Kituo cha utafiti wa kilimo nchini (TARI) kimechagua eneo la
viwanja vya maonesho ya nane nane vilivyopo kata ya Nyakabindi
wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kuwa kituo endelevu cha uenezaji wa teknolojia
lengo likiwa kuwawezesha wakulima kupata huduma za kilimo kwa mwaka
mzima.
Hayo yamebainishwa na Bibi. Mshaghuley Ishika kutoka TARI Dodoma
kwenye kikao cha maandalizi nane nane kilichofanyika Juni 15, 2020 kwenye
jengo la mkoa wa Simiyu lililopo kwenye viwanja hivyo kikwahusiaha viongozi wa
Kanda ya ziwa Mashariki(Simiyu, Mra na Shinyanga).
Aidha, Ishika amesema kituo hicho kitawarahisishia wakulima
kupata bidhaa zinazozalishwa kwenye Kituo hicho ambapo kwa hapa nchini
huzalishwa katika vituo 17, huku
akibainisha kuwa TARI kwa kutambua hilo wameamua kuongeza eneo la vipando katika
Viwanja vya Nyakabindi na kufikia hekari 3.
"Mbali na kuwa kituo endelevu cha usambazaji teknolojia kutakuwa
vifaa na duka la mbegu zinazozalishwa na TARI ambazo zinapatikana katika
vituo 17 hapa nchini na litamsaidia mkulima kujifunza mengi kuhusiana na
kilimo; kituo hiki pia kimepatiwa mtumishi wa kudumu atakayekuwa anasambaza
teknolojia kanda ya ziwa Mashariki ," amesema Ishika.
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
amesema maandalizi ya Maonesho ya
Nanenane Kitaifa mwaka 2020 yamefikia
70% na kuongeza kuwa kwa upande wa vipando vimefikia 75%.
Wakati huo huo Sagini
amewaomba viongozi wote wanaotoka kwenye mikoa inayounda kanda ya
ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na Shinyanga) wakiwemo wakuu wa wilaya na
wakurugenzi watendaji kuhudhuria kikamilifu kwenye vikao vya maandalizi
ili yale wanayokubaliana wayatekeleze kwa wakati.
Akizungumzia masuala ambayo bado yanafanyiwa kazi Sagini amesema
kwa sasa kamati ya maandalizi inaendelea na ni ukarabati wa miundombinu
ikiwemo maji ,barabara na umeme huku akiwaomba washiriki kutoa
michango yao mapema ili kufanikisha maandalizi kwa wakati.
Awali akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mara,Mhe.Adam Malima,
Mkuu wa wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri ambaye pia alikuwa
Mwenyekiti wa kikao hicho, ameuhakikishia umma kuwa Maonesho ya Nanenane mwaka
2020 yatakuwa bora zaidi na yataacha alama; kutokana na maonesho hayo kufanyika kitaifa kwa miaka mitatu mfululizo
katika kanda ya ziwa Mashariki.
Katika hatua nyingine mhandisi Msafiri amezitaka
halmashauri zote ambazo hazijaanza na zile ambazo maandalizi yake
yanaenda taratibu, kuharakisha kusimamia maandalizi hayo na kuhakikisha
yanakuwa ya kuridhisha, ili wakulima watakapokwenda kujifunza waone umuhimu wa
kilimo chenye tija.
Kanda ya ziwa Mashariki inaundwa na mikoa mitatu ambayo ni Mara,
Shinyanga na Simiyu na mwenyeji wa
maonesho ya Nane nane kitaifa ni mkoa wa Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo sasa,
ambapo kwa mwaka 2020 kaulimbiu ya
maonesho haya ni "KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”.
MWISHO
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha maandalizi ya maonesho ya nanenane kitaifa mwaka 2020 ambayo yanafanyika kwa mara ya tatu mfululizo sasa katika kanda ya ziwa Mashariki viwanja vya Nyakabindi Bariadi Mkoani Simiyu wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika katika Viwanja hivyo Juni 15, 2020.
0 comments:
Post a Comment