Shirika
lisilo la Kiserikali la AGPAHI limetoa msaada wa jumla ya vifaa 50 vya kupima
joto mwili vyenye thamani ya shilingi 12,500,000/= kwa mkoa wa Simiyu kwa ajili
ya kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Awali akizungumza kabla
ya kukabidhi vifaa hivyo Mratibu wa AGPAHI Mkoa wa Simiyu, Dkt. Julius Sipemba amesema
Shirika hilo limefuata maelekezo ya Serikali katika utoaji wa misaada ambapo
amebainisha kuwa vifaa hivyo vimepitia wizara ya afya na kupata kibali cha
kuvigawa katika mikoa ili vipelekwe katika vituo vya kutolea huduma.
Akipokea msaada huo kwa
niaba ya serikali Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
ameishukuru AGPAHI kwa kutoa vifaa vya kupima joto mwili na kusema kuwa awali
Mkoa huo ulikuwa na uhaba wa vifaa hivyo; huku akibainisha kuwa vifaa hivyo
vitasaidia hususani kwenye maeneo ambayo yalikuwa hayana ili kuwapima watu joto
mwili kabla ya kuingia kwenye maeneo hayo.
Wakati huo huo Sagini
ameushukuru Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa
wa Simiyu kwa msaada wa vifaa vya kunawia mikono kuunga mkono juhudi za
serikali, katika kuchukua tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya Corona na
kusisitiza kuwa vifaa hivyo vitapelekwa katika maeneo yenye mkusanyiko wa watu
wengi.
“RUWASA ni taasisi mpya
lakini pamoja na upya wake wamejinyima na kutoa shilingi 1,750,000/= kununua
vifaa hivi ili kuokoa maisha ya watu; pamoja na kuhakikisha tunapata maji safi
na salama wameona waunge mkono juhudi za serikali kuhakikisha watu wananawa na
sabuni na maji tiririka kujikinga na Corona, mkoa tunatambua mchango wenu,”
alisema Sagini.
Akizungumza kwa niaba
ya Meneja wa RUWASA Mkoa wa Simiyu, Mhandisi Mahobe Mahuyemba amesema RUWASA
kama wakala mpya umetoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuonesha uhusiano wake na
jamii katika kile kinachofanyika katika utekelezaji wa miradi m ya maji na
uhalisia wa maisha ya watu huku akisisitiza
kuwa vifaa hivyo kupelekwa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu ikiwemo
shule na hospitali.
Kwa upande wake Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amewashukuru AGPAHI na RUWASA kwa
msaada huo kwa jamii ya watu wa Simiyu huku akibainisha namna mkoa wa Simiyu
ulivyonufaika na uwepo wa AGPAHI kama wadau muhimu wa afya.
“Kama mkoa tumekuwa
tukishirikiana na AGPAHI kuboresha huduma za afya katika nyanja mbalimbali
ikiwemo kuboresha huduma za afya kwa watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI kwa
kutoa huduma za matibabu, kujenga uwezo kwa watoa huduma wanaowahudumia, kutoa
magari kwa ajili ya usimamizi shirikishi na kujenga miundombinu yakiwemo
majengo,” amesema Dkt. Dugange.
MWISHO
Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI Mkoa wa Simiyu, Dkt. Julius Sipemba (kushoto) akimuonesha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini moja ya kifaa cha kupima joto mwili ambavyo vimetolewa msaada Juni 25, 2020 na Shirika hilo kwa mkoa wa Simiyu ili kuunga mkono juhui za Serikali katika tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (wan ne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, AGPAHI na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kupima joto mwili kutoka AGPAHI na vifaa vya kunawia mikono Juni 25, 2020 kutoka RUWASA kwa ajili ya tahadhari ya maambukizi ya CORONA.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akinawa mikono kwa sabuni na maji tiririka katika moja ya vifaa vilivyotolewa msaada na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya CORONA, Kulia ni Mhandisi kutoka RUWASA Simiyu Mahobe Mahuyemba.
Sehemu ya msaada wa vifaa vya kunawia mikono vilivyotolewa kama msaada kwa mkoa wa Simiyu Juni 25, 2020 na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya CORONA.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akivikagua vifaa vilivyotolewa msaada kwa mkoa huo na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Simiyu kwa ajili ya kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya CORONA, kulia ni Mhandisi kutoka RUWASA Simiyu Mahobe Mahuyemba.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini (wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, AGPAHI na Wakala wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Simiyu mara baada ya kupokea msaada wa vifaa vya kupima joto mwili kutoka AGPAHI na vifaa vya kunawia mikono Juni 25, 2020 kutoka RUWASA kwa ajili ya tahadhari ya maambukizi ya CORONA.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange akimpima joto Mhandisi kutoka RUWASA Simiyu Mahobe Mahuyemba kwa kutumia kifaa cha kupimia joto mwili ambacho ni miongoni mwa vifaa hivyo 50 vilivyotolewa msaada na AGPAHI Juni 25, 2020 kwa ajili kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya CORONA.
Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali la AGPAHI Mkoa wa Simiyu, Dkt. Julius Sipemba (kushoto) akimuonesha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini moja ya kifaa cha kupimia joto mwili ambavyo vimetolewa msaada Juni 25, 2020 na Shirika hilo kwa mkoa wa Simiyu ili kuunga mkono juhui za Serikali katika tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Mratibu wa Shirika lisilo
la kiserikali la AGPAHI Mkoa wa Simiyu, Dkt. Julius Sipemba (kushoto)
akimuonesha Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini moja ya kifaa
cha kupimia joto mwili ambavyo vimetolewa msaada Juni 25, 2020 na Shirika hilo kwa mkoa wa Simiyu ili kuunga
mkono juhui za Serikali katika tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona.