Blog rasmi ya Mkoa wa Simiyu

Wednesday, July 14, 2021

MKUU WA MKOA AELEKEZA WATENDAJI KUPIMWA KWA MIKATABA AIDHA CHMT ITAKAYOSHINDWA KUSIMAMIA AFYA KUVUNJWA

Ku


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akizungumza na Wadau wa Sekta ya afya 


 

Katibu Tawala Bi. Prisca Kayombo akiwatambulisha Viongozi Mbalimbali waliofuatana na mkuu wa mkoa 

                                        


                                        Wadau wa sekta ya afya wakijiandaa na kikao kazi
Wadau wakisikiliza mada wakati wa Kikao kazi

Kufuatia taarifa ya tathimini kuonesha usimamizi duni sekta ya Afya, RC Kafulila amelekeza kuandaliwa mikataba ya usimamizi kati ya RMO na DMOs,  RAS na DEDs na yeye mwenyewe RCs a DCs ili kuhakikisha wilaya na halmashauri zinasimamia sekta ya afya kikamilifu.  

Maelekezo hayo ameyatoa kufuatia tathimini ya usimamizi wa sekta ya afya kuonyesha kuwa kwa muda mrefu usimamizi wa Kamati za Afya Wilaya ( CHMT) ni dhaifu,  wakurugenzi na wakuu wa wilaya hawajawa na msukumo wa kutosha kuhakikisha usimamizi.

Aidha Mhe. Kafulila ameagiza KUVUNJWA kwa Kamati za usimamizi wa huduma ya Afya (CHMT)  itakayoshindwa kusimamia sekta ya afya katika halmashauri husika.  Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo kufuatia taarifa ya tathimini ya robo mwaka kuonyesha kuwa CHMT zote mkoani Simiyu kwa kipindi kirefu  zimekuwa na usimamizi dhaifu hata kusababisha vifo kizembe. 

Katika tathimini hiyo  Bariadi DC ilipata alama C, Busega D, Bariadi mji C, Meatu E , Maswa F huku Itilima ikipata F. Mhe.Kafulila ameelekeza kuwa katika taarifa ya oOktoba, halmashauri itakayopata chini ya alama B, basi CHMT husika itavunjwa na  wengine kuchukuliwa hatua za kiutumishi.

Mwisho

TANZANIA INAJENGA SGR KWA GHARAMA NAFUU- KAFULILA.

 


 Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akiwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo wakati wa kikao na Waandishi wa habari.


 
Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simyu wakiwa katia mkutano na waandishi wa Habari.

Kuanzia kulia Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi.Prisca Kayombo, Mkuu wa Mkoa Mhe. David Kafulila na Meneja Mradi  Ujenzi wa reli ya kisasa Mwanza- Isaka Eng. Machibya Masanja wakiwa katika kikao na waandishi wa habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu.


Hayo ameleza jana RC KAFULILA wakati akifungua kampeni ya kuhamasisha uelewa wa wananchi kuhusu mradi wa SGR kipande cha Mwanza - Isaka( 341km), kitakachojengwa kwa gharama ya Tsh.3trn sawa na $1.3bn. 


Mhe.Kafulila amempongeza Rais kwa kuendeleza ujenzi huo kwa kasi zaidi na kusema kuwa gharama hii ni nafuu kulinganisha na Kenya na hata Ethiopia na hivyo inathibitisha usimamizi madhubuti wa fedha za Serikali.

 " Hii inazidi kuthibitisha ripoti ya jukwaa la kimataifa kuhusu uchumi- World Economic Forum 2019 kuonesha kwamba Tanzania ni nchi ya 29 katika nchi 186 duniani katika usimamizi thabiti wa matumizi ya fedha za umma".

 Mhe.Kafulila amesisitiza wananchi kujitokeza kwenye kampeni hiyo iliyoanza jana na itakamalizika  alhamisi ili kupata uelewa zaidi wa mradi. Amewahakikishia fidia kulipwa kwa mujibu wa sheria na zaidi kuwaomba wachangamkie fursa za biashara wakati wa ujenzi hususan eneo la Malampaka ambapo kambi kubwa ya ujenzi zinajengwa. Amesisitiza Shirika la reli kutoa upendeleo kwa wafanyabiashara wa mkoa wa Simiyu kwa kazi ambazo zipo ndani ya uwezo.

Mwisho

Monday, June 14, 2021

KATIBU TAWALA MKOA WA SIMIYU BI. PRISCA KAYOMBO AFUNGUA MICHEZO YA UMISSETA MKOA


Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo, tarehe 11/06/2021 alifungua rasmi,michezo ya UMISSETA Mkoa, michezo ambayo ilikuwa ikifanyika katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa.

Akizungumza Kaimu Afisa Elimu Mkoa Bwn.Charles Maganga alisema mashindano ngazi ya Mkoa yameanza leo 11/6/21 na yatakamilika 13/6/21 kwa kuunda timu ya Mkoa. Kauli mbiu ya Mashindano haya ya mwaka 2021 ni : “Michezo,Sanaa na  Taaluma Kwa Maendeleo ya Uchumi wa Viwanda”.

Mashindano haya yana jumla ya washiriki 679, kati yao wanafunzi 600,waalimu 61, madaktari 2 na viongozi 16.Washiriki hawa ni kutoka Halmashauri zote za Mkoa.Idadi ya Michezo inayoshindaniwa ni saba na michezo 4 kati ya hiyo inahusisha wavulana na wasichana.
Michezo hiyo ni pamoja na Riadha, Mpira wa Miguu, Mpira wa Wavu, Mpira wa Mikono,Mpira wa kikapu, Mpira wa Netiboli na fani za ngoma na kwaya.

Ili kuendesha mashindano kwa ufanisi tumeunda kamati ya ndhamu, afya, usafi na mazingira. Pia tumeunda kamati za michezo.Kamati hizi zina jukumu la kusimamia uendeshaji wa michezo kwa kuzingatia sheria na kanuni za michezo husika.Na wajumbe wa kamati hizi ni waalimu wa michezo husika.Hali ya kambi ni nzuri, hatujakumbanana changamoto
yeyote, wanamichezo wana ari kubwa ya kishindana katika hali ya utulivu, upendo

Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa Dkt. Fredrick Sagamiko, alimkaribisha Mgeni rasmi Bi. Kayombo na kumhakikishia kuwa hali ya Maswa ni shwari hivyo wanamichezo wasiwe na wasiwasi kabisa.

Katibu Tawala, Bi. Kayombo  ambaye  alikuwa mgeni rasmi alikuwa na haya ya kusema;
napenda kuwashukuru  Wazazi/ walezi kwa kuwaruhusu wanafunzi kushiriki michezo.Pia niwashukuru wadau mbalimbali kwa kuwezesha maandalizi mazuri.Niwapongeze wanamichezo  wote kwa kuunda timu za halmashauri, ni matumaini yangu kuwa vipaji mlivyo vionyesha vitaendelea kuonekana katika mashindano haya yatakayofanyika katika ngazi ya Taifa, Mkoani Mtwara kuanzia 20/6/2021 - 03/7/2021.

Kama ilivyo  kauli mbiu ya mwaka. huu Michezo na Sanaa ni sehemu ya Taaluma na maendeleo ya Elimu. Michezo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu na imekuwa chimbuko kubwa la kuzalisha na kukuza wanamichezo mbalimbali  wanaounda timu za Taifa. Lengo la michezo hii ni kujenga na kuimarisha umoja, udugu, upendo, mshikamano, hali ya kujiamini, kukuza taaluma na utimamu wa akili kwa wanafunzi.

Tafiti mbalimbali  zimebainisha kuwa michezo huchangia katika kuimarisha ushiriki wa wanafunzi kitaaluma kwa kupunguza utoro na kuimarisha afya za wanafunzi.Michezo imesaidia kujenga mshikamano kimkoa kwa kuwaleta pamoja wadau wa elimu na michezo.

Nitoe  wito kwa wanafunzi wote watakaochaguliwa kuunda timu ya Mkoa, mzingatie kanuni za michezo,  tumieni vipaji vyenu kuhakikisha kuwa  tunapata ushindi. Tumieni fursa hiyo kuutangaza mkoa wa simiyu.Waalimu  chagueni wanafunzi na sio mamluki kwani itakuwa aibu kwa mkoa.Ikiwa mtawela Mamluki.

Changamoto ya viwanja vya michezo, natoa maelekezo maafisa michezo, kuendelea  kupima viwanja vyote vinavyohitajika kwenye maeneo ya shule ili wakuu wa shule waweze kusimamia utengenezaji  wa viwanda hivyo kwa kushirikiana na wanafunzi na vitumike  wakati wote,tusisubiri tu kipindi cha michezo hii ya UMISSETA.

 Ili kufanya vizuri zaidi katika Sekta ya Michezo na Elimu kwa ujumla ni vyema tukazingatia yafuatayo: imarisheni nidhamu yenu katika nyanja zote,nidhamu na maadili ya waalimu na wanafunzi viendelee kudumishwa,Wanafunzi/ wanamichezo sikilizeni na kuzingatia maelekezo, mbinu na mikakati mbalimbali mtakayopewa na waalimu wenu.Watoto waende salama na kurudi salama, nidhamu na maadili vidumishwe, mahusiano kati ya waalimu na watoto, yawe ya mzazi na mtoto.Nami nawatuma mkaniletee ushindi.

Michezo sio uadui hivyo watakaoteuliwa na wasioteuliwa wasilete uadui. Maendeleo yetu hutokana na kuweka  bidii katika michezo.

Akitoa neno la shukrani Bi.Line Chanafi, alisema mgeni rasmi kwa niaba ya wenzangu nikuahidi ushirikiano. Sisi tupo vizuri na tumeanza  vizuri na hatuna mamluki, tuna wanafunzi/ wanamichezo halali, tutafanya yote uliyotuagiza na hasa nidhamu.

MWISHOWAVUVI, SIRI YA MAFANIKIO NI KUFANYA KAZI KWA VIKUNDI

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila wakati wa Ziara yake Wilayani Busega, ambapo alipata fursa ya kuzungumza na Wavuvi wa Nyashimo.

Akifungua  Kikao hicho  Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe.Tano Mwera aliwafahamisha wakazi wa Nyashimo kuwa ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa Mpya wa Simiyu, imelenga kusikiliza kero zao na hatimae kupata ufumbuzi wa kero hizo.

Mhe.Tano aliwataka wawakilishi wa wavuvi hao kuwasilisha kero wanazokabiliana nazo katika shughuli za uvuvi, nao walikuwa na haya ya kusema;

Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyamikoma- Bw.Kurwa Bula; Changamoto, kubwa ni upumzikaji wa siku 10 hii ni changamoto kwani sisi tukipumzisha ziwa watu kutoka maeneo mengine wanakuja kuvua kwetu kwani wao huwa hawapumzishi Ziwa, ni bora,basi hiyo sheria iwekwe kwa mikoa yote mitatu.Kama kufungwa kufungwe Wilaya zote za mikoa jirani.

Akizungumza Diwani wa Kata ya Kabita- Silas Soshola, alisema changamoto kubwa tunazokabilina nazo ni pamoja na Sheria za uvuvi, nyingi ya sheria hizo ni za zamani na si rafiki, sasa hivi tunalipa Tsh. 400,000/- na bado kuna kodi nyingi Sana,Wavuvi wetu tuna Walipia leseni, tunaomba hiyo leseni ifutwe kwani mbona wakulima hawalipi leseni hizo,tunahitaji Masoko, tunaomba tupate masoko angalau mawili. Tuna Shule moja tu ya Sekondari, ambayo ina Wanafunzi 1250 na waalimu 2 wa somo la Biology, Waalimu 2 somo la Kiswahili ,waalimu 2-basic math, hatuna mwalimu wa fizikia. Wengi wa Waalimu wanaokuja hawakai. Wakazi wa Nyashimo walioamua kujenga Shule ya SekondariVenance Mabesho, ambapo tupo katika hatua za mwisho,tunaomba tupate angalau Mifuko 200 ya sementi kwani itasaidia sana katika ujenzi wa Uzio ili watoto wetu wasiliwe na wanyama. Tunaomba tuwekewe alama ya Pundamilia kwani Barabara yetu inakaosa alama hiyo na kwa kipindi cha kwa miaka watu wengi wamepoteza maisha.

Naye Mwenyekiti wa Kijiji-Paulo Makongoro, alisema moja ya changamoto kubwa inayowakabili wakazi wa Nyashimo ni Changamoto ya viboko ambao wana angamiza watu. Mkazi mwingine wa Nyashimo Bw. Marko Shonokwa alisema ''Tunahitaji kituo cha Polisi, Kwani na kituo cha Polisi kilichojengwa na wananchi kukamilika bado wananchi wanaenda Nyamikoma''. 

Kero nyingine  zilizoelezwa na wakazi hao ni  pamoja na  watu kuchukua mamlaka  mkononi na kumtoa madarakani kiongozi aliyeschaguliwa na wananchi. Leseni  ilitajwa kuwa ni changamoto  kwani wakienda kwingine wanakamwatwa kwanini wao wakija huku hawakamatwi.Vilevile ilielezwa kwamba  shamba la Kijiji  limechukuliwa na kumilikiwa na watu binafsi.

Akijibu hoja hizo Mhe. Mkuu wa Mkoa alisema  Eneo la Nyashimo wilaya ya Busega lina ukanda wenye ukubwa wa kilometa za mraba 200 ambazo zinafaa kutumika kwa shughuli ya uvuvi. Uvuvi wa kutumia vizimba ndio wenye tija zaidi mnavyo Vizimba 12, na nimesikia kuwa mnavuna tani 54.

Eneo la kilometa za mraba 200 linaweza  kutumika kutengeneza Vizimba zaidi ya 55,000 na hivyo kupata Samaki kiasi cha tani 250,000, hatimae kuwa vinara katika eneo la uvuvi nchini. Njia nyepesi ya kupata msaada ni kukaa katika vikundi na hivyo kuirahisishia Serikali kutoa msaada mkiwa katika vikundi.

Kuhusu suala la kodi na ushuru, Mkurugenzi na watu wako andaeni taarifa kamili ya aina mbalimbali za ushuru/tozo. Pongezi kwa ujenzi wa Shule, mahitaji yenu ni shule nne namnayo moja, hatua madhubuti zitachukuliwa ili kuona ni kwa jinsi gani tutatatua changamoto hiyo.

MWISHO
MKUU WA MKOA WA SIMIYU- MHE. DAVID KAFULILA AKUTANA NA WADAU WA NYUKI

Mhe. Kafulia amekutana na wadau wa ufugaji wa nyuki Mkoa wa Simiyu ambapo pamoja na mambo mengine alitaka kusikia changamoto zao na namna gani Mkoa unaweza kutatua changamoto hizo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa asali

 Akizungumza Afisa Nyuki Mkoa, Bw.Maganga Juakali Ongala katika taarifa yake kwa Mhe. Kafulila alieleza  kuwa  Mkoa wa Simiyu una vikundi 91 vya ufugaji wa Nyuki.Katika  mwaka wa fedha 2019/2020 uzalishaji wa asali kwa Mkoa ulikuwa lita 31,788. Asali hiyo iliyovunwa kutoka Halmashauri zote Sita za Mkoa wa Simiyu, huku Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi ikiongoza kwa uzalishaji wa lita 8200.

Pamoja na mafanikio hayo wadau wa ufugaji wa Nyuki mkoani hapa wamekuwa wakikabiliana  na Changamoto mbalimbali kama vile, upatikanaji wa soko la asali hii ni ndani na nje ya  nchi.Ukosekanaji wa  mashine za kuchakata na kupaki asali na hivyo kuomba kukopeshwa vifaa hivyo. Changamoto katika kurina asali na utambuzi wa ukomavu wa Asali hivyo elimu inatakiwa kuwa endelevu kwa wazalishaji.

Aidha Wadau hao waliomba Wafugaji binafsi wa Nyuki wakopeshwe mizinga au vifaa vingine muhimu vya Ufugaji nyuki. Changamoto nyingine ni pamoja na Maeneo ya kufugia nyuki, baadhi ya wafugaji nyuki kuchoma mizinga kwa mfano Meatu eneo la Mwasengela kwa kuhofia kunyang'anywa maeneo yao.


Akijibu hoja hizo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. David Kafulila alisema kuwa  ni vyema wafugaji kujiunga kwenye vikundi vya uzalishaji wa asali ili waweze kukopesheka.Ufugaji wa nyuki ni muhimu sana katika uchumi wa Taifa Letu.Vikundi 91 vilivyopo ni vichache sana hivyo basi, vikundi viongezwe ili watu wengi zaidi waweze kufikiwa.
Kwa muda nitakaokuwepo Simiyu nitapenda kuona umaskini wa watu unapungua kupitia shughuli muhimu Sana ya Ufugaji nyuki.Nipo tayari kushughulikia changamoto za ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa asali.Lengo ni kuona kila mfugaji wa nyuki awe na uwezo  wa kutengeneza kipato cha  angalau Tshs.270,000/= kwa mwezi au mil.3 kwa mwaka.

Hivyo ninaelekeza uandaliwe, mkakati utakaoonesha ni vikundi vingapi vilivyopo na vitakavyoongezeka na hitaji la nyongeza ya mizinga au vifaa vingine muhimu ili kuwawezesha wanachama katika vikundi hivyo kutengeneza kipato cha Tshs.270,000/=  kwa mwezi kwa kila mwanachama.Maafisa Nyuki wa Wilaya kwa kushirikiana na Afisa Nyuki Mkoa waandae mkakati wa angalau watu 10,000 waweze kutengeneza kipato cha Tshs.270,000/= kwa mwezi. Mkakati huo uandaliwe kabla au ifikapo tarehe 18/6/2021.

Changamoto ya upatikanaji wa mizinga itafutiwe namna,Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wengine wahusishwe katika upatikanaji wa mizinga hata kwa mkopo, vilevile kwa vifaa vyote vinavyohusiana na ufugaji na uvunaji wa mazao ya nyuki.WMA Makao waandae mkakati kwa ajili ya ufugaji wa nyuki kwa utekelezaji.
MWISHO

Saturday, May 8, 2021

TMDA YATOA MSAADA TAULO ZA KIKE ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 6 SIMIYU

Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) imetoa msaada wa taulo za kike zenye thamani ya shilingi milioni 6 lengo likiwa kuunga mkono maandalizi ya kambi za kitaaluma kwa wanafunzi wa kidato cha nne zinazotarajiwa kuanza mwenzi Agosti, 2021 mkoani Simiyu. 

Akikabidhi taulo hizo meneja wa TMDA kanda ya ziwa Sofia Mziray amesema msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika elimu ambayo ni kipaumbe cha mkoa wa Simiyu huku akiwataka amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili lengo la mkoa huo ya kushika  nafasi ya kwanza  kitaifa. 

“Tumetoa msaada huu kuunga mkono serikali ya mkoa lakini pia tumeona tuwasaidie watoto wa kike waweze kuwepo wakati wote shule, tunataka kusiwe na kisingizio chochote mtoto wa kike kushindwa kuwepo shuleni katika kipindi fulani cha mwezi, sehemu yetu tumefanya tumewaachia ninyi, wito wangu kwenu msome kwa bidii mtimize malengo ya mkoa,” alisema Mziray. 

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameishukuru TMDA kwa msaada huo kuku akitoa rai kwa wazazi kutowatuma wanafunzi katika minada kwa lengo la kuuza bidhaa mbalimbali badala yake kila mzazi aone umuhimu wa elimu na kuifanya elimu kuwa kipaumbele chake kwa kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo. 

Aidha, Mtaka amesisitiza wazazi wenye watoto walio katika madarasa ya mitihani kuwapunguzia kazi ili waweze kupata muda mwingi wa kujisomea kwa ajili ya maandalizi ya mitihani ya Taifa kwa lengo la kufikia azma ya mkoa ya kushika nafasi ya kwanza katika mitihani yote ya Kitaifa.

 

 

Afisa Elimu mkoa wa Simiyu, Mwl. Ernest Hinju amesema misaada inayoendelea kutolewa na wadau mbalimbali wakiwemo TMDA inarahisisha kazi kwa wataalamu wa elimu wanaokuwa na wanafunzi katika kambi za kitaaluma na inachangia kuongeza ari ya kusoma kwa wanafunzi na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri katika mitihani yao. 

Hinju ameomngeza kuwa maandalizi ya kambi za kitaaluma  kwa wanafunzi wa kidato cha nne mkoani hapo zinazotarajia kuanza Agosti, 2021 yameshaanza. 

Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wa kike Jackline Sonda amewashukuru TMDA kwa msaada wataulo za kike na amesema wameupokea msaada huo  kwa mikono miwili huku akiahidi kuwa watasoma kwa bidii kwani miongoni mwa sababu iliyokuwa ikiwafanya baadhi ya wasichana wasihudhurie kikamilifu siku zilizopangwa za kuwepo darasani tayari imepatiwa ufumbuzi.

MWISHO

Baadhi ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Simiyu wakipokea msaada wa taulo za kike kutoka TMDA, wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(katikati ya waanfunzi), Kaimu Meneja wa TMDA Kanda ya Ziwa, Bi. Sophia Mziray (mwenye skafu) na viongozi wengine wa mkoa wa Simiyu. Makabidhiano hayo yamefanyika Mei 7, katika Shule ya Sekondari Simiyu.

TAZAMA PICHA MBALIMBALI KATIKA TUKIO HILO
 

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!