Wednesday, May 29, 2019

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KUWAJENGEA DARAJA BARIADI


Wananchi wa Vijiji vya Ikinabushu na Isuyu wilayani Bariadi wameishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja ambalo limerahisisha mawasiliano na usafirishaji wa abiria, mazao na mizigo kutoka Ikinabushu-Isuyu-Dutwa-Bariadi na Lamadi.

Shukrani hizo zimetolewa mara baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali kufungua daraja la Isuyu Mei 26, 2019

Wananchi hao wamesema kabla ya kujengwa kwa daraja hilo walikuwa wakitumia daraja la kamba na miti na kutozwa fedha.

“ Tunaishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa kutuwezesha kupata daraja sasa hivi watoto wetu wanaenda shuleni kwa raha hata mvua ikinyesha, kabla ya kujenga daraja hili watu walikuwa wanahatarisha maisha” alisema John Maduhu.

“mvua ikinyesha ilikuwa shida kuvuka kwenda Dutwa maana tulikuwa tunatakiwa kuvushwa kwa kamba” alisema Ester Saguda.

Awali akikagua kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa, Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ametoa wito kwa Halmashauri na wawekezaji wengine kutoa kipaumbele kwa wataalam wazawa katika fursa za ajira ili waweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa kati na kulitumikia Taifa.

Akiwasilisha taarifa kwa kiongozi  huyo, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni kuunga mkono utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda kufikia uchumi wa kati na ni mradi wa kujipatia mapato ya ndani.

Ukiwa wilayani Bariadi Mwenge wa Uhuru umepitia miradi minane yenye thamani ya shilingi milioni 700.


Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (wa tatu kushoto) akifungua daraja la Isuyu wilayani Bariadi, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Bw. Melkizedeck Humbe(kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Bw. James John katika Kijiji cha Igaganulwa, Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali  akikagua daraja la Isuyu wilayani Bariadi kabla ya kulifungua, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (wa pili  kushoto) akikagua kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Igaganulwa Dutwa kabla ya kumkaribisha :- Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali (wa tatu kulia) baada ya kukagua kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Sehemu ya Jengo la Kiwanda cha kuchakata alizeti kilichopo kijiji cha Igaganulwa Kata ta Dutwa
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akimtwisha maji mwananchi wa Kijiji cha Msanga B mara baada ya kuzindua mradi wa maji, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.

Hifadhi ya Msitu katika Kijiji cha Sengerema wilayani Bariadi ilikaguliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Mei 25, 2019.
Sehemu ya Bweni lililowekewa jiwe la msingi katika shule ya sekondari Dutwa na Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.
Kiongozi wa Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akikabidhi cheti Klabu ya Kupambana na dawa za kulevya katika Shule ya Sekondari Mwantimba, wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi Mei 25, 2019.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!