Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka ameujulisha Umma wa Watanzania kuwa Maonesho ya Kilimo na Sherehe
za Nanenane Kitaifa kwa mwaka 2020 yatakuwepo na yatafanyika katika Viwanja vya
Nyakabindi Bariadi na viongozi wakuu wa Kitaifa wanatarajiwa kufungua na
kufunga maonesho hayo ambayo yanafanyika kwa mara ya tatu mfululizo.
Mtaka ameyasema hayo leo Juni 03, 2020 katika kikao cha pamoja kati ya Viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Naibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ambaye yuko mkoani Simiyu kwa ziara ya
siku mbili.
"Kumekuwa na maswali
kwa baadhi ya watu kuhusu Nanenane kuwa itakuwepo au haitakuwepo, nitumie
nafasi hii kuwaambia Watanzania kuwa tumepokea taarifa rasmi kutoka Wizara ya
Kilimo kuwa sherehe za Nanenane Kitaifa mwaka 2020 zipo na zitafanyika mkoani
Simiyu na viongozi wakuu wa Kitaifa watashiriki katika ufunguzi na ufungaji;
mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga inayoandaa sherehe hizi imeanza maandalizi,
taasisi za Umma na binafsi pia zimethibitisha kushiriki na nyingine zimeanza
maandalizi,” alisema Mtaka.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akiteta jambo na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.
Abdallah Ulega wakati alipowasili Mjini Bariadi kwa ajili ya kuanza ziara yake
ya siku mbili mkoani Simiyu, Juni 03, 2020.
0 comments:
Post a Comment