Wednesday, June 24, 2020

MSD YAJIPANGA KUJENGA KIWANDA CHA KUTENGENEZA GOZI NA BANDEJI

Bohari ya Dawa (MSD) inatarajia kujenga kiwanda cha kutengeneza bidhaa za afya zitokanazo na pamba hususani gozi na bandeji katika Mkoa wa Simiyu.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze  wakati wa ziara yake aliyoifanya Juni 24, 2020 mkoani Simiyu kwa lengo  kukutana na viongozi wa mkoa, kuangalia eneo la ujenzi wa kiwanda hicho na kutembelea moja ya viwanda vya kuchambua pamba wilayani Bariadi.

“Kama MSD tutatengeneza gozi, bandeji zile ndogo za vidonda na hata zile pamba za masikioni lakini tutaanza kwa awamu kwanza, lakini naamini bidhaa nyingine za pamba pia tutazitengeneza,” alisema Dkt. Mhidze.

Aidha, Dkt. Mhidze amesema kwa sasa bidhaa hizo zinaagizwa kutoka nje ya nchi hivyo ikiwa zitaanza kuzalishwa hapa nchini kutakuwa na soko la uhakika la bidhaa hizo (vifaa tiba).

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema viongozi wote watatoa ushirikiano wote unaotakiwa na MSD huku akimhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa MSD upatikanaji wa nguvu kazi kwa kiwanda hicho.

Kwa upande wake Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla amemhakikishia Mkurugenzi Mkuu wa MSD upatikanaji wa malighafi ambayo ni pamba hai kutoka kwa wachambuzi wa pamba (ginners ) wa ndani ya nchi na hususani Mkoa wa Simiyu.
MWISHO




 Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla(kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze  aina ya pamba inayoweza kutumika kutengeneza vifaa tiba/bidhaa za afya zitokanazo na pamba wakati wa ziara yake kiwandani hapo Juni 23,2020
 Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla(kulia) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze (wa pili kulia mbele) wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 23, 2020.
 Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla (kushoto) akimuongoza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze (wa pili kulia) na viongozi wengine wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 23, 2020.
 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akitoa taarifa kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel ajili Mhidze (wa pili kushoto ) na viongozi wengine mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi Juni 23, 2020 kwa ya kuangalia mazingira ya ujenzi wa kiwanda cha kutemgeneza bidhaa za afya zitokanazo na pamba.
 Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel ajili Mhidze (kulia) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga mara baada ya kuwasili Mjini Bariadi Juni 23, 2020 kwa ya kuangalia mazingira ya ujenzi wa kiwanda cha kutemgeneza bidhaa za afya zitokanazo na pamba.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) , Brigedia Jenerali Dkt. Gabriel ajili Mhidze (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baaadhi ya watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mara baada ya kuhitimisha mazungumzo na viongozi hao wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu Juni 23, 2020.
 Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla akimuongoza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Brigedia Jenerali Dkt. Gabriel Mhidze na viongozi wengine wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 23, 2020.
 Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze (wa pili kulia) akimweleza jambo Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 23, 2020 kuona hali ya upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya kiwanda cha bidhaa za afya zitokanazo na pamba.
 Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla (katikati) akimuongoza Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze (wa tatu kushoto) na viongozi wengine wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 23, 2020.
 Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla(kulia) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze (wa pili kulia mbele) wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 23, 2020.
 Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla (katikati) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze (wa pili kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 23, 2020.
 Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla (kulia) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze (wa tatu kulia) wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 23, 2020.
 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(wa tatu kulia) akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze (wa pili kulia mbele) wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Juni 23, 2020.

Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginneries Limited kilichopo kata ya Kasoli wilayani Bariadi, Bw. Boaz Ogolla(kulia) akimuonesha Mkurugenzi Mkuu wa MSD , Brigedia Jenerali  Dkt. Gabriel Mhidze  aina ya pamba inayoweza kutumika kutengeneza vifaa tiba/bidhaa za afya zitokanazo na pamba wakati wa ziara yake kiwandani hapo Juni 23,2020

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!