Wednesday, June 19, 2019

TUZO YA SERENGETI HIFADHI BORA AFRIKA YATAMBULISHWA KWA WANANCHI SIMIYU NA MARA


Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika imetambulishwa rasmi kwa wananchi wa mikoa ya Simiyu na Mara kutoka katika maeneo yanayoizunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Akiitambulisha tuzo hiyo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla Juni 18, 2019 katika Kijiji cha Robanda wilaya ya Serengeti Mkoani Mara, amesema tuzo hii iwe chachu kwa wahifadhi, viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuimarisha shughuli za uhifadhi hapa nchini.

“Tuzo tuliyoipata ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika iwe chachu ya kutufanya tuendelee kuitangaza zaidi Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili tuweze kushinda tuzo ya Kimataifa; Tuzo hii iwe chachu kwetu wahifadhi, viongozi na wananchi wote kwa ujumla kuendelea kuimarisha shughuli za uhifadhi hapa nchini” alisema Kigwangalla.

Ameongeza kuwa Sekta ya uhifadhi ina faida kubwa zaidi ya utalii ambazo ni pamoja na kutoa hewa ya oksjeni kutoka kwenye misitu, kukamilisha mzunguko wa mvua, kutoa mahali pa wanyamapori kuishi na kusaidia zoezi la uchavushaji kwa mimea unaopelekea kuwepo chakula, hivyo shughuli za uhifadhi ziimarishwe zaidi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA kwa kazi kubwa ya uhifadhi wanayoifanya jambo ambalo limeifanya Mamlaka hiyo kutoa msaada kwa jamii, ambapo alibainisha kuwa TANAPA imechangia jumla ya shilingi milioni 100 katika ujenzi wa shule ya sekondari Simiyu maalum kwa ajili ya michezo.

Aidha, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu ni wadau wakubwa wa uhifadhi na unaunga mkono juhuda zote za uhifadhi zinazofanywa na wizara na wadau mbalimbali wa uhifadhi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima amepongeza Kamati za Ulinzi na Usalama ya Mikoa ya Simiyu na Mara kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhakikisha kuwa zinapambana na uharibifu wowote katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti hali iliyochangia hifadhi hii kuonekana bora zaidi katika Bara la Afrika.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga ambaye pia ni mhifadhi amesema tuzo hiyo I matunda ya juhudi za Serikali na wananchi katika kukomesha ujangili na uwindaji haramu na kupitia tuzo hii itachochea watalii wengi kuingia nchini.

Naye Shawezi Silas mkazi wa Kata ya Ikoma wilaya ya Serengeti amesema tuzo hiyo wananchi wameipokea kwa furaha kubwa sana  na imewasaidia kuilewa maana ya uhifadhi na umuhimu wa kuzilinda rasilimali za Taifa ikiwemo wanyamapori.
 MWISHO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (katiakati), Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka(wa pili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adama Malima wakiwaonesha wananchi Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika, katika halfa ya kuitambulisha tuzo hiyo, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
 Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adama Malima, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka, Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Bi. Karoline Mthapula na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliyesimiama mwenye miwani), wakiangalia tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika, mara baada ya kuhitishwa kwa hafla ya kuitambulisha tuzo hiyo kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.



Kutoka kushoto Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adama Malima, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, mhe. Anthony Mtaka, wakiteta jambo mara baada hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika, , iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.



Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za mkoa wakati wa hafla ya kuitambulisha kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. Adam Malima akitoa salamu za mkoa wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.

Baadhi ya viongozi akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakicheza ngoma na kikundi cha burudani kutoka mkoani Mara, wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Mtaalamu kutoka TANAPA akitoa taarifa ya namna tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika ilivyopatikana, wakati wa hafla ya kuitambulisha tuzo hiyo kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe, Pius Machungwa akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wenzake wa Mkoa wa Simiyu, wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simyu, Bw. Adili Elinipenda, mara baada ya kuwasili katika Kijiji cha Robanda kwa ajili ya Kuongoza Hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mhe. Pius Machungwa mara baada ya kuwasilisha salamu wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kushoto) wakifurahi mara baada ya kupokea zawadi ya Ng’ombe dume ambayo imetolewa na wananchi wa Robanda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha rasilimali za nchi zinasimamiwa na kulindwa, wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019


Baadhi ya wananchi wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019

Baadhi ya viongozi akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakicheza ngoma na kikundi cha burudani kutoka mkoani Mara, wakati wa hafla ya kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi  wakati wa hafla ya kuitambulisha kuitambulisha Tuzo ya Serengeti Hifadhi Bora zaidi Afrika kwa wananchi, iliyofanyika katika Kijiji cha Robanda wilayani Serengeti mkoani Mara, Juni 18, 2019.

0 comments:

Post a Comment

Kumbukumbu za Blogu

Powered by Blogger.
Subscribe Via Email

Subscribe to our newsletter to get the latest updates to your inbox. ;-)

Your email address is safe with us!