Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) Prof. Tadeo Satta amewahakikisha
wananchi wa Mkoa wa Simiyu na mikoa jirani kuwa ujenzi wa awali wa tawi
la Chuo hicho mkoani Simiyu ,unatarajia kukamilika mwezi Septemba mwaka
huu na kuanza kudahili wanafunzi katika mwaka wa masomo 2019/2020 .
Profesa Satta ameyasema
hayo Juni 17, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Tawi la Chuo cha Usimamizi
wa Fedha (IFM) Simiyu katika kijiji cha Sapiwi wilaya ya Bariadi.
Profesa Satta amesema kujengwa kwa kituo hicho
kipya cha mafunzo kutachangia kuongeza udahili na kubainisha kuwa katika mpango mkakati wa chuo
mwaka 2016/2017 hadi mwaka 2020/2021, chuo kimejipanga kuongeza kutoa mafunzo
kwa wateja wake hasa katika mikoa ya Dodoma, Mwanza na Simiyu inayotarajiwa kuchukua
mikoa ya kanda ya ziwa mpaka Tabora.
Ameongeza kuwa azma ya chuo ni kuanza kudahili wanafunzi katika
mwaka wa masomo 2019/2020 kuanzia ngazi ya cheti na matarajio ni kuhamisha wanafunzi wa ngazi
ya cheti na stashahada kutoka Mwanza kuja Simiyu ili Mwanza zibaki kozi za
jioni wanazosoma watu wanaotoka kazini.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amempongeza
Makamu Mkuu wa Chuo IFM, Prof. Tadeo Satta kwa kuwa mtendaji wa mipango aliyoipanga
na kutimiza ahadi ya kuanza kujenga tawi hilo mwaka huu, huku akitoa wito kwa wananchi
wote kuchangamkia fursa mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hosteli,
migahawa na nyumba za kupangisha watumishi.
“Tawi la Chuo cha IFM linajengwa Sapiwi watu wote
wanaalikwa kuchangamkia fursa na wachangamikiaji wa fursa wa kwanza ni wana
Sapiwi wenyewe, tungehitaji kupata hosteli, migahawa ya chakula, maeneo ya watu
kunywa vinywaji na tutawaambia TANROADS waone namna ya kuweka “stendi” maana hapa
Sapiwi kitakuwa kituo kikubwa” alisisitiza Mtaka.
Aidha, Mtaka amewahakikishia viongozi wa Chuo cha IFM
kuwa viongozi wa Mkoa wataendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha azma ya kukamilisha ujenzi
kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuwezesha mkandarasi kufanya kazi saa 24 kwa kuhakikisha
kuna ulinzi na miundombinu ya umeme
inakuwepo katika eneo la ujenzi.
Naye Mayunga Juma Mkazi wa kijiji cha Sapiwi amesema
wananchi wa Sapiwi wanashukuru uwepo wa
ujenzi huo kwani umesaidia kutoa ajira na kuwawezesha kupata fedha za kujikimu
kimaisha.
Kwa upande wake Msimamizi wa Ujenzi huo kutoka Chuo cha
Mafunzo ya Ufundi (VETA) Kagera, Baluye Mitinje ameahidi kusimamia
na kuhakikisha ujenzi unafanyika usiku na mchana ili ukamilike kwa wakati.
Ujenzi wa awali wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha
Tawi la Sapiwi utagharimu kiasi cha shilingi milioni mia tisa na sabini na moja
.
MWISHO
Makamu Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof.Tadeo Satta akitoa maelezo kwa
Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka kuhusu ramani ya majengo
ya Kituo kipya cha chuo hicho kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi wilayani
Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo Juni 17, 2019,
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi
wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFMkinachojengwa Kata
ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini
Sapiwi.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, Prof. Prof.Tadeo Satta akizungumza na
wananchi wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya
Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(kushoto) akifurahia jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha
Usimamizi wa Fedha IFM, Prof. Tadeo Satta wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi
wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya
Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini
Sapiwi.
Mkuu
wa Mkoa wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Sapiwi wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM)
kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni
17, 2019 kijijini Sapiwi/
Baadhi ya wananchi wa
Kata ya Sapiwi Wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka katika hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi
wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu,
iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sapiwi
Wilayani Bariadi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka
katika hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa
Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi
wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini
Baadhi ya wananchi wa Kata
ya Sapiwi wilayani Bariadi wakishuhudia zoezi la uchimbaji msingi wa baadhi ya
majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kinachojengwa Kata
ya Sapiwi wialayni bariadi mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo Juni 17, 2019.
Kikundi cha sanaa
kikitoa burudani katika hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi
wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu,
iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi Mhe. Festo Kiswaga ( mwenye suti ya kahawia) akicheza na baadhi ya
wananchi wa kata ya Sapiwi kufurahia
ujenzi wa kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) , katika hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo hicho kinachojengwa Kata ya
Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini
Sapiwi.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Bariadi, Mhe.Richard Buyamba akizungumza na wananchi
wa Sapiwi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani
Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka( wa nne kushoto) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Ujenzi
wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata
ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini
Sapiwi.
Kaimu Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Donatus Weginah akitambulisha baadhi ya viongozi wa Mkoa huo, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Ujenzi wa Kituo
kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata ya Sapiwi wilaya
ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Baadhi ya wananchi wa
Kata ya Sapiwi wakiangalia ramani ya majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha
Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi
Mkoani Simiyu, mara baada ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi huo iliyofanyika Juni
17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akiwaonesha baadhi ya wananchi wa kata ya Sapiwi ramani ya
majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa katika
Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, mara baada ya hafla ya uzinduzi
wa ujenzi huo iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka( wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Ujenzi
wa Ujenzi wa Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa Kata
ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini
Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka( wa tano kushoto) na baadhi ya viongozi wengine wakizungumza
jambo mara baada ya kukagua eneo
unapochimbwa msingi wa majengo ya Kituo kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha
(IFM) kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati
wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi huo iliyofanyika Juni 17, 2019 kijijini Sapiwi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka(katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya viongozi wa mkoa wa Simiyu na Chuo cha usimamizi wa fedha(IFM), mara baada
ya hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa Kituo kipya
cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kinachojengwa katika Kata ya Sapiwi
wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, wakati wa hafla ya uzinduzi wa ujenzi huo iliyofanyika
Juni 17, 2019kijini Sapiwi.
Baadhi ya wananchi na
viongozi wakishuhudia zoezi la kuchimba msingi wa baadhi ya majengo ya Kituo
kipya cha Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM kinachojengwa Kata ya Sapiwi wialayni
bariadi mkoani Simiyu, wakati wa uzinduzi wa ujenzi huo Juni 17, 2019.
0 comments:
Post a Comment