Mrajis wa Vyama vya
Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege amewataka Maafisa Ushirika kuimarisha
usimamizi katika vyama vya ushirika ili kuhakikisha vyama hivyo vinatekeleza
majukumu yake kwa uadilifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu mbalimbali
za ushirika.
Dkt. Ndiege ametoa
agizo hilo wakati akizungumza na maafisa ushirika wa mkoa wa Simiyu katika
kikao kilichofanyika mjini Bariadi wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani
Simiyu Juni 09, 2020.
“Wekeni mpango wa
kuvitembelea vyama vya ushirika ili kuona shughuli zinazofanyika na kuweka
usimamizi imara ili kuondoa dhana ya kufanya uchunguzi, ni bora kugundua tatizo
kabla halijatokea na kulidhibiti kuliko kusubiri litokee na kuanza kuchukua
hatua,” alisema Dkt. Ndiege.
Aidha, Dkt. Ndiege
amewasisitiza Maafisa ushirika kufuatilia makusanyo ya mfuko wa usimamizi na
ukaguzi kutoka Vyama vya Ushirika ili kupata fedha za kusimamia Vyama hivyo, huku
akiwahakikishia kuwa fedha zote za makusanyo zitaendelea kuletwa kwao ili
waongeze usimamizi na kuimarisha Ushirika.
Wakati huo huo Dkt.
Ndiege ameitaka Bodi ya Chama Kikuu cha
Ushirika cha Mkoa wa Simiyu (SIMCU) kuhakikisha inaweka mipango madhubuti ya
utoaji huduma kwa vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) na kuvisimamia kwa
ukaribu zaidi na kuhakikisha vinatekeleza majukumu inavyopaswa.
Katika hatua nyingine
Dkt.Ndiege ametoa wito kwa Bodi ya chama Kikuu cha ushirika mkoa wa Simiyu
(SIMCU) na Chama Kikuu cha Ushirika Shinyanga (SHIRECU) kufanya maridhiano juu ya mgawanyo wa mali ili
kuendeleza uwekezaji katika mali hizo, ikiwemo viwanda vya kuchambua pamba vya
Luguru, Sola na Malampaka vilivyopo Simiyu.
Mwenyekiti wa Bodi wa
SIMCU Bw. Emanuel Mwerere amesema kuwa makubaliano ya mgawanyo wa mali yamechelewa
kutokana na wanachama wa SIMCU kupitia
Mkutano Mkuu kukubali kupokea mali pekee kutoka SHIRECU na hawakuwa tayari kupokea madeni, huku akibainisha kuwa
hawakuchukua viwanda hivyo kwa ajili ya kukwepa hasara katika uendeshaji
kutokana na hali ya viwanda hivyo ilivyo kwa sasa ambayo hairidhishi.
Kwa upande wake Mrajisi
Msaidizi wa Mkoa Bw. Ibrahim Kadudu kupitia taarifa ya Ushirika ya Mkoa amesema
Vyama vya Ushirika vya pamba Mkoani humo vinakabiliwa na changamoto ya malipo
ya ushuru kiasi cha shilingi bilioni 3.9 na bado wakulima zaidi ya 11,047
wanadai fedha zao za pamba kiasi cha shilingi bilioni 3.4.
Naye Meneja wa
Bariadi Teachers SACCOS Bw. Nchimbi Yahya akiwasilisha taarifa kwa Mrajis ameomba
fedha za akiba za wanachama wao zinazoshikiliwa
na Wakurugenzi wa Halmashauri ziweze kurejeshwa, ambapo Mrajis amekiri
kulifahamu suala hilo na kuahidi kulitafutia ufumbuzi.
MWISHO
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU), Bw. Emanuel Mwerere akitoa taarifa ya chama hicho kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(wan ne kulia) wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.
Mrajis msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahim Kadudu akiwasilisha
taarifa ya ushirika mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya Mrajis wa Vyama vya
Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege mkoani humo Juni 09, 2020.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) akichangia Mjumbe wa Bodi ya Shirika la ukaguzi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) akichangia hoja katika kikao cha Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege na wajumbe wa Bodi ya Chama kikuu cha Ushirika cha mkoa wa Simiyu(SIMCU) kilichofanyika Juni09, 2020 mjini Bariadi.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) vya mjini Bariadi (hawapo pichani) wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 09, 2020.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) vya mjini Bariadi wakimsikiliza Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege (hayupo pichani) wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 09, 2020.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Chama kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU), Bw. Emanuel Mwerere mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Chama hicho Mtaa wa Malambo Mjini Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa ushirika wa mkoa wa Simiyu wakati wa zaiara yake mkoani hapa Juni 09, 2020 (wa tatu kuchoto ni Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Simiyu, Bw. Ibrahimu Kadudu.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege (wa sita kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa ushirika na wajumbe wa bodi ya Chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu(SIMCU) mara baada ya kuhitimisha kikao na wajumbe hao wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani humo Juni 09, 2020.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege(wa nne kulia) akizungumza na ushirika na wajumbe wa bodi ya Chama kikuu cha Ushirika mkoa wa Simiyu (SIMCU) wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.
Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege akizungumza na Maafisa Ushirika wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.
Mrajis
wa Vyama vya Ushirika Tanzania Bara, Dkt. Benson Ndiege akizungumza na Maafisa
Ushirika wa Mkoa wa Simiyu(hawapo pichani) wakati wa ziara yake mkoani humo Juni 09, 2020.
0 comments:
Post a Comment