Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu amesema ni vema Sekreatarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma
iendelee kuwakumbusha viongozi na watumishi wa umma nchini kutimiza wajibu wao
ili kuweza kufikia malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli na Serikali.
Mtaka
ameyasema hayo Juni 03, 2019 Mjini Bariadi, wakati akifungua mafunzo kwa
Viongozi wa Umma mkoani Simiyu, ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Rais
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora.
Amesema
ikiwa kila mmoja katika Utumishi wa Umma atatimiza wajibu wake na kwa
kuzingatia mgawanyo wa uongozi ulivyo ndani ya nchi; jamii na nchi kwa ujumla
wake itaweza kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali katika nyanja mbalimbali
kwa wakati.
“Ni
vizuri Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ikiendelea kuwakumbusha watu
wote wanaofanya kazi zinazoihusu jamii kutimiza wajibu wao, kila mmoja
akitimiza wajibu wake yapo mambo mengi sana sisi kama jamii, mkoa na kwa namna
ambavyo uongozi na mgawanyiko wa .nchi yetu ulivyo tutafikia malengo yetu kwa
wakati” alisema Mtaka.
Aidha,
ametoa wito kwa viongozi wa Umma ambao ni watoa maamuzi katika maeneo yao ya
kazi kuwa makini katika kutoa maamuzi na wahakikishe wanafanya maamuzi kwa
wakati.
Kwa
upande wake Kaimu Katibu Msaidizi Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Kanda ya Magharibi Tabora, Bw. Gerald Mwaitebele amesema viongozi wa Umma
wanapaswa kutoa maamuzi kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo
iliyowekwa ili kutoiletea hasara Serikali.
Ameongeza
kuwa Sekretarieti ya Maadili kwa Viongozi wa Umma itaendelea kutoa elimu kwa
viongozi wa umma juu ya umuhimu wa kuzingatia misingi ya uadilifu katika
uongozi na endapo ikitokea kiongozi yeyote atakengengeuka na kutofuata maadili
sheria itachukua mkondo wake.
Kwa
upande wake Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio
ameshukuru Sekretarieti ya Maadili kwa kutoa mafunzo ya maadili kwa viongozi wa Umma na akatoa wito kwa
viongozi hao kuwa waadilifu, kutekeleza majukumu yao na kutojilimbikizia mali
kinyume na taratibu na maadili ya viongozi wa Umma.
Naye
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa
ametoa wito kwa Sekretarieti ya Maadili kwa viongozi wa Umma kutoa elimu ya
maadili kila viongozi wapya wanapoteuliwa au kuchaguliwa, hususani madiwani
wanapochaguliwa na kuunda Mabaraza mapya ya madiwani ili wajue misingiya
uadilifu inayopaswa kuwaongoza katika kazi zao
MWISHO
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na Viongozi wa Umma mkoani humo, wakati
akifungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019
Mjini Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa
Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo
yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019
Mjini Bariadi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akizungumza na viongozi wa Umma
Mkoani humo, wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni
03, 2019 Mjini Bariadi
Kaimu Katibu Msaidizi
Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw.
Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa
mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini
Bariadi.
Afisa Maadili kutoka
Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw.
Onesmo Msalangi akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa
mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi ya Viongozi wa
Umma mkoani Simiyu wakifuatilia mafunzo
yaliyoandaliwa kwa ajili yao na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019
Mjini Bariadi.
Hakimu mfawidhi wa Mahakama
ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Mary Mrio akichangia hoja wakati wa mafunzo
yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo
yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekitia wa
Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe. Robert Lweyo akichangia hoja wakati wa
mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo
yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Katibu Tawala Msaidizi
Seksheni ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Maganga Simon akichangia hoja wakati wa mafunzo yaliyoandaliwa na
Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi
Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019
Mjini Bariadi.
Makamu Mwenyekiti wa
Halamashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe. Bahame Kaliwa akichangia hoja wakati wa
mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo
yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Hakimu wa Mahakama ya
Mwanzo Somanda, Mhe. Said Majaja akichangia hoja wakati wa mafunzo
yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma
Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, ambayo
yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.
Kaimu Katibu Msaidizi
Sekteratieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora, Bw.
Gerald Mwaitebele, akizungumza na viongozi wa Umma Mkoani Simiyu, wakati wa
mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi hiyo, ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini
Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya viongozi wa umma mkoani humo, mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa
na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi
Tabora kwa viongozi hao , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi.

Tabora kwa viongozi hao , ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya waandishi wa habari mkoani humo( waliosimama, kulia ni Afisa Habari Mkoa) ,
mara baada ya kufungua mafunzo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma Kanda ya Magharibi Tabora kwa viongozi wa Umma ,
ambayo yamefanyika Juni 03, 2019 Mjini Bariadi
0 comments:
Post a Comment