Naibu Waziri
wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe amezindua Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha
Pamba wa miaka mitano (2019-2024) Mkoa wa Simiyu na kuwahimiza wakulima wote
kufungua akaunti za benki kwa kuwa katika msimu ujao Wakulima watalipwa fedha
zao kupitia mfumo wa benki ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za wakulima
yanayofanywa na baadhi ya viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika(AMCOS).
Aidha, Mhe. Bashe amesema Serikali imedhamiria
kuwekeza katika kilimo na kujenga ushirika imara ikiwa ni pamoja na kufufua
baadhi ya Viwanda vya kuchambua pamba(ginneries) vya wakulima kikiwepo kiwanda
cha Luguru wilayani Itilima na viwanda vingine wiwili kutoka wilayani ya Maswa.
Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein
Bashe amezindua Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka mitano
(2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa Shule
ya Sekondari Kusekwa Mjini Bariadi, Machi 05, 2020.
Baadhi ya viongozi na watendaji
wakifuatilia uzinduzi wa Mkakati wa Mapinduzi ya Kilimo cha Pamba wa miaka
mitano (2019-2024) wa Mkoa wa Simiyu, uzinduzi huo ulifanyika katika Ukumbi wa
Shule ya Sekondari Kusekwa Mjini Bariadi, Machi 05, 2020.
0 comments:
Post a Comment