Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani amemuondoa Meneja
wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos Mtae katika nafasi ya
umeneja baada ya kushindwa kusimamia usambazaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme
vijijini (REA) wilayani humo na amemwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO
kumpangia kazi nyingine.
Waziri KALEMANI amechukua hatua
hiyo katika mkutano wa hadhara mjini Meatu akiwa katika ziara yake ya kukagua kazi
zinazofanywa na wakandarasi wa mradi wa Umeme vijijini REA awamu ya tatu Septemba
20, 2018, ambapo anaanzia katika uzinduzi wa
mradi wa umeme katika ofisi ya kijiji cha Dakama wilaya ya Meatu.
Dkt. Kalemani ameoneshwa kutoridhishwa
na kasi ya mkandarasi anayesambaza umeme wilayani Meatu ambaye ni kampuni ya
White City, kutokana na kutokuonekana katika vituo na kutokuwa na vifaa vya
kutosha na vituo vya kutosha.
“Kasi ya mkandarasi hapa ni mbovu niliteegemea
nione wakandarasai wanachakarika maana kote nilikotoka nimekuta wanachakarika,
pili nilitegemea nione yadi ya vifaa vya wakandarasi wetu”
“Huyu meneja ndiye msimamizi wa wakandarasi,
namuuliza anasema hajui leo wakandarasi wako wapi sasa anasimamia nini? Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO pokea maelekezo, kuanzia sasa huyu Meneja wa TANESCO
Wilaya mtoe, weka Meneja mwingine kuanzia kesho hapa, wananchi wanataka umeme
hapa” alisema Dkt. Kalemani.
Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani amewahakikishia
wananchi wa vijiji 36 vya wilaya ya MEATU kupata umeme kupitia Mradi wa
Umeme Vijijini (REA) Awamu ya tatu na akawasisitiza kuwa umeme utakapowafikia
wautumie kwa ajili ya maendeleo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema mkoa wa Simiyu
una asilimia sabini ya Mradi wa Umeme wa REA ambapo wilaya ya Meatu
ilikuwa nyuma katika mradi huo ikilinganishwa na wilaya nyingine.
Aidha,
amesema wananchi wa Meatu wakipata umeme utekelezaji wa Sera ya Viwanda utafanikiwa
kwa kuwa wilaya hiyo ndiyo wilaya inayoongoza kwa kilimo cha pamba Tanzania na
ndiyo wilaya inayoongoza kwa kilimo cha alizeti katika mkoa wa Simiyu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum Khamis akizungumza
kwa niaba ya Wananchi wa Jimbo hilo ameishukuru Serikali kwa kufanikisha
utekelezaji wa usambazaji wa umeme katika vijiji vya wilaya hiyo na akaomba
Wakandarasi waongeze kasi ili umeme awafikie wananchi kwa wakati
Naye mwakilishi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Barnabas
Lupande ameahidi kuyafanyia kazi maagizo ya Waziri wa Nishati Dkt Medard
Kalemani aliyoyatoa katika kuakikisha kazi kusambaza umeme kwa wananchi
inafanyika inavyotakiwa.
MWISHO
Aliyekuwa Meneja wa Meneja
wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos Mtae (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati,
Mhe. Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kulia), wakati wa ziara yake wilayani humo
Septemba 20, 2018.
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard
Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika
Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Baadhi ya iongozi wa Wilaya ya Meatu na
Mkoa wa Simiyu wakishangilia mara baada ya Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard
Kalemani kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika
Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard
Kalemani(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake wilayani Meatu
Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Meatu,
Mhe. Salum Khamis wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard
Kalemani wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamishali
wilayani Meatu wakishangilia baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani
kuwatangazia kuwa vijiji vyote katika wilaya yao vitapata umeme kupitia mradi
waWakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu
ya tatu, baada ya uzinduzi wa zoezi hilo katika Kijiji cha Dakama wilayani
Meatu, Septemba 20,2018
Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum
Khamis(kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock Yakobo wakati
wa Ziara ya Waziri wa Nishati , Mhe. Dkt. Merdad Kalemani wilayani Meatu yenye
lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA awamu ya
tatu, Septemba 20,2018.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani
akiwaonesha wananchi wa Kata ya Mwamishali kifaa cha Umeme kiitwacho UMETA ,
alipozungumza nao wakati wa ziarayake wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba
20, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Mhe. Dkt.
Joseph Chilongani akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu,
wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani wilayani Meatu
yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA
awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mwamishali
wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani(hayupo pichani)
alipozungumza nao wakati wa ziara yake wilayani Meatu yenye lengo la kukagua
maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA awamu ya tatu, Septemba
20,2018.
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mwamishali
wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani(hayupo pichani)
alipozungumza nao wakati wa ziara yake wilayani Meatu yenye lengo la kukagua
maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA awamu ya tatu, Septemba
20,2018.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Simiyu kupitia
CCM, Mhe. Leah Komanya akizungumza kwa
niaba ya wananchi katika Kata ya Mwamishali wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati,
Mhe. Dkt. Merdad Kalemani wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya
kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Enock Yakobo akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu
mkoani Simiyu, wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani yenye
lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA awamu ya
tatu, Septemba 20,2018.
Mbunge wa Jimbo la Meatu Mhe. Salum
Khamis akizungumza kwa niaba ya wananchi katika Kata
ya Mwamishali, wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani
wilayani Meatu yenye lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme
wa REA awamu ya tatu, Septemba 20,2018.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Meatu, Mhe.
Juma Mwiburi akizungumza na wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu
mkoani Simiyu, wakati wa Ziara ya Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani yenye
lengo la kukagua maendeleo ya kazi za Mkandarasi wa Umeme wa REA awamu ya
tatu, Septemba 20,2018.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad
Kalemani(katikati mbele) na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Meatu na Mkoa wa
Simiyu wakifurahia jambo wakati wa ziara ya Waziri huyo Septemba 20, 2018
wilayani Meatu.
0 comments:
Post a Comment