Waziri wa Kilimo amewaomba wanunuzi wa pamba
waliopewa leseni na Bodi ya pamba wanunue pamba kwa wakulima kwa bei elekezi ya
shilingi 1200 kama ilivyopangwa na kukubaliwa katika kikao cha wadau wa pamba
mwezi Mei, 2019.
Waziri Hasunga ameyasema hayo Juni 15, 2019 wakati
wa ziara yake Mkoani Simiyu wakati alipotembelea viwanda vya kuchambua pamba,
vituo vya kununulia pamba na kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
“Naomba nitumie nafasi kuwaomba wanunuzi wa pamba
wenye nia njema na nchi hii waliopewa leseni na Bodi ya Pamba waje kununua pamba
kwa wakulima, bei elekezi ya mwaka huu ni shilingi 1200”-alisema Waziri
Hasunga.
Waziri Hasunga amevitaka vyama vya ushirika vya
msingi kuzikagua mizani kwani itakapobainika kufanyika uchakachuaji wakati wa
kupima hatua kali zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, huku akiwahakikishia
wakulima kuwa changamoto zote zilizobainishwa na wakulima katika msimu wa
2018/2019 zitafanyiwa kazi.
Mkulima wa Pamba kutoka Luguru wilayani Itilima, Bw.
Ngusa Lutenganeja ameishauri Serikali kupanga bei ya pamba wakati wa maandalizi
ya msimu ili wakulima walime wakiwa wanafahamu bei na maandalizi ya fedha
yafanyike mapema wakulima wasikopwe.
Kwa upande wake Mnunuzi wa pamba ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Itilima, Mhe. Njalu Silanga amesema imani yake ni kwamba
Serikali itasimamia na kuhakikisha pamba ya wakulima inanunuliwa kwa bei
elekezi ya shilingi 1200/= na wananchi wanapata fedha zao kwa wakati.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema
mkoa wa Simiyu una viwanda vingi vya kuchambua pamba, ambapo ameshauri kuwa ili
kuliongezea thamani zao la pamba Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na wadau wengine kuona uwezekano
wa kujenga kiwanda cha kutengeneza nguo kwa kuwa uhakika wa soko la bidhaa
zitakazotengenezwa upo.
Katibu wa Chama cha Wanunuzi wa pamba nchini (TCA),
Bw. Boaz Ogola ametoa wito kwa Wanunuzi wa pamba kuunga mkono juhudi za
Serikali katika viwanda kwa kuwekeza kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya
pamba ili tusitegemee soko nje ambalo linayumba.
MWISHO
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga(wa pili kushoto) akiangalia baadhi ya mashine za kuchambua pamba
zinavyofanya kazi, wakati alipotembelea kiwanda cha kuchambua pamba cha
Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi, Mkoani Simiyu Juni 15,
2019.(wa nne kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka.
Meneja wa Kiwanda cha
kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi(kushoto)
akitoa maelezo ya aina za mbegu za pamba zinazozalishwa katika kiwanda hicho
kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(wa pili kushoto) na viongozi wengine
wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga(kushoto) akiangali namna taarifa za wakulima zinavyoandikwa mara
baada ya pamba yao kupimwa wakati alipotembelea moja ya Chama cha Msingi Cha
Ushirika (AMCOS)kilichopo kata ya Luguru wilayani Itilima, wakati wa ziara yake
Mkoani Simiyu, Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga akiangalia baadhi ya marobota ya pamba iliyochambuliwa katika
kiwanda cha NGS kilichopo Majahida wilayani Bariadi, mara baada ya kutembela
kiwanda hicho wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, Juni 15, 2019.
Mkurugenzi wa Kiwanda
cha NGS kilichopo Majahida Bariadi ambaye pia ni Mbunge wa Itilima, Mhe. Njalu
Silanga(wa tatu kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga
(wa tatu kulia), na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara ya
Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Baadhi ya viongozi na
wataalam wa mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet
Hasunga(hayupo pichani) wakati
alipozungumza nao katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa kabla ya kuanza ziara yake
mkoani humo, Juni 15, 2019.
Mbunge wa Itilima, Mhe.
Njalu Silanga akiwasilisha kero za wananchi zinazohusu kilimo kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga(kulia)
katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Katika Kijiji cha Inalo Kata ya Luguru
wilayani Itilima, wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Mjumbe
wa NEC kupitia Mkoa wa Simiyu, Mhe. Gungu Silanga akichangia hoja katika kikao
cha ndani kati ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga na viongozi pamoja na
watendaji mbalimbali, wakati wa ziara ya Waziri huyo mkoani Simiyu Juni 15,
2019.
Meneja wa Kiwanda cha
kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani Bariadi(wa pili
kulia) akitoa maelezo ya namna mbegu za pamba zinazozalishwa katika kiwanda
hicho kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(kushoto) na viongozi wengine
wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga,( wa pili kushoto) akiwa na viongozi wengine wa Mkoa wa Simiyu,
wakiaanagalia namna pamba inavyochambuliwa, wakati walipotembelea Kiwanda cha
kuchambua pamba cha NGS kilichopo Majahida Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani
Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga,( wa pili kushoto mbele) akiwa na viongozi wengine wa Mkoa wa
Simiyu, wakioneshwa mafuta yaliyotengenezwa kutoka katika pamba mbegu,,
walipotembelea Kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS kilichopo Majahida Bariadi,
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Meneja wa Kiwanda cha
kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo Kasoli wilayani
Bariadi(aliyechuchumaa) akitoa maelezo ya namna pamba inavyochambuliwa katika
kiwanda hicho kwa Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(kushoto) na viongozi
wengine wa Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa, wakati wa ziara ya Waziri wa Kilimo,
Mhe. Japhet Hasunga,(kulia) mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika
Kijiji cha Inalo Kata ya Luguru wilayani Itilima, wakati wa ziara yake mkoani
Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga,( aliyenyosha mkono) akiwa na viongozi wengine wa Mkoa wa
Simiyu, wakioneshwa mafuta yaliyotengenezwa kutoka katika pamba mbegu,,
walipotembelea Kiwanda cha kuchambua pamba cha NGS kilichopo Majahida Bariadi,
wakati wa ziara yake mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi
ya Pamba, Marco Mtunga(kushoto) akiwaeleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.
Anthony Mtaka(wa pili kulia), Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga,(wa tatu
kulia) na Meneja wa Alliance Ginnery, katika ziara ya WAZIRI Hasunga katika Kiwanda cha
kuchambua pamba cha Alliance Ginnery, kilichopo Kasoli wilayani Bariadi, wakati
wa ziara yake mkoani Simiyu, Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga(katikati) akitoka katika moja ya majengo ya kiwanda cha
kuchambua pamba cha Alliance Ginnery kilichopo wakati wa ziara yake mkoani
Simiyu, Juni 15, 2019.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka akitoa salamu za Mkoa, wakati wa ziara ya Waziri wa Kilimo,
Mhe. Japhet Hasunga,(kulia) mkoani Simiyu Juni 15, 2019.
Waziri wa Kilimo, Mhe.
Japhet Hasunga, Meneja wa Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery na
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakiteta jambo katika ziara ya
Waziri Hasunga katika Kiwanda cha kuchambua pamba cha Alliance Ginnery,
kilichopo Kasoli wilayani Bariadi, wakati wa ziara yake mkoani Simiyu, Juni 15,
2019.
Waziri
wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na Baadhi ya viongozi na wataalam wa
mkoa wa Simiyu katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa kabla ya kuanza ziara yake mkoani
humo, Juni 15, 2019.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi
ya Pamba, Marco Mtunga akifafanua jambo katika kikao cha ndani kati ya Waziri
wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga na Baadhi ya viongozi na wataalam wa mkoa wa Simiyu
katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa kabla ya kuanza ziara ya Waziri huyo mkoani humo,
Juni 15, 2019.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu, Mhe. Enock
Yakobo(kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka,
wakati wa ziara ya Waziri wa Kilimo, Mhe. Japhet Hasunga (hayupo pichani)
mkoani humo Juni 15, 2019.
0 comments:
Post a Comment