Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania, Bw. Masanja Kadogosa amewataka vijana hapa nchini kuwa ndoto ili
waweze kuona na kuzifikia fursa mbalimbali zilizopo na kukuza Uchumi wao na
Taifa kwa ujumla, kupitia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali ya Awamu ya
Tano katika Sekta mbalimbali.
Kadogosa ameyasema hayo Septemba 14, 2018 wakati akizungumza na Vijana wa
Mkoa wa Simiyu, katika Kongamano la Vijana wa Mkoa wa huo lililoandaliwa na Asasi
ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na
Waliohitimu wanaotoka mkoa wa Simiyu- Simiyu University Students and Associates Association (SUSAA),
lililofanyika Mjini Bariadi .
Amesema Serikali imewekeza fedha nyingi
katika sekta ya viwanda, nishati, ujenzi wa miundombinu kama reli ya
kisasa, barabara na miundombinu ya usafiri wa anga na majini kwa ajili ya
maendeleo ya nchi yetu, hivyo vinana
wanapaswa kuwa na ndoto zitakazowawezesha kuziona fursa ili wajikwamue
kiuchumi.
“Ni jambo muhimu sana kwa vijana kuwa na ndoto kwa sababu wakiwa na ndoto
wataona fursa, ndoto zitawasaidia kufikiria namna ya kujiwekea malengo;
Serikali imewekeza kwenye vitu vingi sana na kutengeneza mazingira wezeshi, ni
wakati wao sasa vijana kutambua nafasi yao katika kuzitumia fursa hizo” alisema.
Aidha, Kadogosa ameshauri makongamano ya Vijana kama lililofanyika Mkoani
Simiyu yafanyike pia katika mikoa mingine na akatoa wito kwa Viongozi na watu
mbalimbali wawe tayari kutoa elimu, ushauri, uzoefu ili kuwajengea uwezo vijana
hapa nchini.
Awali akifungua Kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amewataka vijana
wa mkoa huo kufuata nyayo za wazazi wao katika kuweka jitihada kwenye kilimo
ambapo uzalishaji wa pamba mwaka 2018 umefikia takribani kilo milioni 140
kutoka kilo 70 za msimu uliopita.
Aidha, Kiswaga amesema vijana hao
wajiandae pia katika uwekezaji kwenye viwanda “Sasa hivi Serikali inaenda
kwenye viwanda na hapa naviona viwanda vingi sana hapa naviona viwanda viwanda
vya nguo, naviona viwanda vidogo vingi sana kutoka kwenu, kwa hiyo tujiandae katika kuhakikisha mkoa huu tunawekeza na
wawekezaji ni sisi tuliopo kwenye kongamano hili”.
Kwa upande wake Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Mhe. Luhaga Mpina, ambaye alikuwa miongoni mwa
watoa mada katika kongamano hilo, amewataka vijana hususani wahitimu wa Vyuo Vikuu
kutumia fursa zilizopo hapa nchini
hususani katika sekta ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.
Awali akisoma risala kwa niaba ya Vijana wa Mkoa wa
Simiyu na Viongozi wa SUSAA, Mwenyekiti
wa SUSAA Kanda ya Mashariki, Bw. Musa Joseph amesema lengo kuu la kongamano
hilo ni kuwakutanisha vijana pamoja ili kueleweshana juu ya dhana ya uchumi wa
viwanda nchini na namna kila kijana anavyoweza kushiriki kwa vitendo katika
eneo lake.
Nao baadhi ya Vijana wakiongelea Kongamano hilo wamesema kuwa limewasaidia
fursa kubwa kwao ya wao kupata elimu, ujuzi, na kugundua fursa za uwekezaji na kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri
kuajiriwa.
“ Kongamano hili limetusaidia sana sisi vijana kugundua fursa nyingi za
kuwekeza, kujiajiri ambazo vijana wengi bado hawajaweza kuzitumia katika kuhakikisha
wanajiletea maendeleo, naamini kupitia elimu tuliyoipata leo tutazitumia vizuri
fursa zilizopo, ili tujiletee maendeleo” alisema Emmanuel Lyaganda
Kongamano hili lilihusisha vijana kutoka maeneo tofauti wanaojishughulisha
na shughuli mbalimbali na limeandaliwa
na Asasi ya Vijana walioko Vyuo Vikuu na waliohitimu ambao ni wakazi wa mkoa wa
Simiyu- Simiyu University Students and
Associates Association(SUSAA), likiwa na Kauli mbiu isemayo “
VIJANA NA UWEKEZAJI KATIKA KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA TANZANIA”.
MWISHO
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na
Vijana katika Kongamano la Vijana Mkoa wa Simiyu lililoandaliwa na Wanafunzi
wanaosoma Vyuo Vikuu na waliohitimu ambao wanatoka Mkoa wa Simiyu(Simiyu
University Students and Associates Association -SUSAA), lililofanyika Mjini
Bariadi, Septemba 14, 2018.
Mwenyekiti wa SUSAA
Kanda ya Mashariki, Bw. Musa Joseph akisoma Risala ya Vijana wa Mkoa wa Simiyu
kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe. Festo Kiswaga aliyefungua Kongamano la
Vijana Mkoa wa Simiyu lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wanaosoma Vyuo Vikuu na waliohitimu
ambao wanatoka Mkoa wa Simiyu(Simiyu University Students and Associates
Association -SUSAA), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka lililofanyika Mjini Bariadi,
Septemba 14, 2018.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa wiaya ya Matu mkoani
Simiyu, mhe. Luhaga Mpina akiwasilisha mada katika Kongamano la Vijana Mkoa wa
Simiyu lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi
wanaosoma Vyuo Vikuu na waliohitimu ambao wanatoka Mkoa wa Simiyu(Simiyu
University Students and Associates Association -SUSAA), lililofanyika Mjini
Bariadi, Septemba 14, 2018.
Viongozi na wawasilisha
mada pamoja na viongozi wa SUSAA wakiondoka katika Ukumbi wa Bariadi Alliance
mara baada ya kumalizika kwa Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wanaosoma Vyuo Vikuu na
waliohitimu wanaotoka Mkoa wa
Simiyu(Simiyu University Students and Associates Association -SUSAA),
lililofanyika Mjini Bariadi, Septemba 14, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua Kongamano la Vijana Mkoa wa Simiyu
lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wanaosoma Vyuo Vikuu na waliohitimu wanaotoka
Mkoa wa Simiyu(Simiyu University Students and Associates Association -SUSAA),
kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka lililofanyika Mjini Bariadi, Septemba 14,
2018.
Baadhi ya vijana wa
Mkoa wa Simiyu wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika Kongamano
la Vijana Mkoa wa Simiyu lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wanaosoma Vyuo
Vikuu na waliohitimu ambao wanatoka Mkoa wa Simiyu(Simiyu University Students
and Associates Association -SUSAA), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka lililofanyika Mjini Bariadi,
Septemba 14, 2018.
Mjumbe wa NEC Taifa
kupitia Mkoa waSimiyu ambaye pia ni Mfanyabiashara mkubwa mkoani humo, Bw.
Gungu Silanga akiwasilisha mada katika Kongamano la Vijana Mkoa wa Simiyu
lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi
wanaosoma Vyuo Vikuu na waliohitimu ambao wanatoka Mkoa wa Simiyu(Simiyu University
Students and Associates Association -SUSAA), lililofanyika Mjini Bariadi,
Septemba 14, 2018.
Viongozi wa SUSAA
wakimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga baada ya
kufungua Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wanaosoma Vyuo Vikuu na waliohitimu
wanaotoka Mkoa wa Simiyu(Simiyu University Students and Associates Association
-SUSAA), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka lililofanyika Mjini Bariadi, Septemba 14,
2018.
Kutoka kushoto Waziri
wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli
Tanzania (TRL), Bw. Masanja Kadogosa, Meneja wa Fedha wa AGS , Seleman
Mayongela na Mjumbe wa NEC Taifa kupitia Mkoa wa Simiyu, Bw. Gungu Silanga
wakicheza muziki wakati wa Kongamano la Vijana mkoa wa Simiyu lililoandaliwa na
Umoja wa Wanafunzi wanaosoma Vyuo Vikuu
na waliohitimu wanaotoka Mkoa wa Simiyu(Simiyu University Students and
Associates Association -SUSAA), lililofanyika Mjini Bariadi, Septemba 14, 2018.
Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania (TRL), Bw. Masanja Kadogosa akizungumza na Vijana
katika Kongamano la Vijana mkoa wa Simiyu lililoandaliwa na Umoja wa Wanafunzi wanaosoma Vyuo Vikuu na
waliohitimu wanaotoka Mkoa wa
Simiyu(Simiyu University Students and Associates Association -SUSAA),
lililofanyika Mjini Bariadi, Septemba 14, 2018.
Baadhi yaVijana
wakifuatilia mada mbalimbali katika
Kongamano la Vijana mkoa wa Simiyu lililoandaliwa na Wanafunzi wanaosoma
Vyuo Vikuu na waliohitimu wanaotoka Mkoa
wa Simiyu(Simiyu University Students and Associates Association -SUSAA),
lililofanyika Mjini Bariadi, Septemba 14, 2018.
0 comments:
Post a Comment