Wananchi
wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu wameipongeza Serikali kwa kuwajengea
mahakama ya Wilaya ya Bariadi na Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu jambo ambalo
limeapunguzia adha ya kutumia gharama na muda mrefu kwenda kufuata huduma za
mahakama katika mkoa wa Shinyanga kama ilivyokuwa awali.
Akizungumza katika hafla
ya uzinduzi wa jengo la mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu na Mahakama ya Wilaya
ya Bariadi ambayo ilifanyika Juni 22, 2020 Mjini Bariadi, Bw. Zengila Nyoni
mkazi wa Bariadi ameomba watumishi wa mahakama kutoa huduma kwa kuzingatia
misingi ya haki ili umuhimu wa uwepo wa mahakama uonekane kwa wananchi.
“Tunaishukuru Serikali
kutujenge jengo zuri la mahakama, sasa hivi hatutasafiri kwenda Shinyanga
kufuata huduma za mahakama ya hakimu mkazi ni hapa hapa tu; niwaombe mahakimu
na majaji kutoa haki kwa wananchi ili tufurahie uwepo wa jengo hili zuri, maana
haitakuwa na faida kama tumejengewa jengo zuri halafu huduma zisiwe nzuri,”alisema
Nyoni.
Awali
akizungumza katika uzinduzi huo Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe.
Dkt. Eliezer Feleshi amewashauri Wakuu wa Wilaya na Mikoa nchini kutumia kamati za maadili za wilaya ambazo
wao ni wenyeviti wa kamati hizo kuwajadili mahakimu ambao wanaenda kinyume na
maadili ya utumishi wa Umma.
“ Ni aibu kwa Mkuu wa Wilaya au Mkuu wa Mkoa
kusema kuwa hamtaki hakimu fulani kwenye eneo lake wakati yeye ndiyo mwenyekiti wa kamati ya maadili ya
wilaya au mkoa, mahakimu wasio waadilifu wafikisheni kwenye kamati za maadili, zile
kamati zinajuimisha watu wengi wazuri; niendelee kuwasihi watumishi wa Mahakama
kujiepusha na vitendo vilivyo kinyume na maadili,” alisea Jaji Feleshi.
Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Eliezer Feleshi(katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo la mahakama
ya wilaya ya Bariadi na mahakama Hakimu mkazi Simiyu, uzinduzi uliofanyika
Mjini Bariadi Juni 22, 2020.
Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Eliezer Feleshi(katikati) akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa jengo la
mahakama ya wilaya ya Bariadi na mahakama Hakimu mkazi Simiyu, uzinduzi uliofanyika Mjini Bariadi Juni 22, 2020.Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Shinyanga, Mhe. Gerson Mdemu akizungumza na viongozi mbalimbali, watumishi wa mahakama na wananchi katika hafla ya uzinduzi wa jengo la mahakama ya wilaya ya Bariadi na mahakama Hakimu mkazi Simiyu, uzinduzi uliofanyika Mjini Bariadi Juni 22, 2020.
Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Eliezer Feleshi(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi katika mhimili wa mahakama na mahakimu wa Mahakama mbalimbali mkoani
Simiyu(waliosimama) baada ya uzinduzi wa jengo la mahakama ya wilaya ya Bariadi
na mahakama Hakimu mkazi Simiyu, uzinduzi uliofanyika Mjini Bariadi Juni 22,
2020.
Katibu wa Itikani na Uenezi wa CCM Mkoa wa Simiyu, Bw.
Mayunga George akitoa salamu za Chama katika hafla ya uzinduzi wa jengo la
mahakama ya wilaya ya Bariadi na mahakama Hakimu mkazi Simiyu, uzinduzi uliofanyika
Mjini Bariadi Juni 22, 2020.Baadhi ya viongozi wa taasisi, watumishi wa mahakama na wananchi wakifuatilia kwa makini matukio mbalimbali katika hafla ya uzinduzi wa jengo la mahakama ya wilaya ya Bariadi na mahakama Hakimu mkazi Simiyu, uzinduzi uliofanyika Mjini Bariadi Juni 22, 2020.
Jaji kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt.
Eliezer Feleshi (wa pili kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa
watumishi kuhusu jengo la mahakama ya wilaya ya Bariadi na mahakama Hakimu
mkazi Simiyu, baada ya uzinduzi wa jengo hilo uliofanyika Mjini Bariadi Juni
22, 2020.
0 comments:
Post a Comment