Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
amewataka viongozi na watendaji waandamizi katika idara ya elimu mkoani hapa
kuhakikisha kuwa kila mmoja katika eneo lake anasimamia taaluma kwa kuzingatia
matokeo yanayotarajiwa na mkoa.
Sagini
ameyasema hayo jana katika kikao kazi cha viongozi hao ambacho kimewahusisha
maafisa Elimu na Maafisa Taaluma wa Wilaya, Maafisa Takwimu, wawakilishi wa
Wakuu wa Shule, walimu wakuu, waratibu
elimu kata, wadhibiti ubora pamoja na maafisa wa Tume ya Utumishi wa Walimu
kilichofanyika katika shule ya Msingi Lukungu wilayani Busega.
“Mnapojadili
hapa kila mmoja akumbuke nafasi yake katika kuhakikisha kuwa usimamizi wa
taaluma kwenye mkoa wetu unaendelea kutupa matokeo tunayoyatarajia, kila kada
yenu mnapokutana mkumbuke ajenda ya mkoa wetu sisi elimu na ndiyo kipaumbele
chetu,” alisema Sagini.
0 comments:
Post a Comment