Shirika
lisilo la kiserikali la CUAMM Doctors With Africa kupitia Mradi wa Test and
Treat limejenga jengo jipya la huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye maambukizi
ya Virusi vya Ukimwi, kukarabati baadhi ya majengo na kuchimba kisima cha maji katika zahanati ya Old Maswa iliyopo Halmashauri
ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa jengo hilo (katika zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Jimbo Katoliki Shinyanga) Juni
18, 2020 kwa niaba ya Askofu wa Jimbo
Katoliki Shinyanga, Liberatus Sangu, Makamu
wa Askofu huyo Padri Kizito Nyanga, ameishukuru
CUAMM Doctors with Africa kwa msaada huo na kuahidi kuendelea kushirikiana na
Serikali na wadau wote walio tayari kuhudumia watu.
“Tunawashukuru sana CUAMM kwa
msaada wa jengo hili, vifaa na ukarabati wa majengo mengine katika zahanati ya
Old Maswa; Kanisa lina kiu ya kuwafikia watu kwa huduma siyo maneno na liko
tayari kushirikiana na wote wanaotaka kuwahudumia watu,” alisema Padri Nyanga.
Aidha, Padri Kizito ameishukuru
serikali kwa kuliamini kanisa hususani jimbo Katoliki Shinyanga, kuliamini
kanisa katika kutoa huduma kwa wananchi, kulidhamni katika kuendeleza huduma na
kutoa ushauri wa mara kwa mara katika uendeshaji wa taasisi za kanisa.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali
katika uzinduzi wa jengo hilo Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt.Khamis
Kulemba amesema CUAMM ni miongoni mwa wadau ambao wanafanya kazi kulingana na
malengo ya serikali ya mkoa ya kuboresha miundombinu katika sekta ya afya.
Wakati huo huo Kulemba amewataka
wataalam afya katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa kushirikiana na
watumishi wa Zahanati ya Old Maswa kuhakikisha huduma zinazotolewa katika jengo
hilo la CTC na zahanati hiyo kwa ujumla zinakuwa ni za ubora unaotakiwa na ziendane na thamani ya mradi huo.
Katika hatua nyingine Dkt.
Kulemba ametoa wito kwa viongozi wa Dini mkoani Simiyu kuendelea kushirikiana
na wataalam wa afya katika kulinda afya ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi(VVU),
wanaotumia dawa za kufubaza makali ya
VVU katika kuwahimiza watumie dawa hizo kwa usahihi badala ya kuwataka kuacha
kutumia dawa hizo baada ya kuwaombea.
“Nawaomba viongozi wa dini washirikiane
na wataalam kulinda afya za watu wenye VVU, baadhi yao wamekuwa wakiwaombea
watu wenye VVU na kuwaambia waache kutumia dawa; watu hao wakiacha kutumia dawa
wanakuwa na hali mbaya; kuacha kutumia dawa na kuzirudia tena kunawaletea shida
na kutengeneza usugu, nawaomba viongozi wa dini watusaidie kwenye hili,”
alisema Kulemba.
Naye Mganga mfawidhi wa zahanati
ya Old Maswa Ndaro Lawi amesema huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye Virusi
vya Ukimwi (VVU) katika zahanati hiyo zilianza mwaka 2016, ambapo hadi sasa jumla ya watu 219 wameandikishwa katika kituo
hicho na wanapata huduma mbalimbali bila
malipo.
Kwa upande wake Mratibu wa mradi
wa Test and Treat kutoka CUAMM Doctors With
Africa mikoa ya Shinyanga na Simiyu,
Ndg. Ndg. Franscesco Bonanome amewashukuru watumishi wa CUAMM, viongozi wa
Serikali na Jimbo Katoliki Shinyanga kwa namna walivyofanya kazi kwa ushirikiano
na kuahidi kuwa shirika hilo litaendelea kufanya mambo makubwa siku za zijazo.
Ujenzi wa Jengo la CTC na
ukarabati wa majengo mengine katika Zahanati ya Old Maswa umegharimu shilingi
209, 885, 665/= huku uchimbaji wa kisima ukigharimu shilingi 39,533,540/=
MWISHO
Makamu wa Askofu wa
Jimbo Katoliki Shinyanga, Padri Kizito Nyanga (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo
jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watuwanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC)
Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa
Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors
With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat; katika Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na
Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga (Kulia) Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Dkt. Khamis Kulemba na (kushoto) Mratibu wa Mradi wa Test and Treat Shinyanga na Simiyu ,
Ndg. Franscesco Bonanome.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati
ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga (kushoto) akitoa
maelezo ya utoaji wa huduma katika zahanati hiyo kwa viongozi mbalimbali walioshirikia
katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi
na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la
Kiserikali la Doctors With Africa-CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat (kulia)
ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamisi Kulemba wa Mradi wa Test and Treat Shinyanga na Simiyu ,
Ndg. Franscesco Bonanome.
Mhandisi wa ujezi aliyekuwa
akisimamia ujezi wa jengo jipya la Huduma
za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi naVirusi vya Ukimwi (CTC ) katika
Zahanati ya Old Maswa lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali
la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat, akitoa maelezo ya
namna ukarabati wa majengo mbalimbali katika zahanati ya Old Maswa
ulivyofanyika kwa viongozi mbalimbali kabla ya uzinduzi wa jengo hilo Juni 18,
2020.
Makamu wa Askofu wa
Jimbo Katoliki Shinyanga, Padri Kizito Nyanga akizungumza na viongozi na
watendaji mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba
na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la
Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM
kupitia mradi wa; katika Zahanati ya Old
Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa, Dkt. Khamis Kulemba akizungumza na viongozi na watendaji mbalimbali
katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watuwanaoishi
na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la
Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM
kupitia mradi wa Test and Treat; katika Zahanati
ya Old Maswa inayomilikiwa na kanisa Katoliki.
Mratibu wa Mradi wa Test and Treat Shinyanga na Simiyu ,
Ndg. Franscesco Bonanome akizungumza na viongozi
na watendaji mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba
na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC )Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la
Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM
kupitia mradi wa Test and Treat; katika
Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Makamu
wa Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Padri Kizito Nyanga (wa pili kulia
walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watendaji mbalimbali katika hafla
ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na
Virusi vya Ukimwi (
Sehemu ya mbele ya
jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wenye Virusi vya Ukimwi (CTC)
Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa
Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa
Test and Treat; katika Zahanati ya Old
Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga (kushoto) akitoa maelezo ya utoaji wa huduma katika zahanati hiyo kwa viongozi mbalimbali walioshirikia katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa-CUAMM kupitia mradi wa Test and Trea.t
:- Makamu wa Askofu wa
Jimbo Katoliki Shinyanga, Padri Kizito Nyanga (wa pili kulia walioketi) akiwa
katika picha ya pamoja na viongozi na
watendaji mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba
na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC
)Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada
wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat; katika Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na
Kanisa Kanisa Katoliki.
Mhandisi wa ujenzi aliyekuwa
akisimamia ujezi wa jengo jipya la
Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi naVirusi vya Ukimwi (CTC ) katika
Zahanati ya Old Maswa lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali
la Doctors With Africa- CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat, akitoa maelezo
ya namna ukarabati wa majengo mbalimbali katika zahanati ya Old Maswa
ulivyofanyika kwa viongozi mbalimbali kabla ya uzinduzi wa jengo hilo Juni 18,
2020.
Mwakilishi wa Mganga
Mkuu wa Halashauri ya Mji wa Bariadi, akitoa taarifa katika hafla ya uzinduzi
wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya
Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa
kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa-CUAMM kupitia
mradi wa Test and Treat
Baadhi ya viongozi wakikagua
ujenzi wa nyumba ya pampu ya kisima cha maji kilichochimwa kwa msaada wa
Shirika lisilo la Kiserikali la Doctor With Africa CUAMM katika zahanati ya Old
Maswa kabla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi
na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020
lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With
Africa-CUAMM kupitia mradi wa Test and Treat
Makamu wa Askofu wa
Jimbo Katoliki Shinyanga, Padri Kizito Nyanga (katikati), Kaimu Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Dkt. Khamis Kulemba(kulia) na (kushoto) Mratibu wa Mradi wa Test and Treat Shinyanga na Simiyu ,
Ndg. Franscesco Bonanome wakipiga makofi kufurahia uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na
matunzo kwa watuwanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la
Kiserikali la Doctors With Africa- CUAMM
kupitia mradi wa Test and Treat; katika
Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga.
Mganga Mfawidhi wa
Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga
(kushoto) akitoa maelezo ya utoaji wa huduma katika zahanati hiyo kwa viongozi
mbalimbali walioshirikia katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za
tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18,
2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika
lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa-CUAMM kupitia mradi wa Test and
Treat.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Old Maswa inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga (kushoto) akitoa maelezo ya utoaji wa huduma katika zahanati hiyo kwa viongozi mbalimbali walioshirikia katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa-CUAMM kupitia mradi wa Test and Trea.t
Baadhi ya Viongozi wa
kanisa Jimbo Katoliki Shinyanga, Serikali na Shirika lisilo la Kiserikali wakifuatilia
matukio mbalimbali katika hafla ya uzinduzi
wa jengo jipya la Huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Virusi vya
Ukimwi (CTC ) Juni 18, 2020 lililojengwa
kwa msaada wa Shirika lisilo la Kiserikali la Doctors With Africa-CUAMM kupitia
mradi wa Test and Treat.
0 comments:
Post a Comment