Waziri wa Madini Angela Kairuki
amemwaagiza Mkandarasi anayejenga Kituo cha umahiri cha Madini mkoani SIMIYU,
Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT) kukamilisha
ujenzi ifikapo Januari 2019, ili kiweze kuwasaidia wachimbaji Katika masuala
mbalimbali ikiwa ni kupata mafunzo ya uchimbaji wenye tija.
Kairuki ametoa agizo hilo
alipotembelea na kuona hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Kituo hicho
unaoendelea katika eneo la Nyaumata makao makuu ya mkoa wa SIMIYU Mjini
Bariadi, Novemba 22, 2018.
.
Kairuki amesisitiza usimamizi
uimarishwe zaidi na fedha ziweze kutolewa kwa wakati ili jengo hilo liishe
katika muda uliopangwa, huku akiupongeza uongozi wa mkoa wa SIMIYU kwa kukubali
kutenga eneo la ujenzi wa kituo hicho.
Katika hatua nyingine Waziri Kairuki
amesema Wizara ya madini itahakikisha inawasadia wachimbaji wa chumvi mkoani
Simiyu ili chumvi inayozalishwa iweze kuwa bora na yenye uwezo wa kushindana katika soko, huku akiwakumbusha
wenye leseni za Madini kuzitumia.
“ Kama Wizara tutashirikina na
mkoa wa Simiyu katika kuhakikisha wachimbaji wanachimba kwa tija lakini pia
kuleta migodi ya mifano na namna za nyingine
ya uchenjuaji, pia ikiwemo na hiyo
chumvi, ambayo tutahitaji izalishwe katika ubora, ushindani na kuwekwa katika
vifungashio bora”
“Tuendelee kuhamasisha wachimbaji
wengi zaidi kuendelea kuchimba wasishikilie tu leseni,tunataka kuona ule msamaha
uliotolewa na Mhe. Rais kutoka tozo 16 hadi kufikia tozo 09 kwenye chumvi uwe
na faida kwao” alisema Waziri Kairuki.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi
mwendeshaji kutoka SUMA JKT, Mhandisi Morgan Nyonyi amesema watatekeleza
maelekezo ya Mhe.Waziri na kubainisha kuwa hadi sasa ujenzi wa jengo hilo
umefikia asilimia 35, kufikia Januari 22, 2019 litakuwa limekamilika na mpaka
kukamilika kwa litagharimu takribani shilingi bilioni 1.3.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka uwepo wa kituo cha Umahiri Mkoani hapa
utasaidia kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo na wakubwa wa chumvi katika
Wilaya ya Meatu, pamoja na wazalishaji wengine kwa ujumla ambao watajikita
katika utengenezaji wa chumvi hali itakayosaidia wananchi Simiyu na maeneo
mengine nchini kutumia chumvi itakayozalishwa Meatu badala ya kuagiza kutoka nje
ya nchi.
Ameongeza
kuwa upembuzi yakinifu juu ya uanzishwaji wa kiwanda cha kutengeneza chumvi
wilayani Meatu umeshafanyiwa upembuzi yakinifu na Taasisi ya Utafiti wa Masuala
ya Kijamii na Kiuchumi (ESRF) na unatarajiwa kuwa mradi mwingine mkubwa wa Wilaya
hiyo baada ya mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa.
Aidha,
amesema kukamilika kwa kituo hicho kutachangia kutoa mwanya na fursa kwa
wananchi wa Simiyu kuwa na uwekezaji mwingine(madini) zaidi ya kilimo na
mifugo, huku akibainisha kuwa kitachangia pia kukaribisha wawekezaji wengi
kutokana na kuwepo kwa uhakika wa mahali pa kupata mafunzo na kupima sampuli
mbalimba za madini .
MWISHO
Waziri wa Madini, Mhe.
Angela Kairuki akizungumzana viongozi wa Mkoa wa Simiyu na Shirika la Uzalishaji
Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(SUMA JKT) mara baada ya kutembelea eneo la
Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu kuona hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo hicho
Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018.
Kushoto ni Mtaalam
kutoka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa(SUMA JKT) akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini, Mhe.
Angela Kairuki juu ya hatua iliyofikiwa
katika Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu, wakati alipofanya ziara
ya kukagua ujenzi wa Kituo hicho Mjini Bariadi Novemba 22, 2018.
Waziri wa Madini, Mhe.
Angela Kairuki akiwa na viongozi wengine wakati alipotembelea eneo la Ujenzi wa
Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu kuona hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo hicho
Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka( wa pili kushoto) akimweleza jambo Waziri wa Madini, Mhe. Angela
Kairuki wakati alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Umahiri Mjini
Bariadi Novemba 22, 2018.
Waziri wa Madini, Mhe.
Angela Kairuki(wa tano kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa mkoa wa Simiyu, SUMA JKT na Wizara ya Madini mara baada ya
kutembelea eneo la Ujenzi wa Kituo cha Umahiri cha mkoa wa Simiyu kuona
hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa Kituo
hicho Mjini Bariadi, Novemba 22, 2018.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akizungumza na
Waziri wa Madini, Mhe. Angela Kairuki wakati alipofika ofisini kwake
kabla ya kuanza ziara ya kukagua ujenzi
wa Kituo cha Umahiri cha Mkoa wa Simiyu Mjini Bariadi Novemba 22, 2018.
0 comments:
Post a Comment