Wednesday, September 28, 2016

NAIBU WAZIRI JAFO AFANYA ZIARA MKOANI SIMIYU

Na Stella Kalinga
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI  Mhe. Suleiman Jafo (Mb) amefanya ziara ya siku mbili Mkoani Simiyu

Akizungumza na  Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Halmashauri ya Mji Bariadi na Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi  katika Ukumbi wa Alliance Mjini Bariadi,  Mhe. Jafo amewataka Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kukaa na wakuu wao wa Idara ili kupanga malengo yanayopaswa kutekelezwa kulingana na bajeti walizopanga katika mwaka wa fedha 2016/2017.

Jafo amesema watumishi wengi wa Umma wamekuwa wakifanya kazi wa mazoea  hivyo wanapaswa kuweka malengo yanayopimika ili kila mwisho wa mwaka wapimwe kulingana na matokeo ya kazi zao kwa mujibu wa mifumo iliyopo ikiwa ni pamoja na Mfumo wa wazi wa mapitio na Upimaji Utendaji kazi (OPRAS) .

Aidha, Jafo amesema Wakurugenzi wanapaswa kuibua na kuvitumia  vipaji kwa watumishi walio tayari kuwatumikia wananchi kupitia taaluma zao badala ya kuwakatisha tamaa na kwa kudidimiza na kutotambua mchango wao.

Wakati huo huo Mhe. Jafo amewataka Wakurugenzi  kusimamia suala la upandaji madaraja kwa watumishi ili lifanyike kwa haki badala ya uonevu na upendeleo.

“Kuna baadhi ya maeneo watu wameajiriwa mwaka 2002,wengine 2003 lakini wanafanana mishahara na watu walioajiriwa mwaka 2012,2013 hawajawahi kupanda madaraja toka wameajiriwa, kwa kuwa kupanda daraja ni kwa upendeleo,mpaka mtumishi ajikombekombe kwa mkuu wa idara. Wakurugenzi kalisimamieni hilo, wakuu wa idara fanyeni kazi yenu, tengenezeni mnyororo wa ushirikiano vizuri ili watu wapande madaraja kwa haki zao.

Sanjari na hilo, Mhe. Jafo amewataka watumishi kutumia elimu na uzoefu walionao kubuni mambo mbalimbali yatayoleta mabadiliko katika maeneo yao na akawataka kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili thamani ya kila mmoja ionekane.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amewataka watumishi wa Mkoa huo kila mmoja kwa nafasi yake  kuyafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Naibu Waziri  huyo na  wafanye kazi zenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Naibu Waziri yuko Mkoani Simiyu kwa ziara ya siku mbili ambapo atatembelea wilaya ya Busega, Bariadi, Itilima na Maswa na kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo na kuzungumza na Watumishi wa Serikali za Mitaa.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo(Mb) akizungumza na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Bariadi Mjini Bariadi, katika ziara yake Mkoani Simiyu.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo(Mb) (kushoto)akizungumza na Watumishi wa Sekretaieti ya Mkoa, Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Bariadi (hawapo pichani)  Mjini Bariadi, katika ziara yake Mkoani Simiyu, (wa pili kushoto) Katibu Tawala Mkoa huo, Jumanne Sagini.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka, akizungumza kabla ya kumkaibisha  Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo(Mb)  azungumze na Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Bariadi Mjini Bariadi.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (wa pili kushoto) akimkaribisha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Robert Lweyo (kulia) ili atoe neno la shukrani kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo(Mb)  baada ya kuzungumza na  Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Bariadi Mjini Bariadi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Robert Lweyo (wa pili kulia) akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo (Mb)  baada ya kuzungumza na  Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Bariadi (hawapo pichani)  Mjini Bariadi

Baadhi ya Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Bariadi wakimsikiliza Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleiman Jafo(Mb) (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Tuesday, September 27, 2016

HATIMAYE MKOA WA SIMIYU WAPATA HOSPITALI TEULE YA RUFAA YA MKOA

Na Stella Kalinga
Hatimaye Hospitali ya Somanda iliyokuwa inamilikiwa na Halmashauri ya Mji wa Bariadi yakabidhiwa rasmi  kwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu  na kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa huo.

Makabidhiano hayo yamefanyika  kati ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Melkizedek Humbe na  Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini mjini Bariadi,  mbele ya Uongozi wa Mkoa, Halmashauri na baadhi ya watumishi wa Hospitali.

Katika Makabidhiano hayo Katibu Tawala Mkoa amekabidhiwa baadhi ya watumishi na Mali kutoka katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambapo Sagini amesema watumishi hao pamoja na wale waliokuwa wakisimamiwa na Katibu Tawala Mkoa hapo awali, wote watasimamiwa na Sekretarieti ya mkoa wa Simiyu, chini ya uangalizi wa Mganga Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa

Akizungumza kabla ya makabidhiano hayo Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amewaasa watumishi  wa Hospitali hiyo kufanya kazi kwa weledi na kuhakikisha wanatoa huduma kwa wagonjwa kulingana na taratibu, maadili na miongozo ya taalum ya kitabibu.

Sagini amesema baadhi ya watumishi wa Idara ya afya wamekuwa wakitumia lugha mbaya isiyowaridhisha wateja wao na hivyo kushindwa kuwapa huduma wanayostahili kwa kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa wakikatishwa tamaa.

“Nisingependa kusikia kuna watumishi wanatumia lugha mbaya kwa wagonjwa, wengine wanapowahudumia mama wajawazito wanawatolea maneno makali ambayo hayawapi faraja, tabia hiyo isionekane kabisa katika Hospitali yetu,  zingatieni maadili ya kazi zenu na muwape wananchi huduma wanayostahili ili waendelee kuwaamini’ alisema Sagini.

Aidha, Sagini alimtaka Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Teule ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa  ashirikiane na viongozi wengine kuhakikisha Hospitali hiyo inatoa huduma bora zinazolingana na hadhi iliyonayo kwa sasa ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu wanufaike kwa kupata huduma bora za Rufaa.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Halmasahuri ya Mji amewataka Watumishi waliokabidhiwa kwa Katibu Tawala Mkoa watumie fursa hiyo kufanya kazi kwa bidii zaidi  ili huduma itakayotolewa iendane na hadhi ya Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashuari ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo ametoa wito kwa Serikali kuu kuhakikisha inajenga majengo bora yatakayokuwa na hadhi ya Hospitali ya Mkoa.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Teule ya Rufaa ya Mkoa, Dkt. Fredrick Mlekwa amesema Wananchi wa Halmashauri zote katika Mkoa wa Simiyu watarajie huduma bora zitakazokidhi kiwango.

Kabla ya Hospitali ya Somanda kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa ilikuwa inahudumia wananchi kutoka katika Halmashauri ya Mji Bariadi na Halmashauri Wilaya  jirani za Bariadi, Itilima na baadhi ya vijiji vya  vya Wilaya ya Busega, lakini kuanzia sasa itahudumia Halmashauri zote sita ikiwemo Maswa na Meatu kwa huduma za Rufaa.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (kushoto) na Mkurugenzi wa Mji wa Bariadi , Melkezedeki Humbe(kulia) wakikabidhiana nyaraka mara baada ya makabidhiano ya Hospitali ya Somanda iliyokuwa ya Halmashauri ya Mji ambayo imefanywa kuwa HospitaliTeule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (kushoto) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi , Robert Lweyo wakipeana mikono baada ya makabidhiano ya nyaraka za Hospitali ya Somanda iliyokuwa ya Halmashauri ya Mji Bariadi ambayo imefanywa kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi , Melkezedeki Humbe (kulia) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Mkoa, Halmashauri na Hospitali ya Somanda kabla ya makabidhiano Hospitali ya Somanda iliyokuwa ya Halmashauri ya Mji Bariadi, ambayo imefanywa kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.


Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini(katikati) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Mkoa, Halmashauri na Hospitali ya Somanda kabla ya makabidhiano Hospitali ya Somanda iliyokuwa ya Halmashauri ya Mji Bariadi, ambayo imefanywa kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi , Robert Lweyo akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Mkoa, Halmashauri na Hospitali ya Somanda kabla ya makabidhiano Hospitali ya Somanda iliyokuwa ya Halmashauri ya Mji Bariadi, ambayo imefanywa kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini(katikati) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Mkoa, Halmashauri na Hospitali ya Somanda kabla ya makabidhiano Hospitali ya Somanda iliyokuwa ya Halmashauri ya Mji Bariadi, ambayo imefanywa kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Mkoa, Halmashauri na Hospitali ya Somanda baada ya makabidhiano Hospitali ya Somanda iliyokuwa ya Halmashauri ya Mji Bariadi, ambayo imefanywa kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.
Baadhi ya Viongozi wa Mkoa, Halmashauri na Hospitali ya Somanda wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (hayupo pichani) kabla ya makabidhiano Hospitali ya Somanda iliyokuwa ya Halmashauri ya Mji Bariadi, ambayo imefanywa kuwa Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.


Sehemu ya Jengo la Utawala la Hospitali ya Somanda iliyokuwa inamilikiwa na Halamshauri ya Mji wa Bariadi  ambayo sasa ni Hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.


Thursday, September 22, 2016

SIMIYU YARIDHIA CHAKULA KITOLEWE KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA KUTWA

Na Stella Kalinga
Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Simiyu (RCC) kimeridhia wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari za Kutwa katika mkoa huo kupata chakula cha mchana shuleni ili kuwatengenezea mazingira mazuri ya kujifunza.

Uamuzi huo umefikiwa kufuatia hoja iliyowasilishwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Simiyu kupitia Chama cha Mapinduzi , Mhe. Leah Komanya juu ya taarifa iliyotolewa na Afisa Elimu Mkoa Mwl. Julius Nestory kuwa takribani asilimia 38 ya wanafunzi katika Mkoa wa Simiyu hawahudhurii masomo kikamilifu.

Mhe. Komanya alisema moja ya sababu inayopelekea wanafunzi kutokwenda shule ni kukosa chakula, hivyo endapo watapata chakula shuleni watashawishika kusoma na muda waliokuwa wanakwenda kutafuta chakula watautumia kwa ajili ya masomo.

Komanya alisema kwa mujibu wa taarifa ya shirika moja la Kimataifa lililofanya utafiti wa athari za mabadiliko ya tabia nchi katika Wilaya ya Meatu,  ilibanishwa kuwa watoto kutoka familia za wanawake wajane zimeathiriwa na uwezo duni, hivyo watoto hawaendi shuleni kwa sababu ya kukosa chakula, hli inayopelekea watoto hao kwenda kujitafutia chakula, jukumu ambalo lingepaswa kufanywa na baba zao .

“Matokeo ya darasa la saba Wilaya ya Meatu mwaka 2015, shule iliyokuwa ya mwisho katika Wilaya ya Meatu ilitoka kata ya Mwamanimba na Kata ya Mwamanimba nilivyofuatilia ni kata iliyofanyiwa tathmini ya athari za mabadiliko ya tabia nchi, kwa hiyo ni wazi kwamba chakula kikipatikana uwezo wa wanafunzi wa kuhudhuria na kuchangia shuleni utakuwa mkubwa” alisema Komanya.

  Mhe.Komanya alisema wazazi kwa umoja wao washirikiane na Serikali katika kuchangia chakula ili kusaidia familia ambazo hazina uwezo wa kuchangia fedha ziweze kutoa mazao ya chakula kwa kuwa wakazi wa Mkoa wa Simiyu walio wengi ni wakulima.

Aidha, Mhe. Komanya ametoa wito kwa mashirika na taasisi mbalimbali kuunga mkono Mkoa wa Simiyu kwa kusaidia kutoa vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na majiko banifu katika shule, nishati itakayotumika kupikia, vyakula na vyombo vya kupikia, ambapo yeye ameahidi kutoa vyombo vya kupikia katika Wilaya zote na akaombaWabunge wote wa Mkoa wa Simiyu wamuunge mkono.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema suala la wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi ni la hiari,  hivyo akatoa maelekezo kwa Viongozi Ngazi ya Wilaya kuwafafanulia wananchi ili wawe na uelewa wa pamoja na wafuate taratibu zinazotakiwa kupata vibali vya kuanza kwa zoezi hilo.

Aidha, Mtaka amewatakahadharisha watendajiwa ngazi zote kuhakikisha wanapotoa vibali hivyo kwa Kamati za Shule na Wazazi kuzingatia taratibu ili wanafunzi wapate chakula badala ya kutafuta mianya ya kujinufaisha kwa namna moja au nyingine.


Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Mhe. Mickness Mahela amesema anaunga mkono utaratibu wa chakula mashuleni na katika kata yake ya Nyashimo vikao vya Maendeleo ya Kata vimeshakaa na kukubaliana kuanza kutoa chakula kwa wanafunzi, ambapo Shule ya Sekondari Nasa inatarajia kuanza kutoa chakula kwa wanafunzi Novemba Mosi, 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) katika kikao kilichafanyika leo, mjini Bariadi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) katika kikao kilichafanyika leo, mjini Bariadi, (Kushoto )Mwenyekiti wa CCM (M), Dkt. Titus Kamani, (kulia) Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Jumanne Sagini
Mbunge waViti Maalum mkoa wa Simiyu (CCM), Mhe. Leah Komanya akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani) mara baada ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo Mjini Bariadi.


Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Simiyu wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Afisa Elimu wa Mkoa, Julius Nestory akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Elimu ,  katika  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Simiyu wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Wednesday, September 21, 2016

MKOA WA SIMIYU WATANGAZA KUANZA KUTUMIA CHAKI UNAZOZALISHA WENYEWE

Na Stella Kalinga
Mkoa wa Simiyu unatarajia kuanza kutumia chaki zilizozalishwa na vijana wa Wilaya ya Maswa mkoani humo kuanzia tarehe Mosi Oktoba, 2016.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Kanisa Katoliki Mjini Bariadi.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkoa huo unatumia jumla ya shilingi milioni 25 kununua takribani katoni 1200 za chaki( ambazo zinatengenezwanje ya nchi)  kwa mwezi katika shule za Msingi na Sekondari, hivyo akawaasa Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda na kuthamini vitu vya nchini kwetu ili kuinua uchumi wa Vijana wazalishaji na Taifa kwa ujumla.

“Tuanze kuwafundisha Watanzania kutoka kwenye dhana ya kuwa Chaki ya Kichina ndiyo bora kuliko inayotengenezwa hapa nchini, nahitaji Maafisa Elimu mkae na Walimu Wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu mjadili na muone namna nzuri ya kupata hizo chaki ambazo zitakuwepo katika Banda la Maswa Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi katika wiki ya vijana na baadaye katika maduka yatakayokuwepo kwenye kila wilaya”, alisema Mtaka.

Mtaka amesema Maafisa Elimu wote wa Wilaya wahakikishe wazabuni wanaopeleka chaki katika Shule za Msingi na Sekondari wananunua chaki zinazozalishwa na Vijana wa Wilaya ya Maswa ambazo zitatambulika kama ‘MASWA CHALKS’, ambapo Vijana wa Maswa watafungua duka  kwa kila wilaya hivyo badala ya kuzifuata chaki hizo mahali zinapozalishwa kila wilaya itazipata chaki hizo katika eneo husika

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama atakapokuja katika Uzinduzi wa wiki ya vijana Oktoba 08, 2016 atakwenda kutembelea kiwanda hicho,  kujione uzalishaji unavyoendelea na baadaye Mkoa utaomba kibali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.   John Pombe Joseph Magufuli,  kuruhusu Vijana hawa  wa Kitanzania  kuzalisha bidhaa hii kwa kutumia malighafi kutoka hapa nchini na kuiuza nchi nzima.

Aidha, Mtaka amesema katika Azma ya Mkoa ya kila wilaya kuzalisha bidhaa moja yaani (one distict one product) pamoja na Vijana wa Maswa kuzalisha chaki, Vijana wa Wilaya ya Meatu watakuwa wakisindika maziwa ya ng’ombe kwa kuwa ni Wilaya ya Meatu  ndiyo yenye ng’ombe wengi, hivyo kupitia mradi huo wafugaji wa Meatu na Simiyu kwa ujumla watapata soko la maziwa na thamani yake itaongezeka na yatauzwa katika maduka yatakayokuwepo katika kila wilaya.

Amewataka viongozi kuondokana na dhana ya kuwa kupungunza mifugo ndio njia pekee ya kuwakomboa wafugaji na badala yake wawasaidie kupata majawabu ya changamoto zao ikiwa ni pamaja na kuongeza thamani mazao ya mifugo kama maziwa, ngozi na nyama.

Sanjali na hilo Mtaka ameeleza azma ya kuufanya Mkoa wa Simiyu kuwa Mkoa wa mfano wa kuigwa hasa katika utekelezaji wa maagizo ya Viongozi  Kitaifa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015.

Kwa upande wake Naibu ,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Luhaga Mpina amepongeza jitihada hizo zinazofanywa na akaahidi kushirikiana na Serikali ya Mkoa katika suala la uanzishwaji wa viwanda vidogo ambapo aliahidi kusaidia Mkoa wa Simiyu upate kiwanda cha kutengeneza mkaa kwa kutumia mimea mingine tofauti na miti ili kulinda na kutunza mazingira.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa nne kushoto) akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa sampuli za chaki (MASWA CHALS) zinazozalishwa na Vijana wa Maswa amabazo zinatarajiwa kuanza kuuzwa Oktoba Mosi, 2016
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) (hawapo pichani) katika kikao kilichafanyika leo, mjini Bariadi

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) katika kikao kilichafanyika leo, mjini Bariadi, (Kushoto )Mwenyekiti wa CCM (M), Dkt. Titus Kamani, (kulia) Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Jumanne Sagini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(wa pili kushoto) akiwaonesha wajumbe wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa gudulia la Maziwa ya Ng’ombe  yaliyotengenezwa na Vijana wa Meatu(MEATU MILK). (Kushoto )Mwenyekiti wa CCM (M), Dkt. Titus Kamani, (kulia) Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Jumanne Sagini.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza akimmiminia maziwa yaliyotengenezwa na Vijana wa Wilaya hiyo, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,  Muungano na Mazingira ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa ,  na Mhe. Luhaga Mpina
Mkurugenzi wa Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza akimmiminia maziwa yaliyotengenezwa na Vijana wa Wilaya hiyo; Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Simiyu wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Bariadi
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akichangia jambo katika  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) wa Simiyu wakifuatilia mijadala mbalimbali katika kikao cha kamati hiyo kilichofanyika leo Mjini Bariadi
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga akichangia jambo katika  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo Mjini Bariadi

Mbunge waViti Maalum mkoa wa Simiyu (CCM), Mhe. Leah Komanya akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani) mara baada ya kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,  Joseph Nandrie akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Kilimo na Mifugo ,  katika  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo Mjini Bariadi
Mchungaji wa Kanisa la AICT Bariadi, Josephati Magori akichangia jambo katika  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo Mjini Bariadi.
Afisa Elimu wa Mkoa,Mwl. Julius Nestory akiwasilisha taarifa ya Maendeleo ya Elimu ,  katika  kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa kilichofanyika leo Mjini Bariadi.

Tuesday, September 20, 2016

RC AWATAKA WATENDAJI WA HALMASHAURI NA MADIWANI KUTOINGIZA MASLAHI BINAFSI KATIKA MIRADI YA BARABARA

Na Stella Kalinga
Madiwani na watendaji wa Halmashauri wameaswa kuacha kuingiza maslahi binafsi katika ujenzi wa miradi ya barabara ili kufanya miradi kusimamiwa na kujengwa katika kiwango kinachostahili.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony John Mtaka katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika katika Ukumbi wa kanisa Katoliki Mjini, Bariadi.

Mtaka amesema ili miradi ya ujenzi wa barabara isimamiwe vizuri na iweze kujengwa kwa viwango vinavyotakiwa madiwani na watendaji wasiwe sehemu ya wazabuni au wakandarasi wa miradi hiyo, ili waweze kuwasimamia wakandarasi wa miradi hiyo na kuwachukulia hatua pale wanapotekeleza miradi chini ya kiwango.

Aidha, Mtaka amewataka Wenyeviti wa Halmashauri kusimamia kwa umakini vikao vya mabaraza ya madiwani vya kuamua matengenezo ya barabara ili kipaumbele cha kwanza kiwe ni kwa barabara ambazo zimeharibika sana.

“Wenyeviti wa Halmashauri waongozeni madiwani kuepuka ubinafsi katika miradi ya barabara ambapo kila Diwani anataka apewe fedha kidogo kidogo ya kujenga au kukarabati hata kama fedha hiyo ni kidogo sana. Kipaumbele cha kwanza kiwe ni barabara ambazo zimeharibika sana au hazipitiki kabisa katika Halmashauri” alisema Mtaka.

Sanjali na hilo Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi wa ngazi zote kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa alama za barabarani zinazowekwa na Wakandarasi na Wakala wa Barabara(TANROADS) pamoja na kuacha kupitisha mifugo barabarani ambayo inasababisha mmomonyoko wa udongo ili barabara zidumu.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amesisitiza Wahandisi wa Halmashauri kuhakikisha wanaweka alama katika mipaka ya hifadhi ya barabara ili iwe rahisi kutambua na kuepuka maeneo hayo kuvamiwa na kutumiwa tofauti na yalivyokusudiwa. 
  
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Mhe. Satanslaus Nyongo amesema Wakala wa Barabara(TANROADS) kwa kushirikiana na Wabunge wa Mkoa wa Simiyu, wafanye jitihada za kuzungumza na Waziri mwenye dhamana na ujenzi wa Barabara ili kipande cha barabara cha Maswa hadi Bariadi chenye kilomita 50 kitengewe fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami; kwa kuwa barabara ya Mwigumbi-Maswa-Bariadi –Lamadi itakapokamilika itaweza kuunganisha Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine hivyo kuufungua kiuchumi.

Akizungumzia barabara hiyo Meneja wa Mkoa wa Wakala wa Barabara(TANROADS) Mhandisi Albert Kent amesema kipande cha Lamadi-Bariadi kimekamilika, mkandarasi anaendelea na ujenzi wa kipande cha Mwigumbi-Maswa na kipande cha Maswa hadi Maswa kitajengwa kulingana na kadri kaitakavyotengewe fedha katika bajeti, kwa kuwa utekelezaji wa mradi huo unategemea upatikanaji wa fedha.

Mkoa wa Simiyu una mtandao wa barabara zenye jumla ya kilomita 4,730.95 ambazo zimegawanyika katika makundi yafuatayo:-Barabara kuu kilometa 334.72, barabara za Mkoa kilometa532.30, barabara za wilaya kilometa 2420.5 na barabara za vijijini 1451.53; kati ya hizi kilomita 141.76 zina kiwango cha lami, kilomita 2453.59 kiwango cha chanagarawe na kilometa 2134.7 za kiwango cha udongo. 


Kutoka kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Antony Mtaka, Katibu Tawala Mkoa, Jumanne Sagini na Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Luhaga Mpina wafuatilia mjadala katika kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya Barabara katika Mkoa


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony John Mtaka (kulia) akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao cha Bodi hiyo kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya barabara katika mkoa (kushoto) ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina (kulia) akichangia jambo katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika Mjini Bariadi Mkoni Simiyu kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya Barabara katika Mkoa , (kushoto) Katibu Tawala wa Mkoa huo, Jumanne Sagini.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Mhe. Stanslaus Nyongo (kushoto) akichangia jambo katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa, kilichofanyika Mjini Bariadi Mkoni Simiyu kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya Barabara katika Mkoa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Dkt. Titus Kamani akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Barabara kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya Barabara katika Mkoa huo. 
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka ktika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya Barabara katika Mkoa.
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mhe. Dkt Seif Shekalaghe (wa pili kushoto, mstari wa pili) akichangia jambo katika Kikao Cha Bodi ya Barabara kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya Barabara katika Mkoa
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony John Mtaka (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa(hawapo pichani) katika kikao cha Bodi ya hiyo kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya barabara katika mkoa, (kulia) Katibu Tawala Mkoa Simiyu, Jumanne Sagini.
Meneja wa Mkoa wa Wakala wa Barabara(TANROADS), Mhandisi Albert Kent akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Barabara kwa wajumbe wa kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa kilichofanyika Mjini Bariadi,  kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya Barabara katika Mkoa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa akichangia jambo katika Kikao Cha Bodi ya Barabara kilichofanyika Mjini Bariadi kwa lengo la kupanga na kujadili maendeleo ya Barabara katika Mkoa.

Saturday, September 17, 2016

WAZIRI MHAGAMA AFANYA ZIARA SIMIYU KUONA HALI YA MAANDALIZI YA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2016

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama amefanya kikao cha ndani na Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu leo katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Mjini Bariadi, ili kupata taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016 .

Mkoa wa Simiyu umepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo kwa mwaka huu. Maadhimisho ya wiki ya vijana yatafunguliwa rasmi tarehe 08 Oktoba 2016 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama na kuhitimishwa tarehe 14 Oktoba, 2016, ambapo Vikundi vya Vijana na Wajasiriamali kutoka mikoa yote nchini watashiriki na kuonesha kazi zao za uzalishaji ikiwa ni pamoja na shughuli za ugunduzi wa vitu mbalimbali katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi.

Pamoja na maonesho ya kazi za vijana, Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Baba  kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere yatafanyika tarehe 14 Oktoba 2016 katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli .

Mhe. Mhagama amesema Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2016 ni ya Kihistoria kwa kuwa ni ya kwanza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli  na tukio la kihistoria kwa Mkoa wa Simiyu pia.

Akiwa Wilayani Bariadi  Mhe. Mhagama pamoja na kufanya kikao na viongozi na watendaji, alitembelea na kuona Kanisa la Mtakatifu Yohana(John) la Mjini Bariadi, ambapo Ibada ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere itafanyika, Uwanja wa Sabasaba utakaotumika katika maonesho ya kazi za vijana katika wiki ya vijana na Uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi ambao utatumika katika Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Oktoba 14, 2016.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini mara baada ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya kukutana na Viongozi na Watendaji wa Mkoa huo, kupata taarifa na kujionea maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016 .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Afisa Usalama Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kuwasili mjini Bariadi kwa ajili ya kukutana na Viongozi na Watendaji wa Mkoa huo, kupata taarifa na kujionea maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016 .
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kulia)akitoa maelezo ya utangulizi (Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka) kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama, kabla ya kumkaribisha Katibu Tawala Mkoa, Jumanne Sagini (hayupo pichani) kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akipokea taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016 , kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini.

: Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) , mara baada ya kupata taarifa na kujionea hali ya maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016, (kulia) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama Katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Kanisa la Mtakatifu Yohana(John) la Mjini Bariadi, mahali ambapo Ibada ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa itafanyika tarehe 14 Oktoba  2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akiagana na Padre Kizito Nyanga  mara baada ya kutembelea Kanisa la Mtakatifu Yohana (John) la mjini Bariadi , mahali ambapo Ibada ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa itafanyika tarehe 14 Oktoba  2016
Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo baada ya kukagua sampuli ya mabanda yatakayotumiwa na vijana katika maonesho ya kazi zao wakati wa maonesho ya wiki ya vijana atakayoyafungua rasmi tarehe 08 Oktoba, 2106 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi, (kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Jemasi  Kajugusi
: Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akiangalia baadhi ya miundombinu (haipo pichani) itakayotumiwa na vijana katika maonesho ya kazi zao wakati wa maonesho ya wiki ya vijana atakayoyafungua rasmi tarehe 08 Oktoba, 2106 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi, ( kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, Katibu Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini,  (kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Jemasi Kajugusi.
Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu baada ya kukagua sampuli ya mabanda takayotumiwa na vijana katika maonesho ya kazi zao wakati wa maonesho ya wiki ya vijana atakayoyafungua rasmi tarehe 08 Oktoba, 2106 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi, ( kutoka kulia), Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga, Katibu Tawala mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini,  (kulia) Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu, Bw. Jemasi Kajugusi.

Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Vijana kutoka katika Ofisi yake Bw. Jemasi Kajugusi(wa kwanza kulia),  akiwa na Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu baada ya kukagua sampuli ya mabanda  yatakayotumiwa na vijana katika maonesho ya kazi zao wakati wa maonesho ya wiki ya vijana atakayoyafungua rasmi tarehe 08 Oktoba, 2106 katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Bariadi.Vijana wa Halaiki wa Mkoa wa Simiyu wakitoa heshima mbele ya Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipowatembelea wakati wa ziara yake ya kukagua na kuona Maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016.


:Vijana wa Halaiki wa Mkoa wa Simiyu wakitoa heshima mbele ya Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipowatembelea wakati wa ziara yake ya kukagua na kuona Maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016 .

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (wa pili kushoto,  mbele)  akiwa na Viongozi wengine na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama wakati alipotembea na kukagua Uwanja wa Halmashauri ya Mji Bariadi,  ambao utatumika katika maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, Oktoba 14, 2016. 

Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjni Bariadi kwa lengo la kupata taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016 .
Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu , Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika Mjni Bariadi kwa lengo la kupata taarifa ya maandalizi ya Maadhimisho ya Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa, yanayotarajiwa kufanyika mkoani humo tarehe 8 na 14 Oktoba  2016 .

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!