Askari mkoani Simiyu wameaswa
kulinda hadhi ya jeshi la polisi kwa kujiepusha na vitendo viovu vinavyolitia
dosari jeshi hilo.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa
wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati akizungumza na askari wa mkoa huo Februari
17, 2020 ambapo amevitaja vitendo hivyo kuwa ni pamoja na kutoa siri za jeshi,
kuomba rushwa, utapeli na kushiriki kuharibu ushahidi katika baadhi ya kesi.
“Ni jambo la aibu kwa askari kushiriki
katika uhalifu, kutoa siri za jeshi na
kugeuka kuwa mtoa taarifa kwa wahalifu, ipendeni kazi yenu muepuke mambo
yanayodhalilisha jeshi na mjenge tabia ya kuonyana ili mlinde heshima ya jeshi
letu,” alisema Mtaka.
Aidha, Mtaka ametoa wito kwa askari
mkoani Simiyu kujiendeleza kielimu ili waweze kupata sifa za kulitumikia jeshi
katika nafasi mbalimbali huku akiwaeleza umuhimu wa kuchangamkia fursa za
kiuchumi zilizopo Mkoani humo kwa lengo la kutengeneza kipato cha zaida.
Katika hatua nyingine Mtaka ametoa wito kwa viongozi wa Jeshi la
Polisi kutenda haki kwa askari walio chini yao ikiwemo kutoa nafasi ya
kuwapandisha vyeo askari wanaostahili
kwa wakati uliopo ili kuwapa motisha katika kazi yao.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi wa
Mkoa
wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe amesema kuwa katika Awamu hii ya tano hakuna
kisingizio kwa askari kushindwa kufanya kazi zao kwa kutofuata taratibu.
“Ilikuwa
siyo rahisi sana kumkamata tajiri , lakini sasa hivi Watanzania wote tuko hali
moja hakuna cha huyu ni nani na yule ni nani; sasa hivi mtu akifanya hivyo ni
mapungufu yake binafsi tunafanya kazi kwa kufuata taratibu za jeshi pasipo
kuingiliwa na mtu yeyote, sisi tuliokaa muda mrefu kwenye jeshi la Polisi
tunajua kazi nzuri inayofanywa na Mhe. Rais,” alisema Mwaibambe.
Mwaibambe
ameongeza kuwa askari kama watumishi wa umma wengine wanapaswa kujiepusha na
masuala yanayoleta malalamiko kwa wananchi huku akisisitiza kuwa hawatasita
kuwachukulia hatua askari watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu.
Kwa
upande wao askari wamesema watafanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu huku
wakiomba Serikali ya Mkoa iweze kuwasaidia upatikanaji wa viwanja kwa ajili ya
kujenga makazi yao binafsi na maeneo ya kuweka uwekezaji wao.
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo katika kikao kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya askari Polisi mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka katika kikao kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (wa pili kulia) azungumze na askari wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa katika kikao kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Askari wa Jeshi la Polisi, Koplo Abdallah Manzi akichangia hoja katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na askari hao, kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakifuatilia kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na askari wa Jeshi la Polisi mkoani Simiyu, kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Baadhi ya askari wa
jeshi la polisi mkoa wa Simiyu wakiimba wimbo wa uadilifu kabla ya kikao chao
na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani), kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya
maafisa na askari wa jeshi la polisi mkoani humo, mara baada ya kumalizika kwa
kikao chake na askari polisi, kilichofanyika
Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Askari polisi H.864 DIC
Yassin akichangia hoja katika kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka na askari hao, kilichofanyika Februari
17, 2020 Mjini Bariadi.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Simiyu, SACP Henry Mwaibambe(kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati) na Mkuu wa Upepelezi Mkoa wa Simiyu, SSP
Israel Makongo, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mkuu wa Mkoa na askari polisi, kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(wa tatu kushoto walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na
baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu na Wajumbe wa
Kamati ya Ulinzi naUsalama ya Mkoa huo, mara baada ya kikao cha Mkuu wa Mkoa na
askari polisi, kilichofanyika Februari 17,
2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kikao
cha Mkuu wa Mkoa na askari polisi, kilichofanyika Februari 17, 2020 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati) katika picha ya pamoja na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, SACP
Henry Mwaibambe(kushoto) na Mkuu wa
Upepelezi Mkoa wa Simiyu, SSP Israel Makongo, mara baada ya kumalizika kwa
kikao chake na
askari polisi, kilichofanyika Februari 17,
2020 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment