147 kununua dawa na vifaa tiba zaidi ya 19 kutoka nje ya nchi, tunaamini kwa kuanzisha kiwanda cha vifaa tiba vitokanavyo na pamba  na bidhaa zingine 19 zikiwemo nguo za madaktari na wauguzi tunaamini tutaiondolea MSD uagizaji wa bidha hizo kwa asilimia 38.3,”alisema Mhe. Kairuki.

Amesema kiwanda hicho kitasaidia kufikia azma ya Serikali ya kuongezea thamani zao la pamba badala ya kuisafirisha, ambapo kwa sasa zaidi ya asilimia 70 ya pamba inasafirishwa nje ya nchi.

Aidha, Mhe Kairuki ametoa wito kwa wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu kutumia fursa za uwekezaji zilizopo katika viwanda vya ngozi, nyama,vyakula vya mifugo, viwanda vya mafuta ya kula; huku akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kujenga mazingira wezeshi kwa biashara na uwekezaji, kupunguza kero ya utitiri wa kodi na tozo mbalimbali, kupunguza mamlaka za udhibiti wa kibiashara na kuondoa muingiliano wa mamlaka hizo.

Katika hatua nyingine Mhe. Kairuki ameupongeza uongozi wa mkoa wa Simiyu kwa Simiyu kuwa mkoa wa kwanza kuzindua mwongozo wa uwekezaji nchini mwaka 2017 pamoja na kutekeleza mkakati wa Wilaya Moja Bidhaa Moja(One District One Product -ODOP).

Kwa upande wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji amesema  zabuni ya kiwanda cha vifaa tiba vitokanavyo na pamba  kinachotarajiwa kujengwa Mkoani Simiyu imeshatangazwa na jiwe la msingi linatarajiwa kuwekwa mwezi Mei, 2020.

Naye mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema Bodi ya Pamba itoe viuadudu kwa wakulima wa pamba kwa wakati ili kudhibiti madhara yanayoweza kusababishwa na magonjwa huku akisisitiza bei ya pamba kupangwa mapema kabla ya msimu.

Aidha, Mtaka ameomba Waziri anayeshughulikia Uwekezaji kuona namna ya kuwasaidia wafanyabiashara na wawekezaji katika changamoto ya kufungiwa biashara zao, ambapo baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakifungiwa biashara na viongozi au watendaji kutoka katika Taasisi au Ofisi mbalimbali za Serikali.

Naye Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara mkoa wa Simiyu, Bw. Zebedayo King ameomba mabaraza ya biashara yafanyike  kwa wakati  ili wafanyabiashara waendelee kupata fursa ya kukutana na viongozi wa Serikali na Taasisi za Fedha na kujadili namna ya kutatua changamoto mbalimbali katika biashara na uwekezaji ikiwemo masuala ya kodi, kulipwa madeni yao kwa wakati pamoja na mazingira ya uwekezaji na biashara kwa ujumla.

Awali akiwasilisha changamoto zinazowakabili wakulima wa pamba Mwenyekiti wa chama cha Ushirika Mkoa wa Simiyu(SIMCU) Charles Madata amesema baadhi ya wakulima hawajalipwa fedha zao na dawa hazitolewi kwa wakati, hivyo akaomba wakulima wasaidiwe kutatua changamoto hizo ili waone faida ya kilimo cha zao hilo.

Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliwahusisha viongozi wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu uwekezaji, Mhe. Angella Kairuki, Manaibu Waziri kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Ardhi na Makazi, Wizara ya Maliasili na Utalii, Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira, Wizara ya Madini, Wizara ya ujenzi, Viongozi wa Mkoa, Viongozi wa Jumuiya za Wafanyabiashara, wakulima na Wajasiriamali
MWISHO.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angella Kairuki akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi.


 Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu wakifuatilia hoja na maelezo kutoka kwa Viongozi wa Serikali wakati wa Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi.


 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara mkoa wa Simiyu, Bw. John Sabo akichangia hoja katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi.


 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi.


 Meneja Masoko wa Busega Mazao Company Ltd, Bw. Innocent Mafuru akichangia hoja katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi.


 NaibuWaziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji akitoa ufafanuzi wa changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi.


 NaibuWaziri wa Viwanda na biashara, Eng. Stella Manyanya  akitoa ufafanuzi wa changamoto mbalimbali zilizowasilishwa na wawekezaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi.


Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Mkoa wa Simiyu, Bw. Charles Madata akiwasilisha changamoto za wakulima wa pamba katika Mkutano wa mashauriano kati ya Serikali, Wawekezaji na Wafanyabiashara mkoani Simiyu uliofanyika Februari 25, 2020 Mjini Bariadi.


Tuesday, February 18, 2020

ASKARI WAASWA KUEPUKA VITENDO VINAVYOLITIA DOSARI JESHI LA POLISI


Askari mkoani Simiyu wameaswa kulinda hadhi ya jeshi la polisi kwa kujiepusha na vitendo viovu vinavyolitia dosari jeshi hilo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na askari wa mkoa huo Februari 17, 2020 ambapo amevitaja vitendo hivyo kuwa ni pamoja na kutoa siri za jeshi, kuomba rushwa, utapeli na kushiriki kuharibu ushahidi katika baadhi ya kesi.

“Ni jambo la aibu kwa askari kushiriki katika uhalifu,  kutoa siri za jeshi na kugeuka kuwa mtoa taarifa kwa wahalifu, ipendeni kazi yenu muepuke mambo yanayodhalilisha jeshi na mjenge tabia ya kuonyana ili mlinde heshima ya jeshi letu,” alisema Mtaka.

Aidha, Mtaka ametoa wito kwa askari mkoani Simiyu kujiendeleza kielimu ili waweze kupata sifa za kulitumikia jeshi katika nafasi mbalimbali huku akiwaeleza umuhimu wa kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo Mkoani humo kwa lengo la kutengeneza kipato cha zaida.

Katika hatua nyingine  Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Jeshi la Polisi kutenda haki kwa askari walio chini yao ikiwemo kutoa nafasi ya kuwapandisha vyeo askari wanaostahili  kwa wakati uliopo ili kuwapa motisha katika kazi yao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe amesema kuwa katika Awamu hii ya tano hakuna kisingizio kwa askari kushindwa kufanya kazi zao kwa kutofuata taratibu.

“Ilikuwa siyo rahisi sana kumkamata tajiri , lakini sasa hivi Watanzania wote tuko hali moja hakuna cha huyu ni nani na yule ni nani; sasa hivi mtu akifanya hivyo ni mapungufu yake binafsi tunafanya kazi kwa kufuata taratibu za jeshi pasipo kuingiliwa na mtu yeyote, sisi tuliokaa muda mrefu kwenye jeshi la Polisi tunajua kazi nzuri inayofanywa na Mhe. Rais,” alisema Mwaibambe.

Mwaibambe ameongeza kuwa askari kama watumishi wa umma wengine wanapaswa kujiepusha na masuala yanayoleta malalamiko kwa wananchi huku akisisitiza kuwa hawatasita kuwachukulia hatua askari watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu.

Kwa upande wao askari wamesema watafanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu huku wakiomba Serikali ya Mkoa iweze kuwasaidia upatikanaji wa viwanja kwa ajili ya kujenga makazi yao binafsi na maeneo ya kuweka uwekezaji wao.
MWISHO

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo katika kikao kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya askari Polisi mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka katika kikao kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) azungumze na askari wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa katika kikao kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
 Askari wa Jeshi la Polisi, Koplo Abdallah Manzi akichangia hoja katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na askari hao, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) akiteta jambo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe na  Mkuu wa Upepelezi Mkoa wa Simiyu, SSP Israel Makongo, mara baada ya kumalizika kwa kikao chake na askari polisi, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
 Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na askari wa Jeshi la Polisi mkoani Simiyu,  kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya maafisa na askari wa jeshi la polisi mkoani humo, mara baada ya kumalizika kwa kikao chake na askari polisi, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu wakiimba wimbo wa uadilifu kabla ya kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya maafisa na askari wa jeshi la polisi mkoani humo, mara baada ya kumalizika kwa kikao chake na askari polisi, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Askari polisi H.864 DIC Yassin akichangia hoja katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na askari hao, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe(kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) na Mkuu wa Upepelezi Mkoa wa Simiyu, SSP Israel Makongo, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mkuu wa Mkoa  na askari polisi, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa huo, mara baada ya kikao cha Mkuu wa Mkoa na askari polisi, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kikao cha Mkuu wa Mkoa na askari polisi, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) katika picha ya pamoja  na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe(kushoto) na  Mkuu wa Upepelezi Mkoa wa Simiyu, SSP Israel Makongo, mara baada ya kumalizika kwa kikao chake na askari polisi, kilichofanyika  Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.

Friday, February 14, 2020

WAZABUNI WATAJWA KUCHANGIA UCHELEWESHAJI WA MIRADI

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge  amesema kuwa baadhi ya wazabuni wanaouza vifaa vya ujenzi wamekuwa wakiuza vifaa kwa bei ya juu na kuchelewesha vifaa hivyo pale vinapohitajika, jambo linalopelekea baadhi ya miradi inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi hilo (SUMA JKT) kutokamilika kwa wakati.

Brigedia Jenerali Mbuge ameyasema hayo Februari 13, 2020 mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT mkoani Simiyu.

Ameongeza kuwa katika kukabiliana na changamoto hiyo, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limejipanga kuanzisha maduka ya vifaa vya Ujenzi vitakavyouzwa kwa bei ya  jumla ili kuwezesha upatikanaji wa vifaa kwa urahisi, haraka na kwa bei nafuu ikilinganishwa na wazabuni wengine.

“Tatizo moja ninaloliona kwenye utekelezaji wa miradi ni vifaa kuuzwa kwa bei ya juu sana na kucheleweshwa, tumeamua kuwa  na maduka ya vifaa ya jumla; tutatoa maelekezo kwa wakuu wa kanda za ujenzi watatupatia mahitaji yao, ili kuwawezesha kufanya kazi kwa wakati kama tunavyokubaliana na washitiri wetu,” alisema Brigedia Jenerali Mbuge.

Katika hatua nyingine Brigedia Jenerali Mbuge amesema jeshi hilo litaendelea kuwatumia vijana watakaomaliza mafunzo ya JKT katika shughuli zilizopo kwenye miradi inayotekelezwa na Jeshi hilo lengo likiwa kuwawezesha vijana hao kupata kipato na baadaye waweze kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa pekee.

Vile vile ameahidi kuongeza nguvu kazi ya vijana katika mradi inayotekelezwa na SUMA JKT mkoani Simiyu kuongeza kasi na miradi hiyo iweze kukamilika kwa muda uliopangwa, huku akitoa wito kwa Taasisi mbalimbali kuipa kazi SUMA JKT,  ili iendelee kuwa kutoa gawio kubwa kwa Serikali, ambapo amesema mwaka 2018/2019 ilitoa zaidi ya shilingi bilioni moja na mwaka 2019/2020 linatarajia kupanda zaidi kutokana na uwepo wa vyanzo vya kutosha.

Awali akitoa taarifa, Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya miundombinu katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhandisi Mashaka Luhamba  amesema JKT wanatekeleza miradi minne mkoani Simiyu ukiwemo wa ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,  wodi ya wazazi Hospitali ya Rufaa ya mkoa, ujenzi  jengo la wizara ya kilimo linalojengwa kwenye viwanja vya maonesho ya Nane nane pamoja na  kiwanda cha Chaki Maswa ( Maswa chalk) .

Aidha mhandisi huyo amebainisha kuwa ujenzi wa jengo la Mkuu wa Mkoa unatekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 kwa gharama ya shilingi bilioni 5.7  ambapo ujenzi rasmi ulianza mwezi Mei, 2019 na endapo fedha zitapatikana kwa wakati unatarajiwa kukamilika Novemba,  2020.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema ni vema SUMA JKT ikahuisha uharaka wa kutekeleza miradi kama jamii inavyoutarajia kwa kuwa jamii na Serikali imejenga imani kubwa kwa JKT kutekeleza miradi kwa wakati ikilinganishwa na wakandarasi wengine.

Mtaka ameongeza kuwa miradi inayotekelezwa na SUMA JKT iwe fursa kwa vijana waliopata mafunzo ya JKT na kumaliza mikataba yao ili waweze kupata kipato kitakachowasaidia kwenda kujitegemea na kujiajiri endapo hawataajiriwa.
MWISHO

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji wa Jeshi  mara baada ya kukagua mradi wa Ujenzi wa wodi ya wazazi  unaendela katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, wakati wa ziara yake Mkoani humo Februari 13, 2020  yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji mali la JKT(SUMA JKT).Meneja wa  SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni Fabian Buberwa akiwaongoza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kushoto) na  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini  Brigedia Jenerali Charles Mbuge(wa nne kushoto) kuelekea katika eneo la ujenzi wa wodi ya wazazi  katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, wakati wa ziara Mkuu huyo wa JKT Mkoani humo Februari 13, 2020  yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT.
 Katibu Tawala Msaidizi seksheni ya Miundombinu katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Mashaka Luhamba akitoa maelezo ya hali ya utekelezaji wa miradi ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT Mkoani Simiyu kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini Brigedia Jenerali Charles Mbuge , wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa JKT Mkoani humo Februari 13, 2020  yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT.

 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kushoto) akizungumza jambo katika ziara ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT) Brigedia Jenerali Charles Mbuge Mkoani humo Februari 13, 2020  yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT.


Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT)  Brigedia Jenerali Charles Mbuge(kulia) akimkabidhi kalenda Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akiwa katika zaira ya kikazi  mkoani humo Februari 13, 2020 yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbuge(kulia) akimkabidhi kalenda Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akiwa katika zaira ya kikazi  mkoani humo Februari 13, 2020 yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT, (kushoto) Katibu Tawala Msaidizi seksheni ya Miundombinu katika Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Mashaka Luhamba, (wa pili kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ekwabi Mujungu

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbuge(wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka (wa nne kushoto), wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na baadhi ya Maafisa wa jeshi hilo waliofuatana naye katika ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT Mkoani Simiyu Februari 13, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbuge wakitoka katika Jengo la Wizara ya kilimo linalojengwa katika Uwanja wa Nanenane Nyakabindi Mjini Bariadi, wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa JKT ya kukagua miradi ya ujnezi inayotekelezwa na SUMA JKT Mkoani humo, iliyofanyika Februari 13, 2020.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kulia) akisalimiana na  Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbuge mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT Mkoani humo, iliyofanyika Februari 13, 2020.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbuge(wa nne kulia) akizungumza na wasimamizi wa miradi ya ujenzi  wa majengo ya Serikali inayotekelezwa  na SUMA JKT Mkoani Simiyu wakati wa ziara yake Februari 13, 2020 mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi hiyo.
 Meneja wa  SUMA JKT Kanda ya Ziwa Kapteni Fabian Buberwa(kulia) akitoa maelezo ya hali ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Kilimo katika Uwanja wa Nanenane Mjini Bariadi mkoani Simiyu kwa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini(JKT), Brigedia Jenerali Charles Mbuge(wa pili kushoto), wakati wa ziara yake Februari 13, 2020 ya kukagua miradi inayotekelezwa na SUMA JKT Mkoani Simiyu


Baadhi ya mafundi wakiendelea na kazi katika mradi wa ujenzi wa jengola wodi ya wazazi katika Hospitali ya  Rufaa ya mkoa wa Simiyu, mradi ambao unatekelezwa na SUMA JKT.
 Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (kulia) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Brigedia Jenerali Charles  Mbuge  alipompokea  mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi kwa lengo la kufanya ziara ya kukagua miradi ya ujenzi inayotekelezwa na SUMA JKT Mkoani humo, iliyofanyika Februari 13, 2020. 

 Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini(JKT),  Brigedia Jenerali Charles Mbuge(kulia) akizungumza na baadhi ya viongozi na watendaji  wa Mkoa wa Simiyu (baadhi hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika wakati wa ziara yake Februari 13, 2020 mkoani humo yenye lengo la kukagua miradi inayotekelezwa na SUMA JKT Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT),  Brigedia Jenerali Charles Mbuge akizungumza na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu na watendaji wa Jeshi  mara baada ya kukagua mradi wa Ujenzi wa Jengo la wodi ya wazazi  unaoendela katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi, wakati wa ziara yake Mkoani humo Februari 13, 2020  yenye lengo la kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayotekelezwa na Shirika la Uzalishaji mali la JKT(SUMA JKT).

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!