Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga amesema
Serikali mkoani Simiyu itaendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na watu wenye
ulemavu wa makundi yote bila kubagua na
kuhakikisha wanapata huduma kwa wakati katika taasisi za Serikali wanapoenda
kupata huduma.
Kiswaga ameyasema hayo Juni 13, 2019 wakati wa
alipofungua kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi Mkoa wa Simiyu, kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, kilichofanyika Mjini
Bariadi.
Amesema watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu
wengine hivyo akatoa wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na maeneo
mengine ya kutoa huduma za jamii mkoani Simiyu kufanya utaratibu wa kuweka
wataalam maalum wenye uelewa wa lugha ya alama ili kuondoa changamoto ya
mawasiliano kwa watu wenye ulemavu hususani viziwi.
“Vyombo vya ulinzi na usalama vihakikishe vina mtu
au watu kwa ajili ya kuwasaidia viziwi kuondoa changamoto ya mawasiliano pamoja
na watu wenye ulemavu kwa ujumla wanaohitaji huduma, si lazima kuajiri kwa sasa
kwa kuwa suala la ajira linaweza kuchukua muda; lakini wahakikishe wana mtu wa
kutoa msaada viziwi wapate huduma” alisema Kiswaga.
Aidha, Kiswaga amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu
kwa viziwi kuhusu maeneo yaliyozuiwa kama vile katika vyombo vya ulinzi
(majeshi) na kushauri kuwa ikiwa wanapaswa kwenda katika maeneo hayo waombe
msaada kwa watu wenye uwezo wa kuzungumza ili kuepuka watu hao kuonekana kuwa
wamevunja sheria kwa kukusudia kwenda maeneo hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi
Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Mhandi Zephania amesema viziwi wanakabiliwa
na changamoto ya mawasiliano wanapoenda kupata huduma mbalimbali hivyo chama
hicho kinaendelea kutoa elimu ya lugha ya alama kwa watumishi wa maeneo
mbalimbali ya kutolea huduma ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Naye Mkalimani wa lugha ya alama Bw. Jonathan
Livingstone amesema Wizara ya Elimu imekubali kupokea jukumu la kusanifisha lugha
ya alama iingizwe katika mitaala ifundishwe katika shule za msingi, sekondari
na vyuo.
Katika hatua nyingine Kamanda wa Wilaya ya Maswa,
Jonas Nyaoga amesema Jeshi la polisi limejipanga kuwahudumia viziwi kwa namna
ambayo wakiwa wanahitaji huduma wanasaidiwa kwa kuhakikisha kuwa kila
wanapowahoji viziwi wanatafuta watu wanaofahamu lugha ya alama ili waweze
kuwatafsiria.
Kikao cha kujadili uboreshaji wa huduma za jamii kwa
viziwi mkoani Simiyu kilijumuisha viongozi wa Chama cha Viziwi(CHAVITA) Mkoa wa
Simiyu, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Kamati za Ulinzi na Usalama za
Wilaya zote tano za Mkoa wa Simiyu.
MWISHO
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi,
Mhe. Festo Kiswaga akifungua kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi
mkoa wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Anthony Mtaka, kilichofanyika
Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mwenyekiti wa Chama cha
Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Mhandi Zephania akitoa taarifa ya
Chama hicho katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa
Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mkalimani wa lugha ya
alama Jonathan Livingstone akifafanua jambo katika katika kikao cha cha
uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13,
2019 Mjini Bariadi
Mkuu wa Jeshi la Polisi
Wilaya ya Maswa, akichangia hoja katika kikao cha cha uboreshaji huduma kwa
jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
:- Mkuu wa Wilaya ya
Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (wa tano kushoto mbele) akiwa katika picha ya
pamoja na wajumbe wa kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa
Simiyu, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi mara baada ya kufunga kikao
hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya
ya Bariadi, Bibi. Veronica Kinyemi, akichangia hoja katika kikao cha uboreshaji
huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi ya wajumbe wa
Kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika
Juni 13, 2019 Mjini Bariadi wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao hicho.
Baadhi ya Viongozi wa
Serikali Mkoani Simiyu na baadhi ya viziwi Mkoani Simiyu wakimsikiliza Bw.
Jonathan Livingstone (mkalimani wa lugha ya alama) wakati akiwasilisha taarifa
katika kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu,
kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya
Meatu, Dkt. Joseph Chilongani akichangia hoja katika kikao cha uboreshaji
huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini
Bariadi.
Baadhi
ya Viongozi wa Serikali Mkoani Simiyu na baadhi ya viziwi Mkoani Simiyu
wakifuatilia masuala mbalimbali yaliyowasilishwa katika kikao cha uboreshaji
huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu, kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini
Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Mhandi Zephania mara baada ya kufunga kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Tanzania(CHAVITA) Mkoa wa Simiyu, Bw. Mhandi Zephania mara baada ya kufunga kikao cha uboreshaji huduma kwa jamii ya viziwi mkoa wa Simiyu kilichofanyika Juni 13, 2019 Mjini Bariadi.
0 comments:
Post a Comment