Thursday, September 13, 2018

SIMIYU YAANDAA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI, YAAHIDI KUTOA ARDHI YA UWEKEZAJI BURE

Serikali mkoani Simiyu imesema imeandaa mazingira wezeshi kwa wawekezaji katika Fursa  mbalimbali za uwekezaji  ikiwemo viwanda, kilimo na teknolojia, ambapo imejipanga kutoa ardhi bure kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga  ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo , Mhe. Anthony Mtaka katika Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Kiswaga amesema mkoa huo ni mkoa wenye ajenda ya maendeleo, hivyo umejipanga katika kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji katika fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani humo, ikiwa ni pamoja na  sekta ya viwanda, kilimo, tekonolojia mbalimbali, uchimbaji wa visima na fursa nyingine, ili kufikia lengo kuufanya mkoa huo kuwa  katika nafasi nzuri kiuchumi.

“Mkoa wa Simiyu una fursa nyingi mkifika hapa chagueni tu sehemu mje kuwekeza, mtu atakayekuja kujenga kiwanda kikubwa, kizuri ardhi tutampa bure, sisi tutamuuliza tu kwamba tuandike jina gani kwenye hati na tutamkabidhi hati yake, kwa hiyo ATAPE pelekeni salamu kwa wawekezaji wenzenu kuwa ardhi ya uwekezeaji Simiyu ni bure, ninyi mtafute mtaji tu” alisema Kiswaga.

Ameongeza kuwa wawekezaji wote watakaowekeza mkoani Simiyu watapata soko la uhakika la bidhaa zao, huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu na mikoa inayouzunguka ina wakazi wasiopungua milioni 10 ambao watakuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa zao watakazozalisha.

Aidha, Kiswaga ametoa wito kwa wawekezaji wote wakiwemo ambao ni wanachama wa  Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), kuwekeza katika ujenzi wa hoteli na hosteli katika Eneo la Nyakabindi mahali ulipo Uwanja wa Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi ili kukabiliana na changamoto ya malazi.

Katika hatua nyingine Kiswaga ametoa wito kwa Taasisi za Madhehebu ya Dini kuiga mfano wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE) katika  kuwajenga waumini wao kiroho na kuwaimarisha kiuchumi, ili Taasisi kama hizo zitumike kama madaraja kuwavusha waumini wao kueleka katika Uchumi wa Kati.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), Bw. Fredy Manento amesema pamoja na kutoa huduma za kiroho ATAPE inatoa mafunzo ya  ujasiriamali,  imeweza kuwafikia zaidi ya wananchi 20,000 kupitia huduma za afya za bure na imewekeza zaidi ya shilingi milioni 639 katika miradi mbalimbali.

Makamu Mwenyekiti wa ATAPE Taifa (Upande wa Uwekezaji) Dkt. Dastan Kabiaro amesema katika uwekezaji huo ATAPE imeanza na kilimo ambapo  imeshanunua jumla ya ekari 10,250 katika mikoa ya Tanga, Iringa, Pwani , Njombe na inatarajia kupata eneo jingine katika Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kilimo cha miwa ya sukari.

“ ATAPE imeanza kuwekeza katika kilimo,baadaye tutaenda kwenye maeneo mengine ambayo tumeshaanza kama maji, tutatoa visima \Tanzania nzima kwenye  maeneo yote ambayo hayana maji; katika kilimo tumeanza kuchukua ardhi na kuiendeleza mpaka sasa tuna ekari 10,250, tumeendeleza ardhi hiyo kwa asilimia 10 na tunaendelea kuiendelea ardhi hiyo” alisema.

Mwenyekiti wa ATAPE Kanda ya Bariadi, Bi. Mariam Manyangu amesema  mkoa wa Simiyu una wanachama takribani 80, ambao miongoni mwao ni watalaam katika fani mbalimbali pamoja na wafanyabiashara na wanaendelea kuhamasisha waumini wengi kujiunga na chama hicho,  ili kujenga waumini imara kiuchumi watakaoweza  kuendesha maisha yao na kuchangia kazi ya Mungu.

ATAPE  ni kifupi cha Association Of Tanzania Adventist Proffessionals and Enterpreneurs -Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato)-ambacho kilianzishwa mwaka  1999 kwa lengo kuwafanya Wanataaluma na Wajasiriamali watumie talanta zao kwa faida ya Jamii, Kanisa na kazi ya Mungu.

MWISHO

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kulia) akimuonesha kitu Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadiventista Wasabato (ATAPE), Bw. Fredy Manento, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE) Taifa, Bw. Fredy Manento, akitoa taarifa ya Chama hicho wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), wakimsikiliza  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (hayupo pichan) wakati akifungua  Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE) Taifa (Upande wa Uwekezaji) Dastan Kabiaro, akiwasilisha taarifa ya uwekezaji uliofanywa na ATAPE hapa nchini,  wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Mlezi wa ATAPE Jimbo la Southern Nyanza Conference linalojumisha Mikoa ya Geita, Simiyu, Shinyanga na Mwanza, Mchungaji Nicodemo Ntabindi akitoa neno la shukrani mara baada ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga kufungua Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati)  akiwasikiliza viongozi wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), mara baada ya kufungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Wanakwaya ya Kanisa la Waadiventista Wasabato Ntunzu wakiimba wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE)  lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE)  na Wanakwaya wa Ntuzu SDA Choir kutoka Bariadi  baada ya kufungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (mwenye skafu) akiangalia bidhaa zinazotengenezwa na kuuzwa na Wanachama wa wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE)  kabla ya kufungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE) na Watoa mada katika  Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho baada ya kufungua kongamano hilo Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (mwenye skafu) akizungumza  na viongozi wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE)  baada ya kufungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho,  lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (mwenye skafu) akiwa  katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE) na Wanakwaya ya Shamaliwa SDA Choir kutoka jijini Mwanza,  baada ya kufungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), wakiimba wimbo wa Taifa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho, lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (mwenye skafu)  akifurahia jambo wakati akizungumza na viongozi wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), mara baada ya kufungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (mwenye skafu)  akivikwa nembo ya Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), mara baada ya kufungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!