Jumla ya Wananchi 17,084 wa kata ya Igalukilo na Vijiji jirani
wilayani Busega wanatarajia kunufaika na huduma za vipimo mbalimbali vya afya
na kupunguza umbali wa kupata huduma hiyo mara baada ya kukamilika kwa Jengo la
Maabara linalojengwa katika Kituo cha Afya cha Igalukilo
Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Busega, Dkt.
Godfrey Mbangali wakati akiwasilisha taarifa ya Ujenzi wa jengo hilo kwa
kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kabla ya
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo hilo.
Pamoja na Jengo hilo Mwenge wa Uhuru umepitia miradi mbalimbali
wilayani Busega ikiwa ni pamoja na Vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita
ya vyoo Shule ya Sekondari Ngasamo, ujenzi wa Jengo la Benki ya NMB na Ujenzi
wa Kisima Kirefu cha Maji Kijiji cha Bukabile.
Aidha, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 amekagua kazi
zinazofanywa na vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu pamoja na
kuzindua klabu ya Wapinga rushwa katika Shule ya Sekondari Kabita.
Baadhi ya wananchi
wakishuhudia Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali, akiweka jiwe la msingi Jengo la
Maabara katika kituo cha Afya Igalukilo, wakati wa mbio za Mweng wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(kushoto) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru, Mkuu wa
wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera, kwa ajili ya kuanza mbio zake wilayani
Busega Mei, 27, 2019.
Jengo la Benki ya NMB
lililopo NYASHIMO, lilowekewa jiwe la msingi wakati wa mbio za Mweng wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za
Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi ambao
ni wanachama wa klabu ya kupinga rushwa shule ya sekondari Kabita, walimu wao
walezi, Mbunge wa Busega, Dkt. Raphael Chegeni
(mwenye shati la kijani) na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera(mwenye
skafu na nguo ya kitenge), mara baada ya kuzindua klabu hiyo Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za
Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali, wakimbiza mwenge wa uhuru wengine na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Busega
wakieleka eneo la kutoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru, mara baada ya kukagua
matundu sita ya vyoo, katika shule ya sekondari Ngasamo, wakati wa mbio za
Mweng wa uhuru wilayani Busega Mei 27,
2019.
Mbunge wa Busega Dkt.
Raphael Chegeni (mwenye shati la kijani) akizungumza jambo na Kiongozi wa mbio
za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali, kabla ya kufungua mradi wa Kirefu
cha Maji Kijiji cha Bukabile, wakati wa mbio za Mweng wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
Kiongozi wa mbio za
Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee
Mkongea Ali akipokea maelezo kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha vijana
wanaotengeneza bidhaa za ngozi wialayni Busega, wakati wa mbio za Mweng wa uhuru wilayani Busega Mei 27, 2019.
0 comments:
Post a Comment