Kuelekea
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa amabyo yatafanyika Bariadi
Mkoani Simiyu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Mhe.Ummy Mwalimu amezitaka Halmashauri zote ambazo hazijatenga asilimia kumi ya
mapato ya ndani ambayo ni fedha kwa ajili Wanawake, vijana na watu wenye
ulemavu kuhakikisha zinatenga fedha hizo ifikapo Machi 30, 2020 ili kuyawezesha
makundi hayo kupata mikopo.
Mhe. Ummy Mwalimu ameyasema hayo Machi 05,
2020 wakati wa Uzinduzi wa Maonesho ya shughuli za wanawake wajasiriamali na
jitihada za wadau katika kuwezesha wanawake kiuchumi na kuleta usawa wa
kijinsia, katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Ummy Mwalimu akisaini
katika ubao kwa kutumia chaki zinazotengenezwa Maswa mkoani Simiyu(Maswa Chalks)
wakati wa alipotembelea banda la Maonesho la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa katika maonesho ya wanawake wajasiriamali, taasisi na vikundi
mbalimbali Machi 05, 2020.
0 comments:
Post a Comment