Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi
Mujungu amewataka wanafunzi walimu na maafisa elimu walio katika kambi ya Michezo
ya UMITASHUMTA Ngazi ya mkoa kudumisha nidhamu wakati wote watakapokuwa katika
kambi hiyo ili Mkoa uweze kufanya vizuri katika michezo na elimu kwa ujumla.
Mujungu ameyasema hayo Juni 12, 2019 wakati
akifungua Mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa katika Shule ya Sekondari ya
Wasichana Maswa, ambayo kwa mwaka 2019 yanaongozwa na Kauli Mbiu “MICHEZO
NA SANAA KWA ELIMU BORA PIA NI AJIRA”.
“Ili tuweze kufanya vizuri katika michezo na Elimu
kwa ujumla napenda kusisitiza nidhamu ya usimamizi wakati wa mashindano, kambi
na ngazi ya Taifa; ni lazima kuwe na nidhamu binafsi kwenu ninyi wachezaji na
wasimamizi wanaowasimamia, kama hakuna nidhamu tusitarajie matokeo mazuri”
alisema Mujungu.
Aidha, Mujungu ametoa wito kwa Wakurugenzi wa
Halmashauri mkoani hapa kuwawezesha Walimu wa michezo kupata mafunzo ili waweze
kujua vema sheria za michezo mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia wanafunzi kufahamu
michezo hiyo na kuamua michezo hiyo kwa haki.
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa Wakurugenzi wa
Halmashauri kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutatua
changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya michezo ikiwa ni pamoja na
upungufu wa miundombinu ya viwanja, walimu wa michezo na ratiba ya michezo kutofuatwa.
Awali akitoa taarifa ya mashindano ya UMITASHUMTA ngazi
ya Mkoa mwaka 2019, Kaimu Afisa Elimu wa mkoa, Mwl. Onesmo Simime amesema
mashindano hayo yatashirikisha michezo ya aina sita ambayo ni riadha, mpira wa
miguu, mpira wa wavu, mpira wa mikono, mpira wa pete(wavulana na wasichana kwa
michezo yote mitano) na fani za ndani.
Kwa upande wake Kaimu Afisa michezo wa Mkoa, Bw.
Charles Maganga amesema kupitia mashindano haya ya UMITASHUMTA mwaka 2019
Walimu kwa kushirikiana na Maafisa Michezo waliopo kambini watahakikisha
wanachagua wachezaji wazuri watakaounda timu ya Mkoa yenye ushindani na
matarajio yao ni kufanya vizuri katika mashindano ya Kitaifa.
Naye mwanamichezo (mwanafunzi) Jeremia Boniface
Jeremia kutoka Halamshauri ya Wilaya ya Bariadi akizungumza kwa niaba ya
wenzake amesema matarajio yao ni Mkoa wa Simiyu kufanya vizuri kwa kuwa
wameandaliwa vizuri na kaahidi kuwa watakuwa na nidhamu wakati wote wa
mashindano hayo.
MWISHO
Kaimu Katibu Tawala wa
Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu akizungumza na wanafunzi wa shule za Msingi
walio katika Kambi ya Mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa
wa Simiyu, Mwl. Onesmo Simime akitoa taarifa ya mashindano ya UMITASHUMTA mwaka
2019 ambayo yanayoendelea katika shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Baadhi ya wachezaji kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA
Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji wa
Mpira wa Miguu kutoka Halmashauri ya Mji wa Bariadi na Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakiwa
katika mashindano ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa ambayo yanaendelea katika shule
ya Sekondari ya Wasichana Maswa.
Baadhi ya wachezaji kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi
Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi
wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi
Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA Kimkoa katika shule ya
Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA
Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Busega wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA
Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Meatu wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA
Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka
Halmashauri ya Mji wa Bariadi wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA
Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya wachezaji kutoka
Halmashauri ya Wilaya ya Itilima wakipita mbele ya Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa
wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu wakati wa Ufunguzi wa mashindano ya UMITASHUMTA
Kimkoa katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wakati wa ufunguzi wa Mashindano hayo Juni 12, 2019.
Baadhi ya Maafisa Elimu
na Michezo mkoani Simiyu, wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa Mashindano ya
UMITASHUMTA mwaka 2019 ambayo yanayoendelea katika shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa,
kutoka kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw. Ekwabi Mujungu(hayupo
pichani).
0 comments:
Post a Comment