Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa wananchi wa
Kijiji cha Sapiwi wilayani Bariadi kuwa walinzi wa Tawi jipya la Kanda ya Ziwa
la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) linalojengwa katika eneo hilo.
Mhe. Makamu wa Rais
ametoa rai hiyo Machi 06, 2020 wakati alipozungumza na wananchi wa Kata ya
Sapiwi Machi 06, 2020 mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi Ujenzi wa Tawi jipya
la Chuo hicho.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine
wakishangilia mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa wa Tawi jipya la Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Machi 06,
2020.
0 comments:
Post a Comment