Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony
Mtaka leo Mei 09, 2019 amewaongoza mamia ya waombolezaji kutoka Mikoa ya
Simiyu, Shinyanga, Mwanza , Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, katika
mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali
Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambayo yamefanyika katika eneo la Malinoni,
Mtaa wa Kidinda Mjini Bariadi.
Akizungumza na waombolezaji hao kabla ya
kuaga mwili wa Marehemu Dkt.Balele, Mtaka amesema mkoa wa Simiyu unatambua
mchango wa Marehemu katika jitihada za kuanzisha mkoa wa Simiyu na mapinduzi
makubwa aliyoyafanya katika Elimu na kuahidi kuweka alama yake katika mkoa
kumuenzi.
"Uongozi wa Mkoa kwa kutambua
mchango wa Marehemu Dkt.Balele katika kuanzisha mkoa huu na katika mapinduzi ya
Elimu aliyoyafanya wilayani Bariadi akiwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, tunaweka
alama ya maisha yake kama kumbukumbu katika Shule ya Sekondari Majahida ambayo
itabadilishwa Jina kuwa Dkt.Balele Sekondari na Barabara moja katikati ya Mji
wa Bariadi itaitwa Barabara ya Dkt.Balele" alisema Mtaka.
Akisoma Wasifu wa Marehemu, Dkt.Balele
Kapteni Zaharani Masimba wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) amesema
amelitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa zaidi ya miaka 32 na
kutunikiwa medali mbalimbali, ikiwemo ya Vita, Kagera, miaka 20 ya JWTZ, Miaka
40 ya JWTZ, Utumishi wa muda mrefu na Utumishi uliotukuka.
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, Brigedia Jenerali, Robson Mboli Mwanjela
amesema, licha ya Marehemu kustaafu Jeshi, alitumia vizuri taaluma yake ya
Udaktari kuwasaidia watu mbalimbali na kuwataka wananchi wa Simiyu kuiga mema
mengi aliyoyafanya.
"Marehemu atakumbukwa daima kwa
mchango wake mkubwa alioutoa wakati wa utumishi wake jeshini na kwa Taifa
kwa ujumla, katika vyeo na madaraka mbalimbali aliyopewa wakati wa utumishi
wake na hata baada ya kustaafu" alisema Brig. Jen. Mwanjela.
Nao baadhi ya viongozi waliofanya kazi
na Marehemu Dkt. Balele wamemuelezea kuwa alikuwa mwaminifu, mchapakazi, hodari
na mwenye Upendo huku wakitoa wito kwa wananchi Mkoani Simiyu na hapa nchini
kwa ujumla kuyaenzi mema yake.
"Dkt.Balele alikuwa kiongozi halisi
maana alitumia uwezo na ushawishi wake kuwafanya watu wake wawe kama
anavyotamani wawe, alipenda sana Elimu alitaka watu wasome na pengine hata
zaidi yake, ndiye aliyehamasisha Wafanyabiashara kujenga Biashara Sekondari
hapa BARIADI, naomba wana Simiyu tumuenzi kwa kuwekeza katika elimu"
alisema Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Change
"Marehemu Dkt.Balele alikuwa mdau
mkubwa wa Elimu katika kipindi chake alifanikiwa kuanzisha shule za Sekondari
44 Wilaya ya Bariadi na Itilima ambayo pia kipindi hicho ilikuwa sehemu ya
Bariadi, lakini pia wakati wa mpango wa kuugawa mkoa wa Shinyanga alikuwa na
mchango mkubwa wa kuanzisha mkoa wa Simiyu na makao makuu kuwa Bariadi, naomba
tuendelee kuenzi mema yake" Baraka Konisaga, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi
Mstaafu.
Marehemu Dkt.Balele ambaye alikuwa Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga mwaka 2006 hadi mwaka 2011 alizaliwa Desemba 28,
1948 katika Kijiji Cha Kasoli wilayani Bariadi na alipatwa na mauti Mei 02,
2019 katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa
matibabu.
MWISHO
Askari wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiwa
wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Brigedia
Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini
Dar es salaam na kuzikwa Mei 09, 2019
wilayani Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akitoa heshima za
mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt.
Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki
Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam na
kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Kutoka kulia Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo
Kiswaga na Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge wakiteta jambo kabla ya zoezi la
kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga , Marehemu Brigedia Jenerali
Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es
salaam na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani
Bariadi.
Askari wa Jeshi la
Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiweka Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es
salaam na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani
Bariadi.
Kulia
ni Mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali
Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele akiweka shada la maua kwenye kaburi la mume
wake , ambaye alifariki Mei 02, 2019
jijini Dar es salaam na kuzikwa Mei 09,
2019 wilayani Bariadi.
Naibu wa ziri waMadini,
Mhe. Stanslaus Nyongo akiweka shada la Maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele,
ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mchungaji wa Kanisa la
Waadventista Wasabato, Mch.Elias Swita(wa pili kulia) akibariki kaburi ambalo umezikwa mwili
wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu,
Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es
salaam na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani
Bariadi.
Mwenyekiti wa UVCCM
Taifa, Komredi Kheri James (mwenye kofia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na wengine ni baadhia ya viongozi wakiondoka eneo
alilozikwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali
Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es
salaam na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani
Bariadi.
Kutoka kushoto Brigedia
Jenerali Mstaafu, Michael Isamuhyo, Mkuu
wa Mkoa Mstaafu, Njelu Kasaka, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga wakiteta jambo mara baada ya
zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia
Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele kumalizika katika Uwanja wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es
salaam na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani
Bariadi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akiweka shada la Maua
kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia
Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019
jijini Dar es salaam na kuzikwa Mei 09,
2019 wilayani Bariadi.
Kutoka kushoto Mwenyekiti
wa CCM Mkoa Komredi Enock Yakobo, Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Simiyu, Lumen Mathias ,
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Njelu
Kasaka,wakiteta jambo mara baada ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele
kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei
02, 2019 jijini Dar es salaam na kuzikwa
Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi waliofanya kazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia
Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele baada ya zoezi la kuaga mwili wa marehemu
kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye
alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam
na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Kutoka kushoto Mkuu wa
Mkoa Mstaafu, Njelu Kasaka , Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka , Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Komredi Kheri James, Mkuu wa
Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga na
Mbunge wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge wakiteta
jambo mara baada ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga,
Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele kumalizika katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini
Dar es salaam na kuzikwa Mei 09, 2019
wilayani Bariadi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia
zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi
Balele lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye

Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tatu kulia) akiwaongoza wakuu wa wilaya wenzake
kuweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu
Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02,
2019 jijini Dar es salaam na kuzikwa Mei
09, 2019 wilayani Bariadi.
Baadhi ya viongozi
katika ibada kabla ya zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele
kumalizika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei
02, 2019 jijini Dar es salaam na kuzikwa
Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mbunge wa Bariadi, Mhe.
Andrew Chenge akitoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana
Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini
Dar es salaam na kuzikwa Mei 09, 2019
wilayani Bariadi.
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa,
Komredi Kheri James akitoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana
Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini
Dar es salaam na kuzikwa Mei 09, 2019
wilayani Bariadi.
Daktari wa magonjwa ya
wanawake katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Herbert Kairuki akitoa salamu za
rambirambi rambirambi kwa ndugu, jama na
marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali
Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa
marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye
alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam
na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkuu wa Wilaya Mstaafu,
Baraka Konisaga akitoa salamu rambirambi
kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia
Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili
wa marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye
alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam
na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mbunge
wa Bariadi, Mhe. Andrew Chenge na mkewe wakiweka shada la maua kwenye kaburi la
aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt.
Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Reli Tanzania, Bw. Masanja Kadogosa akitoa salamu za rambirambi kwa
ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia
Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili
wa marehemu, lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye
alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam
na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Mwakilishi wa Mkuu wa
Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance
Mabeyo, Brigedia Jenerali Robsob Mboli
Mwanjela akiwasilisha salamu za rambirambi za Jenerali Mabeyo kwa ndugu, jama na marafiki wa aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana
Daudi Balele, kabla ya kuaza zoezi la kuaga mwili wa marehemu, lililofanyika katika
Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini
Dar es salaam na kuzikwa Mei 09, 2019
wilayani Bariadi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia
zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi
Balele lililofanyika katika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, ambaye
alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam
na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
Naibu wa ziri wa Madini,
Mhe. Stanslaus Nyongo akiweka udongo kwenye
kaburi la aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali
Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es
salaam na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani
Bariadi.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akisalimiana na kumpa pole mjane wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa
wa Shinyanga, Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu, Dkt. Yohana Daudi Balele, ambaye
alifariki Mei 02, 2019 jijini Dar es salaam
na kuzikwa Mei 09, 2019 wilayani Bariadi.
0 comments:
Post a Comment